Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hao viongozi si kwamba hawajui katiba, huwa wana makandokando yao ya figisu za kutaka kutofuata katiba.
Ukimsikiliza January Makamba alivyoongea hivi karibuni alikuwa anasema watu waliokuwa wanafanya kazi Ofisi ya Makamu ya Rais walitengwa, hata salamu walikuwa hawapewi.
Kwa hiyo haya mambo ya kumshirikisha Waziri Mkuu bila kumshirikisha Makamu wa Rais hayakutokea jwa bahati mbaya au kwa kukosa kujua katiba.
Huo ulikuwa ni mpango makusudi wa kumuondoa Makamu wa Rais katika succession plan.
Ukimsikiliza Mabeyo kuna sehemu kasema mambo kwa summary sana, kafupisha sana, hajatoa story kamili. Hii jistoria inahitaji kitabu kizima kuiandika.
Na kuhusu Magufuli alikuwa na haki ya kufia nyumbani kwake, everyone has a right to die with dignity, na moja kati ya haki hizo ni pale mtu anapogundua kuwa haponi, basi apewe nafasi ya kufa nyumbani akizungukwa na wapendwa wake.
Kwanza marehemu hawezi kulaumiwa kwa kutaka kupelekwa kwao au hata angetamka chochote muda huo.
Katika hali kama hiyo ya kukielekea kifo, mgonjwa anasemehewa kwa chochote anachoweza kusema.