Ndio nilichomaanisha mkuu.
Nadhani ni uoga na kutokutanguliza maslahi ya taifa mbele, wanaangalia watu ambao hawatawafunika kisiasa.
Obama anasema alikuwa alifanikiwa zaidi kwakuwa alizungukwa na watu makini na waliomwambia ukweli bila kuogopa. Mara kadhaa hadharani alikuwa akimsifia Makamu wake na kusema ni mtu asiye na mchezo. Hapa kwetu hili likitokea ujue upo ndotoni na unapaswa kuamka ili usijikojolee au kutafuna godoro.
Sasa tuliyenae katokea huko na yeye kaleta wa kutokea huko, bila kuwa na PM mkali na asiye na mchezo, pole yetu.
Kibaya tena na huyo PM akileta ukali na kuonesha makali ataonekana anataka kung'aa zaidi ya boss na atafurushiwa huko mbali.😂😂