Hapana..!!
Bila shaka, wewe ndiye hujui lakini hujui kuwa hujui!
Kikatiba, wakati wowote Rais anapokuwa hayupo au anaumwa au amekufa au kwa sababu zinazotajwa na katiba, basi Vice President automatic ndiye huchukua nafasi ya Rais. Na kwa hiyo anabeba nguvu na mamlaka (power & authority) ya position ya Rais...
CDF, IGP na DGIS ni washauri wa Rais ktk mambo ya ulinzi na usalama wa ndani ya nchi na mipaka yake. Hapo walikusanyana watatu wote kumshauri mgonjwa mahututi na baadaye maiti, au?
Je, hawakupaswa kutenda wajibu wao huo kwa VP ambaye ndiye anayetambuliwa na katiba kwa kuwa Rais alikuwa mahututi na baadaye kuwa amefariki dunia?
Ndiyo maana kwa sababu ya kifo, katiba inataka haraka sana VP apishwe na kuwa Rais ili kuvaa mamlaka ya u - Rais kwa ukamilifu wake..
Na kingine unachopaswa kukumbuka ni kuwa, nchi hii tangu mwaka 1961 imekuwa chini ya uongozi wa kiraia kwa mujibu wa katiba.
Hakuna mahali popote ndani ya katiba Jeshi limepewa mandate ya kuingilia na kuchukua mamlaka halali ya uongozi wa kiraia wa nchi uliowekwa kihalali kwa mujibu wa katiba.
In very rare cases mapinduzi ya kijeshi (Jeshi kupindua uongozi wa kiraia) ktk nchi yanaweza kutokea. Lakini , by then there was no thing like that..
Majukumu na mamlaka ya CDF yako very clearly stated kikatiba.
Lord denning yuko sahihi. Kuna kitu kinafichwa hapa. Kwanini VP alitolewa kwenye chain of command ya mamlaka ya uongozi wa kiraia wa nchi?
Kwanini CDF, IGP na DGIS ndiyo walikuwa wamemzunguka Rais tangu kuumwa hadi kufa kwake huku wakitambua kuwa nchi hii iko chini ya mfumo na utaratibu wa uongozi wa kiraia na sio wa kijeshi?
Walikuwa wanapanga nini? Kwanini finally, dakika za mwisho ndo wanaona ingalau tuwashirikishe Karibu Mkuu kiongozi na Waziri Mkuu huku wakimwacha VP ambaye kikatiba ndiye aliyepaswa kujua jambo hili kila hatua?
Mimi naweza kusema, kwamba, kwa jambo hili, obviously kuna possibilities tatu;
Aidha
1. CDF alikuwa na maelekezo maalumu toka kwa hayati Rais Magufuli mwenyewe kuwa alipoona kuwa uwezekano wa kupona haupo. Ni wazi kuwa CDF aliambiwa maneno haya "....
hawa watu wameshaniua. Sitapona. Tafadhali, bwana CDF nikifa hii nchi jeshi ndilo liongoze.."
Au;
2. CDF, IGP na DGIS wao wenyewe kwa mapatano wali - conspire kutaka kupindua uongozi wa kiraia wa nchi hii na kutumia kifo cha Rais Magufuli kusimika uongozi wa kijeshi na wao wenyewe walikuwa pale wakipanga nani atakuwa nani..
Na au;
3. Kulikuwa na kundi la viongozi wengine wa kiraia kwa kulishawishi Jeshi, walitaka kuleta mapinduzi kuzuia taratibu zilizowekwa na katiba kufuatwa ikiwemo VP kuapishwa na kuwa Rais..