Na yeye mwenyewe aliona ni sahihi kuondoka na kumwacha mgonjwa yu mahututi?
Mkuu,
Ungefuatilia mantiki ya mazungumzo haya, ungeona hapa kuwa swali lako limejengwa katika misingi iliyo misinformed na ni swali la "blaming the victim".
Kitu kikubwa kinachoonekana katika sakata la kifo cha Magufuli, na hata kabla ya kifo , kwenye ugonjwa, na hata kabla ya ugonjwa, kwenye serikali, ni kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Ofisi nzima ya Makamu wa Rais walitengwa kwenye mambo mengi sana.
January Makamba kwenye hotuba yake ya kumkaribisha Samia ughaibuni, nafikiri Italy, hivi majuzi amekuja kuthibitisha hizi habari kutoka kuwa tetesi na kuwa habari rasmi.
Na ukimsikiliza Mabeyo, jinsi taarifa zikivyokuwa zinatolewa, taarifa alikuwa anaopea Waziri Mkuu Majaliwa, si Makamu wa Rais Samia.
Na zaidi, Mabeyo anasema kulikuwa na mpango wa kupindisha katiba ili Samia asiwe Rais kama katiba inavyotaka. Kwa bahati waliweza kusimamia katiba Samia akaapishwa kuwa Rais.
Maana yake kulikuwa na mpango wa watu wakubwa sana serikalini (Mkuu wa Usalama ametajwa) na wa makusudi kabisa, kutaka kumuweka rais mtu kinyume na katiba, Samia arukwe.
Sasa, hapo utaona kuwa Samia alitengwa, hata habari za ugonjwa hakupewa, kapewa habari baadaye baada ya Magufuli kufariki.
Mtu kama huyo unamlaumu vipi kwamba kamuacha mgonjwa wakati pengine na yeye alikuwa anaambiwa rais yuko Ikulu anachapa kazi tu, hakujua mgonjwa? Pengine hata hiyo safari ya Tanga kapangiwa ili watu wakitaka kupindua katiba iwe rahisi.
Wewe unafikiri Samia angejua Magufuli anaumwa mahututi, na yeye Samia ndiye mrithi wa Magufuli, na kuna uwezekano wa mchezo mchafu kuchezwa kupindua katiba, angekubali kwenda Tanga na kuacha kuwa karibu na rais kujua hali inaendaje?
Samia kama hakujua Rais Magufuli anaumwa, ana hali mbaya, angemuacha vipi mgonjwa kama hakujua Magufuli ni mgonjwa hivyo?
Huoni kuwa kumlaumu mtu aliyenyimwa habari kwamba kuna mgonjwa kwa kosa la kumuacha mgonjwa ni kumuonea mtu ambaye na yeye ni muhanga tu wa power politics?