Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Shida hapo ni namba 2 kuwa mwanamke. Yaani waliwaza sana itakuwaje mwanamke kuwa Rais; na hata jinsi ya kumtaarifu iliwawia vigumu. Na sidhani kama hawakujua Katiba inasemaje, na pengine walitaka kuvunja Katiba kama walivyozoea kwa mambo mengine! Hongera kwa CDF msataafu.
 
CDF ameeleza vizuri tu kuwa alikuwepo hospital muda wote siku ya kifo na aliitwa baada ya mgonjwa kuzidiwa

By the way unawajua vizuri wanawake walivyo wanapopata taarifa ya msiba!!

Hii kauki ni vety sexist. Imewafanya wanawake wote watu nyoronyoro wasioweza kuhimili habari za msiba.

Samia hakutakiwa kuambiwa habari kwa sababu ni mwanamke.

Samia alitakiwa kuambiwa habari kwa sababu alikuwa Makamu wa Rais.

Na kama mliona wanawake hawaezi kuhimili taarifa za misiba kwa nini mmeruhusu kikatiba mwanamke awe Makamu wa Rais anayeweza kuja kuwa Rais kwa msiba?

Si mngesema kwenye katiba Makamubwa Rais hatakiwi kuwa mwanamke, kwa sababu wanawake hawawezi kuhimili habati za msiba.
 
Wale waliotaka kupindisha katiba wakati wa kifo cha JPM wana uwezo kweli kulingana na nafasi zao? Walishindwa kuelewa katiba inasemaje? Tena imeandikwa kwa kiswahili.
Walielewa katiba. Hawakutaka kuifuata.

Ni kama vile watu wanajiita Wakristo au Waislamu lakini wanavyoishi matendo yao hayafuati misahafu ya dini zao inavyosema. Sio kwamba hawajui misahafu inasema nini, hawataki tu kuifuata.
 
Mkuu tatizo kubwa katika utawala wa JPM ilikuwa ni kukosekana mifumo imara ya kitaasisi, ukiwemo wa urais, na huku nchi ikiendeshwa kwa "one man show". Inaonyesha JPM hakumuamini makamu wake, kitu ambacho hata wasaidizi wake wa karibu wakajikuta nao wakiwa wameingia katika mkumbo huo.

Ukichunguza utaona kuwa suala la ugonjwa wake, na hata pia taarifa zake zilighubikwa na usiri mkubwa sana, kiasi kwamba hata makamu wake hakuwa ana fahamu kwa undani kuhusu hatua mbalimbali alizopitia za kimatibabu hadi mauti ilipimfikia.
 
- Sioni sababu kwako kutomtaja Mabeyo ikiwa yeye ndie mhusika mkuu kwenye hii habari.

- Mabeyo amesema kuna watu walitaka kupindisha utaratibu, hajasema utaratibu kwenye jambo gani...

Kama ni hili suala la kutoa taarifa kwa VP, nani kati yenu anayejua kama kweli VP alinyimwa taarifa zinazomhusu Hayati Magufuli? au ndio unaegemea hiyo kauli ya Makamba walikuwa hawapewi salamu?!

Kwani wao kutopewa salamu ndio lazima VP asipewe updates kuhusu afya ya Hayati Magufuli? Kwangu thatz not enough. Mhusika mkuu Samia ndie athibitishe hili.

Sioni maana ya kuegemea maneno ya Makamba kwenye jambo linalomhusu Samia ikiwa nae yupo, na wala huo sio ubishi kama unavyoita, ni kutaka uthibitisho usioacha shaka.
 
Mie ningekua Mobeyo, ningekaa kimya tu. Cheap minds ndo zinamsifia ila hana tofauti sana na wale wengine, hata na yy alikua ameinhiwa na kishawishi cha kupindisha mambo ila akakishinda, na najua anajilaumu
 
Kifo cha Magufuli na jinsi Samia alivyokuja kuwa rais, na hizi figisu, na mpaka upinzani dhidi ya Samia kwa sababu ni mwanamke vinatuonesha jambo moja.

Watanzania wengi hawako serious kwenye uongozi, wanakwenda kwa mazoea.

Yani, walimkubali Samia awe Makamu wa Rais wakijua huyu atakuwa Makamu wa Rais pambo tu, mambo yote atafanya Rais Magufuli.

Hawakujua kwamba Makamu wa Rais yupo "one heart beat away" from becoming president.

Yani hata kwa rais ambaye alikuwa ana matatizo ya moyo yaliyojulikana miaka mingi sana kama Magufuli, watu hawakufikiria kwamba Magufuli anaweza kufia madarakani hakafu Samia akawa Rais kwa mujibu wa katiba.

Watanzania wengi waliona Rais wa Tanzania hawezi kufia madarakani, it is against the laws of physics.

Ndiyo maana wengine mpaka leo wanamuona Samia kama si Rais kamili. Wengine wanadiriki hata kusema si Rais halali, kwa sababu hajawa Rais kwa uchaguzi.

Wengi hawaelewi concept ya "running mate" kuwa katika ticket moja na presidential candidate maana yake ni kuwa, unapopiga kura, unaipigia kura ticket nzima, si mtu mmoja, hivyo mandate ya kuongoza Magufuli ina extend mpaka kwa Samia, wale wawili walikuwa ni "a packaged deal".

Ndiyo maana inasikitisha sana kusikia kuna watu wanamnyanyapaa Samiankwa sababu mwanamke.

Kama wanawake hawafai uongozi Tanzania, mlikubalije Samia awe running mate wa Magufuli na hivyo kuwa na potential ya kuwa Rais siku yoyote Magufuli akifia madarakani?
 
Wewe hujui hata kufuatilia habari kimantiki na hivyo siwezi kujibizana nawe kimantiki.

Kichwa chako kina logic iliyopinda kwa hiyo nikikupa logic sahihi ndogo tu wewe utaona imepinda, na wewe ukinipa logic unayoona sahihi mimi naona imepinda.

Awali kabisa, tunakwenda na habari za Mabeyo hapa.

Kuna sehemu Mabeyo kasema Makamu wa Rais alipewa habari za mgonjwa kabla hajafa?

Kama Makamu wa Rais ndiye mrithi halali wa Rais kikatiba, kwa nini habari za hali mbaya ya afya ya rais apewe Waziri Mkuu na si Makamu wa Rais?
 
Ndugu, hili unaliona leo? Nchi hii tunaowaita viongozi, hawaijui Katiba ya nchi japo huapa kuilinda na kuitetea, bali si kuitii na kufuata maagizo yaliyomo ndani yake! Wanafuata maneno yatokayo mdomoni mwa aliye kiongozi wao hasa wa ccm.
 
Aisee, umeiweka vizuri sana hii. Na kimsingi huwezi kutenganisha kura za Mgombea na Mgombea mwenza; hawa wote wanabebana!
 
Mabeyo amefanya kitu kimoja nikaitwa KOSA LA KIUFUNDI....

Mbele ya utaratibu wa Kijeshi sidhani kama alipaswa kureveal hayo kwa sababu hii taharuki inayoanza kuenea inaibua maswali ya kimantiki na wakosoaji wanapata nafasi kujua udhaifu wa Sponsor na Amiri Mkuu.

Pia inamuanika hadharani Waziri Mkuu ambaye kumbe alikuwa anafuatilia kila kitu kuhusu afya ya Rais huku akisimama majukwaani kuongea uongo.
 
Aisee, umeiweka vizuri sana hii. Na kimsingi huwezi kutenganisha kura za Mgombea na Mgombea mwenza; hawa wote wanabebana!
Naam,

Kimsingi, watu wamepigia kura ticket ya CCM iliyowakilishwa na John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan.

Hawakumpigia kura mtu.

Ndiyo maana kuna kipindi Mkapa alifoka akasema msiseme serikali ya Magufuli, semeni serikali ya CCM. Magufuli angepata urais bila kupewa uanachama, ubunge, uwaziri na nomination ya urais ya CCM?

Sasa hapo utatenganisha vipi wangapi wamepiga kwa sababu ya nani?

Maana yake kura ni zao wote.

Na tulifanya hivi makusudi kumpa huyu Makamu wa Rais political legitimacy ya kuja kuwa rais ikiwa rais atafariki.

Yani, zaidi ya ike legal legitimacy, kwamba kikatiba anamrithi Rais, lakini pia kuwepo na political legitimacy kwamba na yeye alichagukiwa na watu pamoja na rais.

Sasa, inashangaza sana kusikia kuna wakuu wa nchi walikuwa wanajadili kama Samia awe Rais au asiwe, wakati jambo lipo wazo kabisa kikatiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…