Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Watu wenyewe si ndio nyie wabishi na wajuaji,mmekumbatia vya mzungu na kuviona Bora na kuvidharau vyenu, endeleeni kunywa mseto,waacheni wanaoupenda Uafrica wafiche roho zao kwenye miti
Halafu hii idea nzuri sana ,kwanza unaweza anzisha NGO kabisa na ukapata fedha za mzungu mpaka uzikimbie ,
Maana kwanza unaokoa maisha halafu unatunza mazingira , kwa kuhifadhi roho za watu kwenye mimea (miti)
Bonge moja la idea ,
Ngoja nilifanyie kazi ,lazima niwe bilionea kabisa [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Madame B habar za masiku,sorry out of jokes 😂,hivi kwenye ile michezo yetu haina madhara kwenye mitambiko 😂,najua umeelewa ninachokisemea
 
Upo sawa.
Juzi tumeona wizara ilianzisha tahasusi za dini mbili. A level
Je kati ya hizo umeona hata moja inayohusu hao wazee wa mila?
Km sivyo ni kwanini haipo?
Yote ya mila za kiafrika ni mabaya?
Nafkiri hii inajulikana kama ipo lkn ndio hivyo mara nyingi wahusika wanaitumia kwa namna mbaya km kuangamiza n k. Ndio maana inafanyika kisirisiri. Ni km vile ipo forbidden mama inajulikana ikiachiwa ikatumika dhahir watu wengi wataumia.
Ni mawazo yangu tu
 
Hizi hoja zako zimekaa kama unasuta. Embu tuliza ubongo twende taratibu. Jibu swali kwanini hiyo elimu ni siri. Jibu kwa ufupi tu bila mbwembwe zisizo na ulazima.
Sorry,una umri gan kwanza mkuu,?,cha kukushauri endelea kukua haya mambo utayakuta mbelen sasa hivi endelea kukaza fuvu
 
OK, Achana na porojo na imoji imoji nenda kwenye jibu. Sababu za msingi za elimu ya kuweka roho kwenye miti kutokuwa wazi ni zipi?
Una maana gani haziko wazi?

Kwamba kulitakiwa kuwe na shule kama Jangwani secondary school? Kwamba kuwe na kipindi shuleni na mwalimu anaefundisha “jinsi ya kuweka roho kwenye mti? Una maana hii?

Nimekuuliza kabla, unaelewa nini ukisikia neno Mila? Desturi? Tamaduni?

Wewe kwenye family/ukoo wako hakuna Mila? Desturi? Tamaduni?

Unatambua kila elimu/utaalamu unapatikana kwa mujibu wa taratibu?

Sasa wewe umetafuta lini hiyo elimu ya kuweka roho kwenye mti ukaikosa? Ulifuata masharti na kutimiza vigezo?

Wewe hiyo elimu ya chekechea mpaka ulipoishia, ulikutana nayo barabarani ikakuvagaa ama ulifuatishwa/ulifuata utaratibu, masharti na ukatimiza vigezo ndio ukaipata?
 
Ndio sababu huwa inashauriwa miti mikubwa isikatwe ovyo
 
Wakati nasoma chuo kulikuwa na mkaka kwao sumbawanga aliwahi kunisimulia story inafanana na hii alisema huyo mtu had aliwaambia mwenyew wafukue mlangoni wakakuta nguozake zimezikwa walivozitoa ndio akafa
Uko sahihi Aaliyyah.
Kwetu kipindi cha mavuno, familia nyingi hukataza watoto/vijana wao kucheza nje jua linapoanza kuzama kwani msimu huu ndio watoto/vijana wengi hupelekwa mashambani kuvuna kimiujiza.
Na sio lazima wachukuliwa msukule, hapana ila kama anacheza au yuko na vijana wenzake mtashangaa mtoto wenu analala usingizi mzito na haamki mpaka amalize kazi ndio anashtuka.
Ila wazee wa kule hawana uchoyo kuwapa uchawi wajukuu....🤔

Wazee kushindana kufanya uchawi hadharani kweupe, kwetu ni jambo la kawaida sana.

Watoto kuua wazazi kwa amri ya mababu, ni jambo la kawaida sana kwetu.
Kuna kisa kimoja huwa kiliniacha hoi mpaka leo..
 
Hapo ndo shida
Wanaudharau na kuutukuza wa weupw
 
Kwenye sayansi ya kiafrika Yapo kweli mkuu.
Nimeyashuhudia. Ila huwa nashangaa kwanini wanatafuta njia ya kuwauwa?
Kwanini wasithubutu kuangalia mwisho wake?
Na Mimi ningependa nijue.

Pengine uwoga wa harufu mbaya na mtu alieoza kuongea?

Lakini vipi Kama ukipatikana ujasiri wa kusubiri mpaka mwisho kuona ni nini kitatokea?
Ataoza na kubaki sauti tu ama kitabadirika na kuwa kitu kingine?

Kweli hakuna uwezekano kuna watu wanajua tayari? Hao Jamaa wengine wanapenda sana “kujua kila kitu ni kweli hawajatafiti na kutumia majibu to their advantage?

Kwanini sisi (Africans)tunaogopa sana kifo? Wazee hawa wanajua Siri gani kuhusu hii Dunia mpaka wanaweza kuunga roho na miti?
 
Interested, mkuu tutaamini vipi hii taarifa, tupe source ya taarifa tujifunze
kuna jamaa angu mmoja alitoka kumzika babu yake vijiji vya mkoa wa mara huko. Aliniambia kitu kama hicho aisee.

Kwamba babu yao amekufa kifo cha mateso sana maana ilifikia hatua mwili unaoza lakini bado ni mzima sababu alijifunganisha roho yake na vitu gani gani sijui vya mila zao hadi walivyofanya hizo tamaduni kutimiza masharti ndipo alifariki. Japo nilimsikiliza tu bila kuamini wala kukataa lakini ndio hivyo ilitokea.
 
Mwanakondoo alishachinjwa pale Calvary na damu yake inatosha kufuta laana zote na mikosi yote inayowaandama, huhitaji tena kuchinja kondoo wengine.

Okoka Sasa na mpokee Kristo Ili uwe huru na laana za ki Ukoo.

Rabbon Yesu Anakuja
 
Sikatai uchawi upo ila kuna mambo mengine hata mtoto wa la kwanza tu anaona kwamba hapa tunapigwa
 
Una maana gani haziko wazi?
Kuwa wazi namaanisha zisiwe za hadithi hadithi, kwamba mtu kama anaihitaji hiyo elimu anaweza fika sehemu rasmi na akapewa maelekezo. Sehemu rasmi.
Kwamba kulitakiwa kuwe na shule kama Jangwani secondary school? Kwamba kuwe na kipindi shuleni na mwalimu anaefundisha “jinsi ya kuweka roho kwenye mti? Una maana hii?
Mfano ukihitaji kupata elimu ya kutibu malaria kwa njia ya asili unajua kabisa unaweza muona mzee fulani pale kariakoo. Ni rasmi
Wewe kwenye family/ukoo wako hakuna Mila? Desturi? Tamaduni?
MIla zetu zipo wazi. kwenye nchi yangu kuna kuna library kabisa ya asili na tamaduni zetu pale makumbusho. Litembelee.
Unatambua kila elimu/utaalamu unapatikana kwa mujibu wa taratibu?
Utaratibu upi wa kufuata ukihitaji kupata elimu ya kuhamisha roho kwenye miti?
Sasa wewe umetafuta lini hiyo elimu ya kuweka roho kwenye mti ukaikosa? Ulifuata masharti na kutimiza vigezo?
Vinapatikana wapi? Kwa nani? Kwa utaratibu upi?
Wewe hiyo elimu ya chekechea mpaka ulipoishia, ulikutana nayo barabarani ikakuvagaa ama ulifuatishwa/ulifuata utaratibu, masharti na ukatimiza vigezo ndio ukaipata?
Hizi ni porojo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…