Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao?

Mkuu
Haujamuelewa mtoa mada
Kwa ufupi hajamaanisha jinsi ulivyoelewa. Vise versa is also true.
 
Ndugu yangu Pasko, asante kwa maoni yako. Dah....!
Agreeing to disagree is the key word.
Reading between the lines, bandiko lako like 'twisted' na hii si bahati mbaya you being a veteran journalist.
 
Ndug paskali nimesikitishwa sana na hili bandiko lako hasa kutokana na unguli ugwiji na umwamba wako kwenye kujenga hoja nilikuwa nimekaa natamani hata ukanushe kuwa hili sio bandiko lako au kuna dogo kakuhulk.

Sivutiwi sana na siasa za kupigia promo jinsia ya mtu na hata kama huenda wamarekani wamemwacha Kamala kwa sababu hiyo tu basi litakuwa tatizo kubwa sana jambo ambalo sitaki kuamini hata kidogo.
Wachambuzi wengi wa ndani wa marekani kwenyewe wanaona kwamba kilichompaisha Trump ni sera zake za kufufua uchumi kwa kuyapunguzia kodi mataikoon, jambo litakalopunguza bei za bidhaa na kupunguza makali ya maisha kupunguza fedha inayotumika kufadhili vita hivyo kuhakikisha fedha ya marekani inanufaisha wamarekani kwanza.
Ndo maana haikushangaza mataifa mengi hasa ulaya walipigwa ganzi kwa muda kuona trump kashinda. Haikuwa kwa kuwa mwanaume bali kwa vile sera zake ni marekani na wamarekani kwanza.
 
inderect speech
 
Hii ndiyo Bongozozo anaita fujo isiyoumiza.
 
Wacha hiyo wewe! Huyu tumekuwa naye kwa bahati mbaya sana! Hebu aishie hapo alipofikia imetosha sasa! Kama Wamarekani wamemkataa mtu mwe ye IQ kubwa sisi ni nani hata tuendelee na zero?
Ndiyo maana Baltasar ameamua kufanya vile, ametuma ujumbe mkubwa sana wenye akili kubwa tu ndiyo watauelewa.
 
Wamarekani sio muungano wa Nchi 1 na kuna vichwa vina akili ya kuiongoza dunia na kusaidia dunia kwa kumchagua Mwanaume inadhihirisha wazi kua Wamarekani haitokuja itokee waongozwe na rais Mwanamke yaan Wanawake hii ndio ilikuwa karata yao ya Mwisho na sio Marekani tu, labda itokee Ndondokela Trump amchague Makamu Mwanamke kisha wamfyeke hapo ndio Mwanamke anaweza kuchukua Nchi kinyume na hapo wasahau na pia Trump sio fala kuchagua Makamu Mwanamke ili baadae akifa Nchi ichukuliwe na Mwanamke kamchagua Mwanaume awe Makamu wake
 
Pia walikuwa hawapigi kura kabisa
 
Mwanaume Mwanaume tu acha kupigapiga konakona nyingi saaaana ibaki kua hivyo everybody wants Trump in thaf state house hata Kamala Harris na watu wake nahisi watakua wamempigia kura Trump
 
Wamarekani wa huku Namanyele wameshamchagua Kamala Harris mpaka 2030 ni kuonyesha jinsi gani wana Akili sana kuzidi Wamarekani wa Washington DC
 
Shukrani mkuu. Hata mimi nakubaliana na wewe kwamba Wamarekani si wajinga, tumchague Ili tuwaonyeshe kuwa ni wajinga
Mmarekani wa Bariadi akichangia hoja kua yeye 2025 anaenda na Kamala Harris mpaka 2030 na Kamala akitaka kuongeza mpaka 2035 yupo tayari kumbakisha Ikulu kwa kumpigia kura, umeeleweka
 
Hili jukwaa kweli ni la Great Thinkers, naona wachangiaji wengi hawajaelewa. Umerusha jiwe gizani na kuingia kichwa kichwa inabidi uwe na mwanasheria wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…