Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Halafu wazazi wenye mtazamo wa kuja kulelewa na watoto, mara nyingi huwa hawawajibiki ipasavyo kulea watoto wao.Mtoto kumlea mzazi wake ni yeye aamue tu lakini hawajibiki moja kwa moja kumlea.
Sana sana wanawake wa kichagga..Hili ulilosema nalo huchangia sana vwatoto kuwasahau wazazi wao,akisha zama katika penzi la mke basi anamsahau hata mzazi wake
Kabisa, na mtoto kumlea mzazi ni hisani tu ya mtoto, na ukijiona huna uwezo wa kulea watoto na uwezo wa kujilea uzeeni ni heri usizae!Watoto iwe second au third option na sio first..
Kweli kabisa mkuu..Kabisa, na mtoto kumlea mzazi ni hisani tu ya mtoto, na ukijiona huna uwezo wa kulea watoto na uwezo wa kujilea uzeeni ni heri usizae!
Kiukweli kabisa mzazi ana wajibu wa kumlea mtoto.Nakubaliana na wewe juu ya hoja yako
Lakini
Kuna wengine wamepata malezi mazuri ila baada ya kuwa na ndoa zao basi kila kitu kinabadilika
View attachment 3188476
Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu
Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao
Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu
Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia
Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao
Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo
Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi
Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo
Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako
Ni hayo tu!
VIpi kwa ambao hawajaoa wala kuolewa lakini wana wakataa wazazi,Sasa tupo pamoja.
Mtoto aliyelelewa na kutunzwa kwa moyo mmoja na wazazi wake kisha akaja kuwatelekeza ukubwani mara nyingi (sio zote) huwa anakuwa anatawaliwa na mke wake.
Yaani anatunza sana ndugu wa mke kuliko ndugu zake na ikitokea amefilisika mke anamkimbia na ndugu wa mke pia wanamzimia simu.
KATAA NDOA.
Ni kweli hii ya mtoto kumtajirisha mzazi au kutwishwa wajibu wa mzazi wake imekuja na ile ya WAUMINI WA DINI KUWATAJIRISHA VIONGOZI WAO WA DINI IWE NI WANAO JIDAI UTUME AU UNABII AU UINJILISTI NK ,,,ni pakeji za kiseng3 kabisa ...ccm ni mafiiiiMzazi ndiye anatakiwa kuachia watoto urithi. Waafrika na watu wengi duniani wameishi hivyo kwa miaka mingi sana. Hii ya kusaidia wazazi kimali imekuja juzi juzi tu.
Kuna tukio kubwa walifanyiwa na hao wazazi na sasa it's a pay back time. Wanalipa kisasi..VIpi kwa ambao hawajaoa wala kuolewa lakini wana wakataa wazazi,
Mkuu uko sahihi,Wakuu waliotoa hoja hapo juu wako sahihi sana ya kwamba, Sio Majukumu ya mtoto kumlea mzazi, Ukizaa manake una means ya kulea hao watoto, pia mzazi jiandalie maisha yako ya uzeeni, Usitegemee watoto!
Una hoja katika hilo,,,lakini je kwa watoto mlio zaliwa wengi pamoja na kuwa na majukumu yenu ya kulea familia zenu,watashindwa kuchangia kidogo kidogo na kulea wazazi wao?Kiukweli kabisa mzazi ana wajibu wa kumlea mtoto.
Na mtoto akikua akioa na yeye ana wajibu wa kumlea mtoto wake.
Ukitaka mtoto amlee mzazi unaharibu order.
Mzazi anatakiwa kulea watoto huku akijiwekea akiba ya uzeeni.
Mtoto alee mtoto wake na mzazi wake na hapo hapo ajiwekee akiba ya uzeeni hapo ndiyo unaanza kualika ufisadi watu waibe pesa ili kulea wazazi, watoto, kujiwekea akiba.
Mzazi anayemtegemea mtoto wake amlee uzeeni, huyo mtoto akifa kabla ya mzazi itakuwaje hapo?
This happens quite a lot nowadays.
Kuna namna watu wa namna hii waliumizwa na wazazi wao. Mimi mama yangu sijazungumza naye sasa ni mwaka mmoja na miezi 5 (miezi 17 jumla)....Tuje kwa hawa wengine watu wazima lakini wamewatenga wazazi wao kiasi kwamba hadi majirani na watu wa karibu wanaingilia kati lakini wapi,
So tunaconclude kwamba hakuna mwenye makosa, ni wazazi wanalipia karma zao kwa matendo kadha wa kadha waliyowafanyia watoto wao?Kuna tukio kubwa walifanyiwa na hao wazazi na sasa it's a pay back time. Wanalipa kisasi..
Baadhi ya watu wanataka kuleta huruma za kijinga humu. Mkuu, watu wanasema kwa sasa mimi ni cold heart sana. Yaani mimi wa mwaka 2019 na mimi huyu wa mwaka 2024 ni watu wawili tofauti kabisa.Wao hawa wazazi wasiolelewa je walilea wazazi wao?
Duuh, i feel sorry for you😥Kuna namna watu wa namna hii waliumizwa na wazazi wao. Mimi mama yangu sijazungumza naye sasa ni mwaka mmoja na miezi 5 (miezi 17 jumla)....
Boss wangu,kichwa cha uzi kinajieleza wazi kwamba inakuwaje mzazi anaweza lea watoto wengi lkn watoto wanashindwa kulea mzazi wao,hatujatofautiana hapoTumia akili hata huyo mtoto atalea watoto wake kibao ...tumia akili jibu lipo umelitamka mwenyewe labda ungesema inakuwaje mzazi kalea watoto kibao ila hao watoto wanashindwa kulea watoto wao kibao.
Katika suala la PESA YANGU mimi sinaga msalie mtume. Kwanza tambua hilo. Mtu anayecheza na pesa yangu, hata kama ni mzazi wangu, atageuka kuwa adui on the spot. Kwangu mimi wa kwanza Mungu, wa pili mimi mwenyewe, wa tatu, PESA/HELA YANGU alafu wengine ndio wanaofuata...So tunaconclude kwamba hakuna mwenye makosa, ni wazazi wanalipia karma zao kwa matendo kadha wa kadha waliyowafanyia watoto wao?
Em tujaribu kugeuza kioo, means kuanzia ukiwa mdogo hujawahi kuwakwaza wazazi wako kwa namna yoyote ile?,. Na kwanini uwe mzito kumsamehe mzazi aliyakua nawe yapo mengi mlimkwaza kwa kujua ama kutokujua na alipiga moyo konde kukukuza mpaka umefika ulipo?
Una msimamo mkali sana,. Ila ni vizuri as long as unaishi kwa amaniKatika suala la PESA YANGU mimi sinaga msalie mtume. Kwanza tambua hilo. Mtu anayecheza na pesa yangu, hata kama ni mzazi wangu, atageuka kuwa adui on the spot. Kwangu mimi wa kwanza Mungu, wa pili mimi mwenyewe, wa tatu, PESA/HELA YANGU alafu wengine ndio wanaofuata...
Siwezi kuogopa jitu jehu kama wewe , Nina mambo mengi ya msingi ndio maana Nakuwa nakupuuza . Uwezo ninao wa kula sahani Moja na wewe jino kwa jino.ushakwisha dawa yako kama unataka kupona omba msamaha humu hadharani. La sivyo hata hayo masomo yako nitayakatisha.
Sipendi upuzi