Inasikitisha na kustua sana. Marehemu Kambayao wa TRA alikuwa pia Mwanachuo CBE Dodoma

Inasikitisha na kustua sana. Marehemu Kambayao wa TRA alikuwa pia Mwanachuo CBE Dodoma

Watu wakionewa kiuonevu machozi yao pia hayataisha bure wa kulaumiiwa ni serikali ya ccm na wabunge (bunge) walioruhusu raia kutekwa kishamba bila kuchukua hatua au bunge kuihoji serikali matokeo yake raia wameamua kujilinda wenyewe dhidi ya wasiojulikana.kwani katika nyakati hizi za kutekana nani angejua hao wanyatiaji wa usiku ni TRA na sio watu wasiojulikana?
Au nao wana namba feki, kama za hiyo BMW au za wale wa Tarimo
 
Kabla ya kusikitika jiulize,TRA kwenye lile tukio alikua kama dereva wa gari ya serikali,gari ya serikali huendeshwa na dereva muajiriwa na ambae hupaswa kua kazini muda wote na kuitunza gari,sasa aliwezaje kua mwanafunzi wa CBE -Dodoma akiwa anasomea degree ya mahesabu na kodi kama permanent student?!!

Tukio limetokea siku ya kazi,na kipindi ambacho vyuo vimefunguliwa,imekuaje hayupo chuo akawa yupo Dar na ilihali pia sio muda wa Field?!!

Gari walilokua wanataka kumteka(maana ule utekaji usiku kwenye foleni) namba DHZ ni usajili wa zaidi ya miaka minne nyuma,kwa nini hawajawahi kumuita mmiliki na kumkamata ilihali taarifa zake za mmiliki wa gari huwa zipopaka namba za simu?!!
Million dollar questions
 
TRA wanasema ni permanent employee wao nawe unadai yuko field, mtaendelea kujichanganya mpaka mrukwe na akili. Habari ya kwanza immediately baada ya raia wema kufanikiwa kuzuia utekaji alihusishwa na SUA, vipi hilo likayeyuka ikaja ya TRA na then ikaja ya CBE Idodomya yaani drama juu ya drama.
Mpaka mtanena kwa lugha this time around.
Nje ya mada: Huo muandiko wa darasa la pili ndiyo maana mnatumika kirahisi, so sad.
Kisomo cha wazee wa Tanga kinaleta majibu haraka sana
 
ART wameamua kutumika kufunika kombe lkn za ndani kutoka kwenye kiini ni kuwa kipepeo mweupe alikuwa katika majukumu yake ya nyuma ya pazia na siku ikawa mbaya kazini. Ndosababu unaona viranja kama wamechanganyikiwa vile, kila kiranja anatoa tamko.
 
Ni mtumishi wa TRA as a driver, na CBE ni mwanafunzi, so kila ofisi ime response kwa namna wanavyorelate naye.
Akiwa TRA ni mtumishi dereva while akiwa CBE ni mwanafunzi
Na madereva wengi wakishapata kazi ndio huanza kupambana kupata hizi degree baadae wanakuwa ma officer kabisa, bahati mbaya tu imemkuta
 
Umeambiwa ni TRA officer, soma vizuri na uelewe.
Hujaelewa
Unapokuwa field ,,, unaonekana kama ni mtumishi wa sehemu husika

Mfano

Ukienda feild bank ya N.M.B utaoneka mfanyakazi wa N.M.B

Ukienda field shuleni utaonekana mwalimu wa shule husika


Kijana alikuwa field T.R.A hivyo alikuwa T.R.A Officer..

Kwa hiyo wapo sahihi kusema ni mfanyakazi wa T.R.A wapo sahihi maana hawajataka kulezea kwa mapana zaidi kama alikuwa mfanyakazi wa vitendo au wa mkataba lakin kama alikuwa ni wa vitendo (field)

Mbona muda wa vitendo (filed ) umeisha ?? Ina maana yeye aliendela na field japokuwa muda umeisha ?? Kama ndiyo je alifanya hivyo kwa sheria zipi na taratubu zipi za T.R.A ??
 
Ni jambo la ajabu sana kuona kwamba TRA waenda mitaani kufuatilia gari ambalo wanahisi halijalipiwa kodi.

Zipo njia nyingi za kuhakikisha gari hilo halitembei pale linapogundulika halijalipiwa kodi.
Obviously lengo mama la usakaji huo, sio kukusanya mapato ya serikali kizalendo, bali ni kutumia nafasi hiyo kudai rushwa. Na hawahitaji kuongozana na polisi kwa sababu mgao wa hiyo rushwa utakuwa kidogo watakapoamua kugawana..
 
Kwamba hakuna maderva competent hapo wizarani hadi wamtumie dereva mwanafunzi?
Yule marehemu kwa umri wake inaonekana alikuwa ameanza kuajiriwa kisha akaenda kujiendeleza elimu huku akiwa kazini.
Pengine hakuchukua likizo ya masomo alikuwa on duty siku ile.
Kumbuka Kuna executive classes ambazo zina accommodate waajiriwa.
 
Back
Top Bottom