Kifo cha Magufuli na jinsi Samia alivyokuja kuwa rais, na hizi figisu, na mpaka upinzani dhidi ya Samia kwa sababu ni mwanamke vinatuonesha jambo moja.
Watanzania wengi hawako serious kwenye uongozi, wanakwenda kwa mazoea.
Yani, walimkubali Samia awe Makamu wa Rais wakijua huyu atakuwa Makamu wa Rais pambo tu, mambo yote atafanya Rais Magufuli.
Hawakujua kwamba Makamu wa Rais yupo "one heart beat away" from becoming president.
Yani hata kwa rais ambaye alikuwa ana matatizo ya moyo yaliyojulikana miaka mingi sana kama Magufuli, watu hawakufikiria kwamba Magufuli anaweza kufia madarakani hakafu Samia akawa Rais kwa mujibu wa katiba.
Watanzania wengi waliona Rais wa Tanzania hawezi kufia madarakani, it is against the laws of physics.
Ndiyo maana wengine mpaka leo wanamuona Samia kama si Rais kamili. Wengine wanadiriki hata kusema si Rais halali, kwa sababu hajawa Rais kwa uchaguzi.
Wengi hawaelewi concept ya "running mate" kuwa katika ticket moja na presidential candidate maana yake ni kuwa, unapopiga kura, unaipigia kura ticket nzima, si mtu mmoja, hivyo mandate ya kuongoza Magufuli ina extend mpaka kwa Samia, wale wawili walikuwa ni "a packaged deal".
Ndiyo maana inasikitisha sana kusikia kuna watu wanamnyanyapaa Samiankwa sababu mwanamke.
Kama wanawake hawafai uongozi Tanzania, mlikubalije Samia awe running mate wa Magufuli na hivyo kuwa na potential ya kuwa Rais siku yoyote Magufuli akifia madarakani?