Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Hao viongozi si kwamba hawajui katiba, huwa wana makandokando yao ya figisu za kutaka kutofuata katiba.

Ukimsikiliza January Makamba alivyoongea hivi karibuni alikuwa anasema watu waliokuwa wanafanya kazi Ofisi ya Makamu ya Rais walitengwa, hata salamu walikuwa hawapewi.

Kwa hiyo haya mambo ya kumshirikisha Waziri Mkuu bila kumshirikisha Makamu wa Rais hayakutokea jwa bahati mbaya au kwa kukosa kujua katiba.

Huo ulikuwa ni mpango makusudi wa kumuondoa Makamu wa Rais katika succession plan.

Ukimsikiliza Mabeyo kuna sehemu kasema mambo kwa summary sana, kafupisha sana, hajatoa story kamili. Hii jistoria inahitaji kitabu kizima kuiandika.

Na kuhusu Magufuli alikuwa na haki ya kufia nyumbani kwake, everyone has a right to die with dignity, na moja kati ya haki hizo ni pale mtu anapogundua kuwa haponi, basi apewe nafasi ya kufa nyumbani akizungukwa na wapendwa wake.
Rais afie chato??
 
Rais afie chato??
Mkuu,

Chato si kwao, tatizo liko wapi?

Unataka wewe umpangie mtu pa kufia wakati yeye mwenyewe kashasema anataka kufia kwao?

Unamnyima tamanio lake la mwisho la kufa akiwa kazungukwa na ndugu zake kwao?

Kwa watu fulani, ni muhimu sana kufia kwao, na kama hilo ndiyo takwa lao la mwisho, wewe ni nani uwakatalie?
 
Mkuu,

Chato si kwao, tatizo liko wapi?

Unataka wewe umpangie mtu pa kufia wakati yeye mwenyewe kashasema anataka kufia kwao?

Unamnyima tamanio lake la mwisho la kufa akiwa kazungukwa na ndugu zake kwao?
Usifananishe rais na takataka zingine,we hata ukitaka kufia porini sawa tu sio rahisi,uhai wake unapiganiwa kwa gharama zote na kuna watu wanakuwa responsible ikitokea uzembe wowote ule,rais hupangiwa mambo mengi maana ni taasisi
 
ujuaji wa kipumbavu tunao watanzania

aliye kuwa na mgonjwa ni mabeyo

makamu yuko tanga

waziri yuko dodoma, ko ulitaka aliye na mgonjwa (aliye eneo la tukio ) asifahamu hali ya mgonjwa afahamu aliye tanga na dodoma

acheni ujuaji wa kipumbavu
 
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.

Ndio maana wabongo tunafeli Sana exams because ni wavivu kusoma na kuelewa

CDF alikuwepo wakati Magu anafariki because alipigiwa simu na madoctor kuwa Hali ya Mzee imebadilika so CDF alienda pale JPM akiwa mzima na kafa mbele yao

Sasa ww unaongea mambo tofauti
 
Mkuu,

Here are facts.

1.Hakuna popote nilipomtaja CDF Mabeyo.

2.CDF Mabeyo mwenyewe kasema kuna watu walitaka kupindisha utaratibu.

3. Kwa mujibu wa CDF Mabeyo Makamu wa Rais alirukwa kabisa kwenye updates za kutoka hospitalini, habari alikuwa anapewa Waziri Mkuu Majaliwa. Licha ya kwamba Makamu wa Rais ndiye mrithi wa Rais, ikiwa Rais atafariki, kikatiba.

4. Habari hii ya CDF ina corroborate habari ya Makamba kwamba Ofisi ya Makamu wa Rais ilitengwa.

Sasa unataka kukataa maneno ya CDF kwamba kuna watu walitakankupindisha katiba Makamu wa Rais asiwe Rais?

Unataka kusema January Makamba kasema uongo mbele ya Rais Samia, Makamu wa Rais na watu wa Ofisi yaje hawakutengwa? Mbona haya mambo tuliyasikia tangu Magufuli yupo hai?

Unachobisha ni kipi hasa?

Kaka hiyo namba 3 unachanganya mambo hebu sikiliza tena vizuri
 
Ndio maana wabongo tunafeli Sana exams because ni wavivu kusoma na kuelewa

CDF alikuwepo wakati Magu anafariki because alipigiwa simu na madoctor kuwa Hali ya Mzee imebadilika so CDF alienda pale JPM akiwa mzima na kafa mbele yao

Sasa ww unaongea mambo tofauti
ujuaji wa kipumbavu mkuu
yaan mtu aliye na mgonjwa asifahamu hali ya mgonjwa afahamu aliyeko tanga
 
Wewe hujui hata kufuatilia habari kimantiki na hivyo siwezi kujibizana nawe kimantiki.

Kichwa chako kina logic iliyopinda kwa hiyo nikikupa logic sahihi ndogo tu wewe utaona imepinda, na wewe ukinipa logic unayoona sahihi mimi naona imepinda.

Awali kabisa, tunakwenda na habari za Mabeyo hapa.

Kuna sehemu Mabeyo kasema Makamu wa Rais alipewa habari za mgonjwa kabla hajafa?

Kama Makamu wa Rais ndiye mrithi halali wa Rais kikatiba, kwa nini habari za hali mbaya ya afya ya rais apewe Waziri Mkuu na si Makamu wa Rais?
Unadai siwezi kufuatilia habari kimantiki wakati wewe unatumia mfano wa Makamba kudai kunyimwa salamu, kama justification yako kwa Samia kutopewa taarifa za hali ya kiafya ya Hayati Magufuli.!!

Samia yupo kwanini asiulizwe hili ili aje na majibu yake badala ya kutumia majibu ya wengine kama Makamba ambayo hata hayaendani na uhalisia wa kile kilichozungumzwa na Mabeyo? Hii kwako ndio mantiki?

Anyway, good night..
 
Sin
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
Sina uelewa mpana sana kuhusu haya masuala lkn ninahisi yafuatayo yalilengwa.

1; Kufariki kwa Rais wa Nchi tena akiwa madaraka huenda kukatumiwa na wasiositahili kukwapua madaraka hivyo ni lazima mkuu wa vyombo vya ulinzi wa Nchi husika apate taarifa ili apange vikosi vyake kuwa tayari kwa lolote.

2; Ukubali wa mkuu wa Majeshi ya ulinzi kumpa ushirikiano wa dhati mrithi wa nafasi ya Rais licha ya kiapo chake kumtaka afanye hivyo ila kwakuwa sisi ni watoto wa binadamu tumeumbiwa kukengeuka.

Ninahisi hivyo wakuu.
 
Usifananishe rais na takataka zingine,we hata ukitaka kufia porini sawa tu sio rahisi,uhai wake unapiganiwa kwa gharama zote na kuna watu wanakuwa responsible ikitokea uzembe wowote ule,rais hupangiwa mambo mengi maana ni taasisi
Sasa mbona mmeshindwa kumpangia asife?

Watanzania wengi kama wewe hawaelewi uhuru ni nini.

Hivyo hawaelewi uhuru wa mtu binafsi ni nini.

Hawaelewi kuwa hata Rais, licha ya itifaki zote, bado pia ana uhuru wa mtu binafsi.

Yani mtu mshajua anakufa tu huyu. Yeye anataka afie kwao kazungukwa na ndugu zake.

Mnavyomkataza asipate hilo takwa lake la mwisho itasaidia nini? Ndiyo itazuia asife?
 
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
Ila we jamaa duuuh
 
Unadai siwezi kufuatilia habari kimantiki wakati wewe unatumia mfano wa Makamba kudai kunyimwa salamu, kama justification yako kwa Samia kutopewa taarifa za hali ya kiafya ya Hayati Magufuli.!!

Samia yupo kwanini asiulizwe hili ili aje na majibu yake badala ya kutumia majibu ya wengine kama Makamba ambayo hata hayaendani na uhalisia wa kile kilichozungumzwa na Mabeyo? Hii kwako ndio mantiki?

Anyway, good night..

Unazidi kuthibitisha huwezi kufuatilia mambo kimantiki.

Sijatumia mfano wa January kama justification ya Samia kutopewa taarifa.

Kitu kilichotokea baadaye hakiwezi kuwa justification ya kitu kikichotokea awali.

Justification inafanyika hivi.

Jambo 1 linatokea awali, watu wanalitumia hili jambo 1 lililotokea awali ku justify jambo 2 linalofuatia.

Sasa hapa katika timeline, Makamu wa Rais kutengwa / kutopewa taarifa ni jambon 1, limetokea awali, Makamba kusema ofisi ya Makamu wa Rais ilitengwa ni jambo 2, limetokea baadaye, nitatumiaje jambo 2 kama justification ya jambo 1?

Pili, mimi napinga Makamu wa Rais kutengwa na kutopewa taarifa, nita justify vipi kitu ninachokipinga?

Unajua kusoma kwa ufahamu wewe kweli?

Sijui hata kama unaelewa justification ni nini na kwamba hiyo sentensi yako tukiichambua kimantiki tutaikuta haina maana, ni kama imeandikwa na mtu mwenye matatizo ya akili asiyeweza kupanga maneno yake vizuri.

Unaelewa "justification" maana yake ni ni kweli? Na unaona hilo neno umelitumia sahihi kabisa hapo?

Wewe unaona kisiasa Samia anavyojua Magufuli ana wafuasi wengi mpaka kesho itakuwa busara kwake kusema "Magufuli alinitenga sana"? Wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi wa 2025?

Unaona huyo Makamba mpaka kusema hivyo mbele ya Samia kajiropokea tu bila kupewa go ahead na Samia?

Samia anatafuta "plausible deniability". Anataka kusema alitengwa, lakini hataki kusema yeye mwenyewe, ndiyo maana kazi hiyo kaachiwa Makamba, mtu expendable, watu wakimbana Samia aweze kusema mimi sijawahi kusema hilo, hayo maneno ya Makamba, lakini, anataka ujumbe wake ufike.

Mabeyo kasema habari za maendeleo ya afya alikuwa anapewa Waziri Mkuu, hakupewa Makamu wa Rais ambaye ndiye mrithi wa rais. Wewe huoni hili linazidisha ushahidi kuwa Makamu wa Rais alitengwa? Kwa nini taarifa alipewa Waziri Mkuu na si Makamu wa Rais ambaye ndiye mrithi wa rais kikatiba?
 
Na nahisi mengi yanakuja kwakuwa kama CDF kaongea tumsubiri Na DG na yeye Ataongea tu siku moja au IGP pia Kiufupi hata wale viongozi wa siasa..
Ukweli huwa una tabia moja unatabia ya kukereketa na Unabeba Hatia..
Kwahyo mtu akiusema huona kashusha hatia..
Tusubiri
Kama Siri njema hufichuka haraka ile iliyo mbaya haifichiki kamwe
 
Back
Top Bottom