Inadaiwa Lazaro hakufa bali alipewa dawa akalala usingizi mzito, baada ya saa 72 akaziduka huku Yesu akija na kudai kumfufua

Yohana 11: 17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.

Bwana Yesu alilia machozi zaidi ya mara tatu kabla ya kumfufua Lazaro.
Hakuna aliemuhoji lazaro aliona nini huko baada ya kifo chake
 
Mhh tuache haya mambo
 
Yohana 11: 38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

-----------
Unataka ushahidi gani zaidi ya maandiko hayo yanavyo shuhudia???
Maandiko yanasema wazi Lazaro alikuwa maiti siku nne, Lazaro alikuwa maiti inanuka (imeanza kuoza)

Acha story za vijiweni mwamini Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wako
 
Story za wahuni wa Roma😁
 
Utashambuliwa, ila uliloliwakilisha linaweza kuwa na ukweli mkubwa kabisa.
 
"Inadaiwa na nani" Hz akili hz
 
Naona umebambikiwa sentensi na bahati mbaya fuvu liko empty ukaleta humu bila tafakuri

Nalaaabukk
 
Yaani wewe wa leo ndio unajifanya unaweza kuthibitisha kulala, kufa au kuoza kwa mtu. Acha hizo, huo ni utoto.
Tatizo walioandika hayo yote walikuwa ni wale inner circle ya Yesu, inawezekana kabisa wakashuhudia uongo ili kuhalalisha walichokuwa wakikiamini kwa waliyekuwa wakimfuata na kumtii. Ukisoma maandiko ya wengine wa nyakati hizo (waliokuwa si wanafunzi wa Yesu) kama ya Josephus utaona hadithi tofauti tofauti.
 
Hata Mwamposa anaponya magonjwa yaliyokosa tiba na wafuasi wake wanashuhudia kupona.
 
Yesu alikufa kwa kuwambwa msalabani, ila kwenye kufufuka tulipigwa changa la macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…