Mbona wanalalamikiwa kwa ushoga na kuwabagua wakristo??
Ushoga upo karibia kila nchi kwa kwa hiyo wanaolalamika basi na walalamikie Tanzania pia lakini kulalamika kwamba ushoga upo Israel pekee au as if chanzo ni wayahudi hizo ni chuki binafsi.
Kuhusu kuwabagua wakristo kwa maana ya kwamba kuna wayahudi wanawabagua wakristo nii sawa kwa sababu haiwezekani wayahudi wote 100% wakaupenda ukristo lakini kuna wayahudi wengi sana wakristo tena walokole. Ila kuna watu wenye chuki zao ambao hueneza propaganda wakimaanisha wayahudi woote wanauchukia ukristo au huo eti ni msimamo wa serikali ya Israel huu ni uwongo.
Ingekuwa wayahudi wengi wanawachukia wakristo kwa jinsi inavyosemwa basi wasingeruhusu wakristo kuingia Israel lakini kila mwaka wakristo kibao wanaenda kutembelea Israel kujifunza, na kufanya maombi.
Nimalizie kwa kusema Tangu taifa la Israel limeana kuasisiwa kumekuwa na chuki kubwa isiyo kifani juu yake ndiyo maana Farao aliwatumikisha vibaya walipokuwa misri pamoja na historia nzuri sana ya myahudi aitwaye Yusufu kuitumikia misri kwa uaminifu mkubwa uliotukuka. Wakiwa wanatoka Misri kwenda Kaanani walipigana vita nyingi sana njiani, kuingia Kaanani kulikuwa kwa vita, walipigwa vita na akina Hamani, walipigwa vita na dola ya rumi, na wakateswa mnooo, waliuwawa wayahudi wengi sana na Hitler, na ndiyo maana wayahudi wengi walipenda kwenda kuishi USA na guess what USA imekuwa taifa kubwa kwa miaka kadhaa kwa sababu ya mchango wao mkubwa sana maana wamebarikiwa na Mungu tokea kwa baba yao Ibrahimu.
Shetani ana hasira kubwa mno na taifa la Israel simply sababu Yesu alizaliwa kutokea kwa wayahudi ambapo amekuwa mwokozi wa ulimwengu na kupitia yeye binadamu amepatana tena na Mungu endapo atamwamwini Mungu na atatubu dhambi, makosa na uovu wake.
Ndiyo maana vita ya mwisho ya duniani ni kati ya mpinga kristo yaani majeshi ya nchi zote na nchi ya Israel. Ashukuriwe Yesu ambaye atashuka kuja kumaliza hiyo vita then atatawala dunia nzima na Yerusalemu yatakuwa makao makuu ya serikali ya Yesu Kristo.