IPP Media na Clouds Media uzeni kampuni zenu kwa wawekezaji vijana, bado mpo kizee sana

Nahizo ndio media ambazo habari zake zinaaminika kuliko media yyte ukisikia habari popote usitangaze akikisha unasikiliza kutoka katika hizo media kwnza
 
1080p pia nayo ni HD sio lazima uiite full HD. Hata youtube wameipa 1080p jina la HD kutokana na technolojia kukua.

Pia uang'avu wa 1080p unajulikana hata ukiuangalia kwa macho. 720p haina uang'avu wa namna ile kwenye screen kubwa ya 55inch.

Ila sikupingi just nimetoa tofaut ya HD na FHD

Kwa Azam nawez kubal kama HD yao walimaanisha FHD ya 1080p
 
Ila sikupingi just nimetoa tofaut ya HD na FHD

Kwa Azam nawez kubal kama HD yao walimaanisha FHD ya 1080p
Lakini pia resolution ya 1920x1080 unaweza kuset kwenye Decoder yako kama inaruhusu kwamfano mimi nabadilishaga kwenye Decoder yangu ya DSTv Explora, sijajua kwenye Azam Tv kama wana hiyo feature
 
Kumzidi kwenye nini mkuu? Youtube ni standard platform ya video sharing. Ni kama official gallery ya video
Kwenye Video, Twitter karuhusu video ndefu, pale YouTube kinachowafanya watu wabaki pale ni vichenji wanavyolipwa na YouTube
 
Umeongea point sana.. sana sana itv... Mfano mtu aliefariki miaka ya 2000 mwanzoni, leo akifufuka, hata ona mabadiliko yoyote itv....

Itv kuanzia utangazaji, watanagazaji, mfumo wa vipindi, matangazo .. yote ni yale yale ya miaka ya zamani
 
Kwa tz azam Media kajitaida xnaa na tunapoelekea anazid kutisha...natamn siku moja waanze kuonesha ligi ya England hapo sitokuwa na cha kuwadai
 
Umewasahau STAR TV [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hawa wanadunia yao ya kabla ya uhuru
 
Lakini pia resolution ya 1920x1080 unaweza kuset kwenye Decoder yako kama inaruhusu kwamfano mimi nabadilishaga kwenye Decoder yangu ya DSTv Explora, sijajua kwenye Azam Tv kama wana hiyo feature
decoder inaweza kuruhusu lkn kama channel hain ni haina tu
 
Bora CMG ila IPP ni achokile sana
Mfano, ITV, EATV na EA Radio wanatia huruma sana . Angalia studio zao na Hali ya baadhi ya waandishi wao, achokile sana

Sema kwa ITV huwa napenda kuangalia taarifa ya habari ya saa mbili tu na tena msomaji awe Odana Madai au Farhia Middle🥰 (yeye anatamka Midle ila mimi najua ni Modo)

EATV hata kuajiri hawawezi yaani waandishi ni wale wale akina Exhaud Mtei, Donald Mtani , Kisa Daniel na Samsoni Charles

Sema biashara ya matangazo inayoingizaa kipato imekuwa ngumu sana kutokana na kukua kwa teknolojia

CMG kupitia Clouds TV na Clouds FM wako vizuri sana , ni wabunifu sana na sijawahi kuchoka kusikiliza au kutazama vipindi vyao ninapopata muda

Natamani siku moja nikutane na Farhia Middle na Odana Madai🥰
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…