Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Afu ujue kabudi anapigiwa kampeni wazi wazi tena kwao kilosa, Baba wa kabudi alikaa kilosa kama mwinjilisti ndio jamaa kazaliwa kule lakini ni mgogo leo hii anaitwa mtu wa kilosa na jimbo anapewa na hana hata kibanda pale anafikia hotel
Nyumba si inaweza jengwa ndani ya mwezi mmoja? Mpeni Prof. Ubunge wa jimbo huenda akapewa nafasi kubwa zaidi ya aliyonayo
 
Mimi naamini hakuna mtu wa kuzuia ndoto ya mwingine
Ndiyo kapatikana sasa hata kugombea wanaccm wanalazimika kuomba ruhusa kwa Yesu wao.

Sikutegemea kama nchi ndani ya miaka mitano itakuwa imefikia huku.
 
Nimejiuliza, Rais wetu mpendwa alipokuwa Mwalimu pale Sengerema Secondary School, alipoomba Ruhusa ya kwenda kugombea Ubunge kule Biharamulo. Je, aliachishwa kazi? Watu wanaomba ruhusa ili wakajaribu bahati zao, badala ya kupewa ruhusa wanatumbuliwa. Hii mnaionaje raia?

Binafsi naona sio sawa jamani au kwa vile ni nafasi za kuteuliwa? Najiuliza wale wa kwenye sector zisizo za kuteuliwa i.e watumishi wengine mfano walimu n.k wakiomba ruhusa nao wataachishwa kazi badala ya kupewa ruhusa. It means ukishindwa imekula kwako.

Hii ndo Tanzania ya Magufuli.
Kila zama na vitabu vyake. Achia nafasi nenda kagombee, kuna watu wana elimu kazi hawana,waachie wewe nenda kagombee
 
Nimejiuliza, Rais wetu mpendwa alipokuwa Mwalimu pale Sengerema Secondary School, alipoomba Ruhusa ya kwenda kugombea Ubunge kule Biharamulo. Je, aliachishwa kazi? Watu wanaomba ruhusa ili wakajaribu bahati zao, badala ya kupewa ruhusa wanatumbuliwa. Hii mnaionaje raia?...
Walimu nao ni wateule wa mkulu?
 
This is not fair. Kamishina wa Elimu angemnyima ruhusa enzi zile,mpaka sasa si angekuwa anakamata chalk ?
Nimemsikia ITV live Magu akiwapiga vijembe vya RUKSA kwa wale wanaotaka kutia nia.Lakini sijui kama wataambulia kitu.Mchezo ndio kwanza umeanza.
 
Sasa wakati wewe umeomba ruhusa huku nyuma kazi zako afanye nani? Serikali hii umeshaambiwa kauli mbiu yake ni HAPA KAZI TU?

Mtumishi wa uma ana haki ya kupata ruhusa ama likizo wakati wowote akiwa na uhitaji. Haondoki na ofisi.
Kuhusu kutia nia inajulikana kwa waliopo katika nafasi za utumishi wanatakiwa kuacha kazi wakishapitishwa na vyama vyao (kama wanatenguliwa sasa hivi basi ni maamuzi ya mamlaka za uteuzi wao)
 
Kama kweli akina Ally Happi na genge lake ni vidume, wajitose sasa kugombea Ubunge tuone. Shenzy kabisa.
 
Hujui lolote. Kwanza Magufuli hakuwa anafundisha Iringa,pili Magufuli kishawahi kushindwa kura za maoni kule Biharamulo mara mbili,hadi lilipogawanywa ndo akaja akapita kura za maoni .Naona unaleta story za vijiweni kwenye Gahawa.

Exactly aliyemshinda alikua marehemu kabuye, katika dunia hii uambiwe uridhike na ulipo na wewe ukubali tayari umekubali kutawaliwa fikra na mtu mwingine na matokeo yake ndio leo unashangaa tunaambiwa mara ni yesu, mara mbeba maono na lugha nyingine za namna hiyo
 
Inafaa sasa Gwajina naye atumbuliwe kwa kuacha kazi ya Uaskofu na kukimbilia ubunge. Prof.Kabudi na PhD Kitila Mkumbo wapate mkasi au krosi kwa kukimbilia ubunge ili hali wamekalia ofisi za umma.

Walimu na watumishi wote wa umma wanaojipanga kutia nia na kugombea watumbuliwe mapema ili nafasi zao ziwe wazi vijana wapewe ajira.

Ni suala la kuwa moto au baridi na siyo vuguvugu, ndiyo maana Mhe Lukuvi na wenzake waliondolewa kamati kuu na kwenye kamati ya maadili ya chama.

Mtu mmoja nafasi moja, haya ndiyo maelekezo ya CCM. Hatutatarajia kuona kunakuwa na ubaguzi ktk kusimamia haki kwa wote.
Kazi njema.
 
Hujui lolote. Kwanza Magufuli hakuwa anafundisha Iringa,pili Magufuli kishawahi kushindwa kura za maoni kule Biharamulo mara mbili,hadi lilipogawanywa ndo akaja akapita kura za maoni .Naona unaleta story za vijiweni kwenye Gahawa.
Sawa Mimi Sijui lolote wewe unajua inaonekana upo jikoni, Subiri teuzi.
 
Kashasema inategemea ameamkaje. Sasa nini tena tunataka kwa jiwe. Tusubiri akiamka vizuri.
 
Ilikuwaje Magufuli alipoenda Biharamulo akashindwa kura za maoni then akarudi kushika chalc ?What about Dr Mwele mwaka 2015 aliomba ruhusa kwenda kugombea Urais aliposhindwa akarudi kwenye ukurugenzi wake?
Kuna kuomba kibali UTUMISHI kama unataka kugombea. Ukishapitishwa na chama chako kama mgombea, utumishi wako unakoma
 
Magufuli Alichaguliwa na Mkapa kugombea ubunge 1995, Baada ya Mkapa kupita Chato na kuona pako very Primitive, ndiyo akauliza ninani anaweza kuwa mbunge ambaye anatoka pale kjijini, ndiyo wazee wakampendekeza Magufuli kipindi hicho Ni Mwalimu iringa.

Note: Tofautisha Kuomba Ruhusa na Kuchaguliwa.
Mkapa alipita chato huo mwaka 1995 kama nani kiasi cha kuona pako primitive na kumchagua magufuli kugombea ubunge?
 
Afu ujue kabudi anapigiwa kampeni wazi wazi tena kwao kilosa, Baba wa kabudi alikaa kilosa kama mwinjilisti ndio jamaa kazaliwa kule lakini ni mgogo leo hii anaitwa mtu wa kilosa na jimbo anapewa na hana hata kibanda pale anafikia hotel
Huyo si mkaguru+mgongo, Ndiyo akajenge Sasa mwenzake mkulo yuko huko na Ana mji wake pia

Ova
 
Acheni tamaa wengine hawana ajira bado mnawazongazonga mtaka yote hukosa yote. Hii inaonyesha wazi kwamba mnafanya kazi ambazo.

Sio profession zenu. Wewe ni mwalimu alafu unataka siasa basi ualimu sio profession yako unaganga njaa tu alafu unalaumu.
Mkuu hivi Magufuli si alikua Mwalimu na aligombea mara mbili akashindwa lakini aliendelea na ualimu baadae? Au Historia ya huku imebadirika tangu 2015?
 
Nimejiuliza, Rais wetu mpendwa alipokuwa Mwalimu pale Sengerema Secondary School, alipoomba Ruhusa ya kwenda kugombea Ubunge kule Biharamulo. Je, aliachishwa kazi? Watu wanaomba ruhusa ili wakajaribu bahati zao, badala ya kupewa ruhusa wanatumbuliwa. Hii mnaionaje raia?

Binafsi naona sio sawa jamani au kwa vile ni nafasi za kuteuliwa? Najiuliza wale wa kwenye sector zisizo za kuteuliwa i.e watumishi wengine mfano walimu n.k wakiomba ruhusa nao wataachishwa kazi badala ya kupewa ruhusa. It means ukishindwa imekula kwako.

Hii ndo Tanzania ya Magufuli.
Acha wafu wazikane
 
Ilikuwaje Magufuli alipoenda Biharamulo akashindwa kura za maoni then akarudi kushika chalc ?What about Dr Mwele mwaka 2015 aliomba ruhusa kwenda kugombea Urais aliposhindwa akarudi kwenye ukurugenzi wake?
Jiwe anamuogopa na kumchukia SANA mpaka leo pamoja kuwa alikuwa keshamtumbua
 
Back
Top Bottom