Inadaiwa kuanzia Jumatatu hatakiwi kuonekana machinga yeyote mjini Mwanza

Kutoka hapo walipo ndio kupangwa kwenyewe

Ama what is ur definition ya 'kupangwa'!
 
MTAONDOKA Kwani haya sio maeneo husika na salama na ndani yenu wako vibaka. Tatizo likitokea mnavamia badala ya kusaidia. Huu ni uhuni!

Hivi nanyi mnajiita wafanyi Biashara kweli au WACHUUZI?! Unapangaje matunda barabarani. TANROAD Mko wapi?

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Sheria ni msumeno mkali sana
Pole kwa wamachinga
 
Hilo kaa la moto la wamachinga CCM wamelichochea wenyewe, kwakutengeneza Sera mbovu kwaajili ya kufanya siasa 'uncertainty policy' tumekuwa tukiandika humu waliziba pamba masikio
 
Kila mmoja wetu afuate Sheria za Nchi,hakuna aliye juu ya Sheria haiwezekani mtu alipe Kodi zote stahiki hala ukapange Biashara mbele ya Biashara yake.

Mkijifanya kufanya Vurugu mkono wa dola upo.
Machinga wana mikwara sn wkt hawafati sheria na kodi hawalipi
 
Sis viongozi wa Kariakoo , leo tulikuwa na mkutano na ndugu zetu matching guys, lengo letu ni kutengeneza na kuimarisha taifa lenye uchumi wenye nguvu wa kimachinga
 
Chief hizi hasira ni halali
Ila hazitakusaidia mbele ya mkono wa sheria...jiulize kisheria kama una haki ya kuwa hapo kwenye hilo eneo?una vibali ama ulivamia?.

Kisheria...Kodi haidaiwi kirejareja
Lazima uwe na 'registered place of business',leseni, vibali nk

Kuepusha dhahama
Jiungeni mkodishe fremu maisha yaendelee

Sanasana bomoa bomoa itapita usiku
Hifadhini mali zenu mapema
 
Ikiwa mlio wa bomu la machozi tu watu kukimbia ka swala katimuliwa na chui je bunduki na risasi halisi mtaweza kuhimili?
 
Sis viongozi wa Kariakoo , leo tulikuwa na mkutano na ndugu zetu matching guys, lengo letu ni kutengeneza na kuimarisha taifa lenye uchumi wenye nguvu wa kimachinga
Mnashauriana kufuata taratibu lakini?
Au mna maoni gani kuhusu hilo?
 
Subutuuuu! Wabongo kwa mdomo! Ila matendo O.

Watendaji hawaongeagi. Ni action tu.
 
Machinga wa jiji la Mwanza fanyeni mambo kisomi, mkitumia nguvu mtakwama mapema!
Najua wengi mpo humu....Watafute wabunge wa majimbo ya Ilemela, na Nyamagana pamoja na madiwani wote....waambia bila kuwaonyesha wapi mkafanyie biashara wasahau kura zenu 2025 wasahau....mtafute Mbunge Msukuma Kasheku muombe ushauri wa kiufundi...
TAfuteni wagombea ubunge na madiwani walioondolewa au kushindwa kwa hila 2020 panga nao mbinu za kusamabaza chuki kwa Mabulas kuanzia kwa machinga , mama/baba Lishe.

Mwisho kuweni makini na viongozi wenu....karibia wananuliwa!
 
Tutawashughulikia vizuri nyie wachafuzi wa mazingira.

Serikali iko macho. Jaribuni muone jumatatu mtawasimulia wake zenu kitakachowapata.
 
Lissu aliitisha maandamano yasiyokoma nchi nzima. siku ya kuandamana hata yeye hakuonekana😃😃😃😃
Ndio hapo sasa hao amachinga wametumika sana na mfumo nyonyaji wa nchi. Sasa wajaribu waone.


Kipigo cha mbwa koko chaja.
 
Maendeleo hayana vyama.

Sukuma group watanyoka.
 
Ungekuwa unaijua siasa sasa hivi ungeficha hizi kumbukumbu mbovu, ungejifanya unasikitika nao ili hatimaye wakuone wewe una afadhali kuliko washindani wake. Siasa ni mchezo wa mahesabu ya kimkakati, kuvizia hisia za watu dhidi ya mshindani wako.
Hatuko kwenye siasa za opportunistic. Hao unawalilia leo kesho wanakugeuka.

Twende hivyo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…