Hapa tunaweza kusema kwamba si kwamba una/mnabaguliwa ila nyinyi waislamu mnalazimisha udini sehemu zisizohitaji udini.
Nakupa mfano kupitia mifano uliyotoa;
Jamaa kaenda posta kwenye ofisi kuomba kazi,dress code ni suruali ya kitambaa na shati na chini kiatu cheusi. Kinyume chake yeye kaenda na kanzu na kiremba kichwani akakosa kazi. Huyu jamaa kakaja na malalamiko kabaguliwa kisa muislamu . Lakini asichojua Ni kwamba ubaguzi ni zaidi ya vile alivyotafsiri,maana kwa kitendo Cha kuvaa tofauti na wengine na kujihesabia wewe ni wa dini fulani,tayari huo ni udini maana amewabagua wasio waislamu.
Kuna ishu ya waislamu kule ujerumani kulazimisha kuvaa ijab kwenye nchi isiyo na misingi ya kiislamu,Hadi wakaleta vurugu na kuandamana kwamba wanabaguliwa. Lakini ukilitazama hili swala kwa undani unagundua kwamba wao ndiyo wabaguzi maana katka nchi ambayo wameweka misingi yao,wewe wa kuja ukaja na msingi wako ili ujitofautishe na wenyeji huo ni ubaguzi tayari.
Mkuu
adriz ubaguzi ni zaidi ya tunavyoutafsiri. Na asilimia kubwa ya waislamu wanaolalamika kubaguliwa,ukweli Ni kwamba wao ndiyo wabaguzi maana wakifika sehemu wanalazimisha kuibadili misingi ya Hilo eneo na kuleta itikadi zao ambazo Ni tofauti na wenyeji,wakikemewa wanaolalamika kubaguliwa. Ubaguzi unaanzia ndani ya mtu kwa kuanza kujitenga na wengine.
Focus.