SIPENDI SIASA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 791
- 1,199
Alinitelekeza baada ya kustaafu na kupewa kiinua mgongo cha 70 millions. Alikuwa na deni langu, kwa jeuri tu hajanilipa..Duuh, i feel sorry for you😥
But sidhani kama hiyo itakua sababu ya kushindwa kumhudumia akihitaji msaada wako wakati wa matatizo yake?
Just prove us wrong
Aisee, haya mambo ni magumu sana 🙌🙌Alinitelekeza baada ya kustaafu na kupewa kiinua mgongo cha 70 millions. Alikuwa na deni langu, kwa jeuri tu hajanilipa..
Heshima ni two way traffic. Haunipi heshima, na mimi sikupi. Just like that..
Huenda umepitia mazingira fulani ambayo yamekufanya uwe hivyo,inaweza kuelewekaBaadhi ya watu wanataka kuleta huruma za kijinga humu. Mkuu, watu wanasema kwa sasa mimi ni cold heart sana. Yaani mimi wa mwaka 2019 na mimi huyu wa mwaka 2024 ni watu wawili tofauti kabisa.
Experience can turn a sheep into a wolf..
Ni Majukumu yako Kumlea mwanao tena malezi mazuri, ambayo atapata mahitaji yake ya msingi kama Ellimu, afya, Mavazi na Malazi. Hii haimaanishi umewekeza kwake, Huu ni wajibu wake. Yeye kuja kulipa kwa kukutunza ni utashi wake na Hisani yake ila si lazima. Wewe ndiye ulichagua azaliwe, yeye hakuwa na option ya kuzaliwa.Mkuu uko sahihi,
But incase hukufanikiwa kujiandalia maisha yako mazuri na ulijitahidi kwa kila namna kuwaweka wanao mahali pazuri na wamekuwa,
kWahiyo huzistahili japo kidogo fadhila za wanao?🤔
Nilikuwa ninawasaidia saana watu from 2015 mpaka 2019 December. Nilifilisika 2020 mpaka sasa sijainuka financially, hakuna rangi sijaacha kuona kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Sasa nimejifunza kuwa roho mbaya inalipa kuliko kuwa mtu mwema..Una msimamo mkali sana,. Ila ni vizuri as long as unaishi kwa amani
Umenifafanulia vizuri sana,Ni Majukumu yako Kumlea mwanao tena malezi mazuri, ambayo atapata mahitaji yake ya msingi kama Ellimu, afya, Mavazi na Malazi. Hii haimaanishi umewekeza kwake, Huu ni wajibu wake. Yeye kuja kulipa kwa kukutunza ni utashi wake na Hisani yake ila si lazima. Wewe ndiye ulichagua azaliwe, yeye hakuwa na option ya kuzaliwa.
Ki Africa tunadhani ni wajibu wa mtoto kumlea mzazi ila sio kweli. Tujitahidi sisi kama wazazi tutengeneze maisha Bora ya wanetu huku tukijitengenezea kesho yetu pia.
I wish you the same. I'm no longer a human being. I'm a lion as of now. No more mercy kwa walioninyanyasa..Aisee, haya mambo ni magumu sana 🙌🙌
Hope you found peace and you good🤝
Duh kwahiyo kwako wewe pesa mbele ya utu si chochote,kwa tafsiri nyingine umeiweka pesa mbele sanaKatika suala la PESA YANGU mimi sinaga msalie mtume. Kwanza tambua hilo. Mtu anayecheza na pesa yangu, hata kama ni mzazi wangu, atageuka kuwa adui on the spot. Kwangu mimi wa kwanza Mungu, wa pili mimi mwenyewe, wa tatu, PESA/HELA YANGU alafu wengine ndio wanaofuata...
Wazazi wanatakiwa wajiandae kwa maisha ya uzeeni, mambo ya kusubiria watoto waje kuwalea ni kuzidisha tu mnyororo wa umaskini.Unatambua hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha,je pale wazazi wako wanapokosa nguvu ya kujitafutia unataka nani awatunze?
Tuache kuwa na fikra na tamaduni za kimagharibi kutaka wazazi wetu wakatunzwe katika nyumba za wazee
Acha tu mkuu. Inatisha..Huenda umepitia mazingira fulani ambayo yamekufanya uwe hivyo.
Hili pia mimi nimejifunza in a hard way, japo wazazi wangu always wako upande wangu and i always thank Lord for that🙏Nilikuwa ninawasaidia saana watu from 2015 mpaka 2019 December. Nilifilisika 2020 mpaka sasa sijainuka financially, hakuna rangi sijaacha kuona kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Sasa nimejifunza kuwa roho mbaya inalipa kuliko kuwa mtu mwema..
I Understand youI wish you the same. I'm no longer a human being. I'm a lion as of now. No more mercy kwa walioninyanyasa..
Hongera sana kama una wazazi wanaokujali, hongera sana mkuu. Ninapanga siku nikiinuka financially, mirathi yangu sitaandika mzazi hata mmoja..Hili pia mimi nimejifunza in a hard way, japo wazazi wangu always wako upande wangu and i always thank Lord for that🙏
Thanks too..I Understand you
Thanks🤝
Kama ulivyosema maisha yamebadilika sana,hizo rasilimali za wakati huo hazipo tena,kwahiyo inabidi tuishi kuendana na wakati sasaWazazi wanatakiwa wajiandae kwa maisha ya uzeeni, mambo ya kusubiria watoto waje kuwalea ni kuzidisha tu mnyororo wa umaskini.
Zamani wazazi walikuwa wanamiliki mashamba na mifugo mpaka uzeeni, vinatumika kuwahudumia wakiwa wazee na wanawawaachia watoto wao urithi, sasa hivi hayo mambo yanazidi kuisha. Watu wanaishi mijini maisha yao yote wanategemea kibanda cha matunda, fremu ya kuuza sukari na maji mtaani, vibarua n.k.
Sio majukumu ya mtoto kumlea mzazi maana na yeye anamajukumu ya kulea watoto wakeView attachment 3188476
Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu
Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao
Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu
Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia
Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao
Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo
Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi
Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo
Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako
Ni hayo tu!
Pole sanaAcha tu mkuu. Inatisha..
Thanks..Pole sana
Nawewe umejizaa!Mimi nadhani Mungu awasamehe sana wanaoshindwa kuwalea watoto wao.
Mimi wajibu wangu ni kulea niliowazaa. Wazazi mimi sijawazaa.