Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Dini ni zao la nani?Binaadam kwa kutumia utashi tu angeandaa namna nyingine ya kujisimamia.
Unaona kuna hizi sheria zimesimama ili kutoa haki,ingawa sio 100% ni zao la binaadam.
Kwa maelezo hayo unamaanisha kwamba hakuna maisha pasipo na dini? Kama ni hivyo basi dini ni jambo muhimu sana kwa mwanadamu.Nani huyo alisahau kukwambia haiwezekani kabisa kutenganisha maisha ya mwanadamu na dini?
Mwanadamu kihulka ni mtu wa dini.
Labda kama hujui maana ya dini, hapo unaweza kueleweka.
Hakuna kipengele cha maisha ambapo dini inaweza kukwepeka.
Mungu ana dini ya watu safi. Sheitwani Ibilisi naye ana dini yake chafu ya kuzimu.
Hapo upo?
Mwanadamu ajihadhari sana sana asije akawa anaikimbilia baharini akidhamiria kuikwepa mvua.
Siku binadamu akitambua kwamba hana amri kuhusu maisha yake, basi huo utakuwa uvumbuzi mkuu mno kuliko nadharia na mavumbuzi yote ya wanasayansi kwa pamoja.
Dini/Religion- Way of life, belief and practices.Nipe tofauti mkuu ili nisichanganye hayo mambo mawili
Bob, siyo tu kwamba hakuna maisha nje ya dini.Kwa maelezo hayo unamaanisha kwamba hakuna maisha pasipo na dini? Kama ni hivyo basi dini ni jambo muhimu sana kwa mwanadamu.
Pia naomba unijuze maana ya neno dini huenda mimi naelewa tofauti
Umetofautisha vyema kabisa, na vipi kuhusu sheria zilizomo ndani ya dini husika, je ni Mungu wao ndyo huzitoa au ni wao kwa utashi wao wenyewe?Dini/Religion- Way of life, belief and practices.
Mungu/Miungu- Supernatural being/power.
All religions have the potential to bring humanity peace of mind, Calmness, Compassion etc. Question is Where does your peace and gentleness come from? That is your religion.
Mkuu nimekupata, inamaana ambao wanakataa uwepo au kukubaliana na dini bado hawana sifa za kuwa wanadamu?Bob, siyo tu kwamba hakuna maisha nje ya dini.
Ni kwamba hakuna personality inayoitwa mwanadamu bila dini.
Naweza kusema pasi na shaka kwamba ndani ya zile herufi herufi kwenye DNA ya mwanadamu, ambazo wajenetikia hujivunia kama uvumbuzi wa karne, zichunguzwe upya kuna codes za dini humo.
I may sound almost fictitious, but I know I'm not wrong.
Unajua kuna vitu automatically wala havihitaji mtu awekewe sheria au makatazo ndio ajue kwamba ni vibaya.Nimesoma na nimewaelewa, ila bado sijapata jibu la ingekuwa vipi maisha bia sheria na makatazo
Hao mie nawafananisha na akina Elon Musk wanaopania kuikimbia dunia na pia kukwepa kifo kibinadamu.Mkuu nimekupata, inamaana ambao wanakataa uwepo au kukubaliana na dini bado hawana sifa za kuwa wanadamu?
Kwa maana hiyo sheria za dini pia zina umuhimu wake au sheria za mwanadamu tu zinatosha kutoa muongozo wa namna ya kuishi?Sheria ni jambo la msingi sana ili binadamu huyu akitaka kubadilika ajue kwamba sheria itamwajibisha.
Mimi sina dini wala imani ya aina yeyote ile.Bob, siyo tu kwamba hakuna maisha nje ya dini.
Ni kwamba hakuna personality inayoitwa mwanadamu bila dini.
Naweza kusema pasi na shaka kwamba ndani ya zile herufi herufi kwenye DNA ya mwanadamu, ambazo wajenetikia hujivunia kama uvumbuzi wa karne, zichunguzwe upya kuna codes za dini humo.
I may sound almost fictitious, but I know I'm not wrong.
Sawa mkuu, pia uhuru wa kuchagua ndyo chanzo cha yote hayo. Lakini kama ulivyo sema mwisho tunarudi tulipo anziamwisho wa siku anarudi palepale kwenye kituo cha mwanzo alikoanzia safari.
Kila Mungu, Miungu lazima iwe na dini- way of living, practicing, believes.Umetofautisha vyema kabisa, na vipi kuhusu sheria zilizomo ndani ya dini husika, je ni Mungu wao ndyo huzitoa au ni wao kwa utashi wao wenyewe?
🎙️FA rocks
Mkuu lakini Buddhist si wanayo masanamu na wameyaweka ndani? Wanaomba na kutoa shukurani. Je ile sio Miungu yao?Kila Mungu, Miungu lazima iwe na dini- way of living, practicing, believes.
Si kila dini lazima iwe inainvolve Mungu, zipo dini ambazo haziamini Mungu/super natural being mfano mzuri ni Buddhism.
Aliwahi kuulizwa His Holiness, the Dalai Lama kwenye series ya “Searching For God In America”
Do Buddhists believe in God?
Majibu yake yakawa haya hapa
"If “God” is Ultimate Truth, Ultimate Energy, Infinite Love, then yes Buddhists believe in God But If “God” is a supernatural creator being, then no Buddhists do not believe in God.
Kwanza sheria zote ni za kibinadamu. Ziwe za kidini au kiserikali zote zimetungwa na wanadamu.Kwa maana hiyo sheria za dini pia zina umuhimu wake au sheria za mwanadamu tu zinatosha kutoa muongozo wa namna ya kuishi?
Mkuu ni vipi unathibitisha kwamba sheria za dini zimetungwa na mwanadamu?Kwanza sheria zote ni za kibinadamu. Ziwe za kidini au kiserikali zote zimetungwa na wanadamu.
Sheria za mwanadamu tu zinatosha kutoa muongozo wa namna ya kuishi.
Hizi sheria za dini ni nyongeza tu, hazina jipya zaidi ya kurudia sheria zilezile za mwanadamu ambazo automatically anazijua bila hata kuambiwa.
Mfano usiue, usiibe, usitamani mke wa mwingine. Hizi wala huhitaji dini ikwambie. Yani hata asiye na dini anajua automatic kwamba hapaswi kuua, kuiba au kutembea na mke wa mtu.
Kwa vile hata wewe binafsi hupendi ufanyiwe hivyo.
Mojawapo ya mtu aliyetunga sheria za dini ni Mussa, Musa alikuwa mwanadamu.Mkuu ni vipi unathibitisha kwamba sheria za dini zimetungwa na mwanadamu?
Ni wapi mussa alisema yeye ndiye mtungaji wa sheria hizo?Mojawapo ya mtu aliyetunga sheria za dini ni Mussa, Musa alikuwa mwanadamu.
Kwanza inabidi ukubali hakuna aliyewahi kukutana, kumuona au kuongea Na Mungu.Mkuu ni vipi unathibitisha kwamba sheria za dini zimetungwa na mwanadamu?