Iran ni nchi ya maajabu sana

Asante mkuu kwa haya uliyoyaandika.
Wakati sisi tunaandika mambo yenye uhalisia, wengine wanaleta story za kwenye vitabu vya dini, huku wakisahau kuwa hata huyo msaudia na nchi zingine za falme za kiarabu ni waislamu lkn ni maadui wakubwa wa huyu jemedari wa vita na silaha.
 
Mimi siongelei mambo ya dini, bali uwezo wa kijeshi wa nchi ambayo iliwekewa vikwazo vya kijeshi miaka zaidi ya 50, lkn bado ni tishio kwa waliomuwekea vikwazo hivyo.
 
Jibu ni moja Wana akili za uvumbuzi kama tuu Koreans zote..

Hiki ni kipawa kama vipawa vingine..

Na bado wanatoa misaada na kukopesha Nchi zingine ikiwemo Tanzania 👇
 

Attachments

  • FWWvd0BWYAAm2L4.jpg
    63.9 KB · Views: 8
Mkuu agiza supu ya njiwa nakuja kulipa. Jamaa anajifanaya ana elimu kuhusu mamb haya tunayojadili.

Lakini cha kushangaza ameshindwa kuonesha elimu yake hata namna ya kuandika nchi husika 😂😂😂
 
Mkuu huyu jamaa ukimsoma kwa makini utagundua kuwa ni wale vijana wenye mihamko fulan ambayo haina ulazima wa kuitaja.

Ila kiuhalisia hawana fact yoyote ya kuandika hapa.
 
Kuna akili inanambia tz nasisi tungewekewa vikwazo tangu Uhuru tungekua Kama Iran.
Bila kuwa na asili ya akili kubwa kama Iran kamwe hamuwezi kutoboa.

Angalia wenzenu Cuba, Venezuela, Libya na nyinginezo nyingi zilivyoomba poo kwa vikwazo vya miaka michache tu, tena vikwazo vya kiuchumi na sio silaha.
 
Baki na propaganda zako ulizolishwa na magharibi mkuu.
Ukiona mtu anakimbilia kumwambia mwenzake amelishwa propaganda na upande flani basi jua fika kwamba hana uelewa na issue anayoiongelea. Mbona wewe hujaambiwa uliyoandika ni propaganda?
 
Ukiona mtu anakimbilia kumwambia mwenzake amelishwa propaganda na upande flani basi jua fika kwamba hana uelewa na issue anayoiongelea. Mbona wewe hujaambiwa uliyoandika ni propaganda?
Mfano huu ulioutoa pia uelekeze kwa Israel. Ukiona Israel inapiga kelele kuwa Iran iendelee kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kijeshi, jua yenyewe haijiamini, inahofia Iran ikiachwa huru itamuacha mbali kisilaha na kiuchumi?

Pia jiulize mbona Iran haijawahi kuomba au kulalamika kuwa Israel iwekewe vikwazo vya kijeshi, uchumi nk?
 
Unazijua Nordic countries? Norway, Sweden, Denmark and Finland? Wana democracy ya kutosha na maendeleo makubwa. Ndiyo nchi zinaongoza kwa raia wake kuwa na furaha. Nchi yoyote inayoongozwa kidikteta tambua hilo linafanyika kwa faida ya watawala. Na ukikuta raia anashadidia utawala wa kidikteta basi tambua huyo raia hana hata uwezo wa kujiendesha yeye mwenyewe na pia kuiendesha familia yake. Ni raia ambaye kwanza haamini kabisa kwamba yeye kama yeye anauwezo wa kuwa na mchango kwenye jamii anayoishi, yaani maisha yake yoooteee huwa anategemea msaada wa mamlaka au mtu mwingine. Hasara ya raia wa aina hii ni pamoja na UCHAWA PRO MAX, majungu na kufuatilia maisha ya wengine, wivu mkubwa na chuki kwa waliofanikiwa na mwisho hawezi kuwa na ubunifu au mchango wowote kwa jamii na familia yake kwa sababu huamini kuwa huo uwezo hana.
 
Ni hawa hawa Iran wenye uwezo wa kuifuta Isreal kwenye uso wa dunia kwa maneno ya mdomoni, usifanye mchezo na taifa la kiyahudi, level yao ni juu mara mia zaidi ya binadamu mwingine yoyote anayeishi duniani....Israel is blessed.
Acha kutuletea hekaya za Abunuwasi wewe! Israel inaendelea kuwepo kutokana na sapoti kubwa kutoka Marekani na nchi za Ulaya ambako Jewish Lobby is very powerful. Without American support Israel is a paper tiger fit only to frighten the cowards.
 
Hili Taifa unalolisifu Mungu aliwalaani siku nyingi na wengine aliwageuza manyani kutokana na kufuru zao kubwa. Hawa ni watu washenzi wasiomheshimu Mungu na binadamu wenzao. Hawa ndio kwa imani yenu walimkamata Yesu wakamsulubu na kumuua. Hawa hawamuamini Yesu wala Injili. Watu washenzi wa kiwango hiki wanawezaje kuwa Taifa teule.
 
Iran imekataa kutawaliwa na ukoloni mamboleo, na ni nchi inayosimamia raslimali yake kubwa ya mafuta na gesi kwa manufaa yake. Hilo ndiyo chanzo ya ugomvi na nchi za Magharibi.
Ni nchi mmojawapo ya Kiislamu inayo ongoza kuelimisha wanawake.
 
Iran ni nchi imara tena tajiri wa mali na utamaduni.
Ila tatizo iran huenda ikajikanga kwa mafuta yake yenyewe kwa kujiwekea sera na itikadi isiyo na tija kiuchumi kwa wananchi wake.
Mapinduzi ya kidini yana faida gani? Badala ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi yenye kufaidisha umma wao wanaua hadi wanawake kwa kutovaa hijab. Polisi wa maadili wanahangaika kusimamia watu waingie misikitini kusali. Sasa wakishasali inasaidia nini kiuchumi.
Kiuchumi iran wanaendeleza uchumi wa kibepari wanasema uislamu unaruhusu kulimbikiza mali kibepari.
Kwa hivyo iran haina sera ya kuona usawa na haki kwenye mgawanyo wa keki ya taifa.
Kwa kuwalazimisha wananchi kusali na wanawake kuvaa hijab ni mambo hayana faida yoyote na uchumi wao.
Siku si nyingi tutazamie mapinduzi ya kidini kusambaratika iran na pengine kurithiwa na mapinduzi ya kiuchumi kwa wavuja jasho kuchukua hatamu ya dola ili kupata uhuru wa nafsi zao na uhuru kiuchumi.
 
Acha kutuletea hekaya za Abunuwasi wewe! Israel inaendelea kuwepo kutokana na sapoti kubwa kutoka Marekani na nchi za Ulaya ambako Jewish Lobby is very powerful. Without American support Israel is a paper tiger fit only to frighten the cowards.
Wewe unafikiri innovations zinazotumia akili kubwa huko marekani na ulaya zinafanywa na nani kama siyo waisreali wanaoishi huko, unafikiri wanawakumbatia kindezi............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…