#COVID19 Ina maana muda wote huu Rais alikuwa hajachanjwa?

#COVID19 Ina maana muda wote huu Rais alikuwa hajachanjwa?

Hamna kitu hapo ni danganya toto. Wanachanjwa dawa zingine kuhamasisha uma chanjo. Hakuna rais achome hayo madude. Hata huko Ulaya mbele ya camera inaonesha amechanjwa covid ila ki uhalisia kachoma hizi dawa za kawaida

Ni kutimiza tu masharti.
 
Hamna kitu hapo ni danganya toto. Wanachanjwa dawa zingine kuhamasisha uma chanjo.hakuna rais achome hayo madude. Hata huko ulaya mbele ya camera inaonesha amechanjwa covid ila ki uhalisia kachoma hizi dawa za kawaida .
Ni kutimiza tu mashart.
Ma Mkubwa we utachanjwa?
 
Kuna mtu kakataa?!
Huyu jamaa anayejiita 'nyani ngabu' bado yuko kwenye denial..hataki kuamini kama jembe lao chuma JPM is no more. Hataki kabisa reforms zinazofanywa na SSH na ndio maana kila kukicha anaanzisha thread za kupinga na kudumaza juhudi za marekebisho ya madudu aliyoacha JPM. Watu wa dizain yake sisi tumewabatiza jina la 'sukuma gang'
 
Nyani wakati covid inaanza ulikuwa unasema ipo over rated, lini umebadili gia angani?
 
Msimamo wangu huo haujabadilika mbona…
Chanjo ni hiari, hata huko ulipo, kuna siku ulituonesha certificate yako ya kukamilisha chanjo, sasa kama msimamo wako haujabadilika kwa nini ulichanja kujikinga na ugonjwa ambao ni over rated?
 
Wabongo bwana 😂 ulijuaje corona ilikuisha rasmi ndani ya mipaka ya Tanzania?, takwimu hazikutolewa sasa utajuaje ilitoweka mzehe!!!!!!
Tulihimizwa kusherekea kuondoka kwa corona kwenye kila kona ya nchi. Ilivyofika mwishoni mwa mei 2020, msimamo wa serikali ni kuwa corona ilitokomezwa, ndio maana viongozi wote wa serikali waliacha kuvaa barakoa na kufuata miongozo mingine ya wataalamu wa afya.


 
Chanjo ni hiari, hata huko ulipo, kuna siku ulituonesha certificate yako ya kukamilisha chanjo, sasa kama msimamo wako haujabadilika kwa nini ulichanja kujikinga na ugonjwa ambao ni over rated?
Huelewi!

Ndiyo, chanjo ni hiari. Hakuna mtu anayewekewa mtutu wa bunduki kumlazimisha achanje.

Lakini pia, mtu inategemea na unafanya shughuli gani maishani mwako.

Waajiri wengi sasa hivi wanawataka waajiriwa wao wachanjwe. Ila hawakulazimishi.

Kama hulipendi hilo takwa lao, basi, acha kazi hapo, nenda kwingine.

Mimi nimechanja kwa sababu ya convenience. Kazi yangu inanisafirisha sana.


Chanjo yenyewe ni bure. Wala sijadhurika kwa namna yoyote ile.

Kwa hiyo siyo kwamba nimechanjwa kisa ninaogopa corona. Nimechanjwa kuepuka usumbufu tu maana nyumbani watoto lazima wale na waende shule!

Nikiacha kazi wewe utanilipia ada za watoto shule?
 
Back
Top Bottom