Imeniuma Sana kuona ng'ombe anakatwa kichwa, sitakula nyama maisha yangu yote

Imeniuma Sana kuona ng'ombe anakatwa kichwa, sitakula nyama maisha yangu yote

Hujawahi kuona nguruwe akichinjwa ,akilia kelele mnasikia Kijiji Cha pili ,ndo maana watu kumwua wanamvizia anapigwa na nyuma ya shoka kwenye uchogo.

Sasa njoo kwa punda ,anapochinjwa huku anajamba.
 
Daah! Hizi comments sasa 😂😂😂😂😂😂
 
Hujawahi kuona nguruwe akichinjwa ,akilia kelele mnasikia Kijiji Cha pili ,ndo maana watu kumwua wanamvizia anapigwa na nyuma ya shoka kwenye uchogo.

Sasa njoo kwa punda ,anapochinjwa huku anajamba.
Punda anachinjwa ili iweje? Huyo ni mnyamakazi.
 
Ndugu Wana Jamiiforums sikujua Kama ng'ombe anachinjwa kikatili vile.
Alilia Sana
Akatoa haja zote
Mwisho alilia machozi
Macho yakageuka rangi huku machozi yakambubujika kwa uchungu.

Imeniuma Sana naahidi kuwa vegan.

Superbug
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”Mwanzo 1:26-28
 
miaka fulani jamaa mmoja alipata kazi kwenye kampuni fulani ya kizungu kwa bahati ikatokea kipindi cha Noel na wazungu wakawa wanafikiria ni kwa jinsi gani wanaweza kuchinja bata mzinga.
jamaa akawajibu simple naweza basi jamaa akenda kwao akakamata kama tulivyozoea kuchicha kuku akawachinjia lakini kilichotokea sasa.
wakamwambia Kazi kwao basi kwa kuwa walimwona ni mtu katili sana.
 
Ukata huu utatuua, mkuu ongeza kipato.
 
Back
Top Bottom