Bishweko
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 3,406
- 2,521
Nimemsikiliza Rais Mama Samia tokea achukue hatamu za uongozi na leo spika wa Bunge kuhusu Bandari ya Bagamoyo ninashawishika kuamini kuwa Kakoko wa TPA alisimamishwa haraka na mama kwa lengo la kufungulia mradi wa Bagamoyo.
Kakoko alikuwa kikwazo cha ulaji au uwekezaji huu.
Nawakumbusha viongozi kuwa Magufuli alikuwa na ana watu wengi sana Watanzania wanaomwamini kuwa ndie alikuwa mtetezi wa kweli wa rasilimali na Watanzania. Hivyo waende taratibu maana akitokea kichaa akahoji kuhusu kifo na kushawishi vinginevyo kwa matendo yao nchi itayumba.
Nyerere alisema huwezi kumgusa Rais nchi isitikisike. Kifo kimemgusa Rais twendeni taratibu tusitake kuwachafua waliokuwa watumishi waaminifu wa marehemu maana wakijitetea watawashinda mbele ya Umma
Hivi unajua ata shetani anao watu wengi wanaofuata sheria na matendo yake?
Sasa ilo alifanyi kua shetani na wafuasi wake wapo sawa.