Iran ni nchi ya maajabu sana

Uzi mrefu ila ni porojo tupu na matangopori.

Iran pamoja na utajiri wake mkubwa wa mafuta na eneo kubwa

GDP ya Iran ni billioni 191USD, wakati ya Israel ni billioni 402USD.

Kipato cha mtu kwa mwaka Iran ni USD 2,200 wakati Israel ni USD 43,000.
 
Mkuu mimi ni mwamini wa dini!!
Lakini kwene uchanbuzi hatulinganishi vitu hivo!! Aidha unachanganya mambo sana Shekhe!! na nina uhakika u wa mlengo huo!!
“Israeli ni taifa teule” kidini na kihistoria No doubt
-hata kwen Quran ipo hyo na waarabu au wanaokijua kitabu wanaelewa

Kiuhalisia sasa!
-Usichanganye kati ya akili na Power (Nchi za Africa wenye akili ndyo masikini na wenye power hawana akili so ivi vitu n touti)

-Utajiri na Akili ( Ingawa vinashabihiana lakini si mara zote vinaenda sambamba) -utajiri n matokeo ya mazingira,fulsa na maamuzi sahihi na wala haitegemei uwe genius!…. ndyo maana darasa la saba au mtu ambae hata hajasoma anaweza mzidi mtu aliokua anaongoza darasana

-Kutawaliwa na akili (vitu tofauti pia kutawaliwa ni matokeo ya kuzidiwa kiuchumi,kijeshi,kimabavu nk kama mtu yyte ana power atakutawala itachukua akili nyingi na muda mwingi kujinasua

-Waisrael wengi wana IQ kubwa lakini hyo haifanyi kua wao wawe matajiri kwasababu utajiri una formula yake ingawa akili ina mchango wake ! Mfano mdogo Africa Taifa lenye watu wenye akili zaidi ni Siera Lione, eritrea lakini izi nchi ndyo nchi masikini Africa haziko hata top 20 !! Nadhani unapa picha

-Israel imezaliwa 1948 (isael ya sasa) lakini walipofika leo huwezi kuringanisha na mataifa mengine yaliozaliwa mwaka huo!! nchi iliyozaliwa Jagwani!
Alafu uilinganishe na nchi za ulaya kama britain yenye karne kadhaa
Kifupi kwene kuringanisha kuna kanuni zake
“HUWEZI KUPIMA AKILI YA SAMAKI NA NYANI KWA KUWASHINDANISHA KUPANDA MITI”….
 
Nchi ya Iran ni hovyo sana, hakuna jambo lolote la maana la kimfumo kuiga huko katika utawala wa kidikteta wa ma-Ayatollah.

Uchumi wa South Africa umewaacha mbali sana hao waajemi, kama mnataka igeni mifumo ya bondeni au Algeria.
Nchi yetu kuwa na mifumo aina ile ya Iran bado sana. Itatuchukua miaka 50 na kina Magufuli kama 10 hivi ndo angalau tufikie nusu yake.
 
Nyanja zote za technolojia zinazohitaji akili kubwa ni wao, either wako marekani, ulaya au urusi. Usichokijua waisrael wametapakaa kote marekani, ulaya hadi urusi.
Kutapakaa sio tatizo maana hata waafrika, waarabu, wahindi, wachina nk wametapakaa dunia nzima.

1) Swali ni kwanini hizo nchi unazosema zinawategemea wa Israel zina uchumi mkubwa, teknolojia kubwa na nguvu kubwa za kijeshi kuliko Israel yenyewe?
2) Je hawapendi nchi yao iwe super power zaidi ya Marekan, China, Japan nk?
3) Au inakuaje kuaje hadi Israel ishindwe kufikia angalau nchi ya 5 kwa uchumi na nguvu za kijeshi duniani?

Maana leo hii hilo taifa lako teule linashindwa hata na India uchumi na nguvu za kijeshi.

Naomba unijibu maswali yang hayo matatu tu tafadhali, afu ndio tuendelee.
 
Korea Kaskazini ya Kiduku ni maskini kuliko Kenya na nchi nyingine nyingi za Africa.
Ukimpiga chura teke unampa mwendo zaidi,angalia Russian,North Korea,Irani,Hata akina China but matokeo ya kutumia akili zao wakijua maandui zao kamwe hawayataki maendeleo yao[emoji125][emoji125]
 
Nchi ya Iran ni hovyo sana, hakuna jambo lolote la maana la kimfumo kuiga huko katika utawala wa kidikteta wa ma-Ayatollah.

Uchumi wa South Africa umewaacha mbali sana hao waajemi, kama mnataka igeni mifumo ya bondeni au Algeria.
South Africa ina vikwazo vya kiuchumi?
Miaka ya 2000 kushuka chini SA ilikuwa imeachwa mbali kiuchumi na Zimbabwe, lkn leo baada ya vikwazo vya magharibi dhidi ya Zimbabwe ndo maana unaona iko mbali zaidi ya Zimbabwe na nchi nyingine zilizowekewa vikwazo.

So kama unatumia akili bila kuweka mihamko mbele, ni lazima utaona sababu ya uchumi wa Iran, Zimbabwe nk kuwa chini ya nchi zingine.
 
Ukiacha hizo silaha ulizozingumiza katika posti nzima na makapeti ya kukalia vitu gani vingine Iran wanatengeneza na kufanya biashara kubwa duniani??
 
Ndo hapo sasa wao ni taifa teule, yaani kuumiza kichwa juu yao ni kujisumbua........kuipoteza israel kwenye uso wa dunia ni sawa na dunia kufikia tamati. Maana Mungu hawezi kufanya jambo duniani bila uwepo wa taifa la Israel, yaani ni lango lake kwa jambo linalotakiwa lifanyike au litokee duniani.
 
Ni akili ndogo na za hovyo sana zinazoweza kutamani kuwa kama Irani katika karne ya 21
Kuna akili inanambia tz nasisi tungewekewa vikwazo tangu Uhuru tungekua Kama Iran.
 
Nitoe mfano wa kibinadamu, tuseme unao watoto 12..........ila kuna mtoto mmoja unayemwamini kumwachia maagizo, maelekezo au kuwasimamia wale wengine na yeye ndo unategemea akupe taarifa ya kitu gani kinaendelea. Ndo jinsi hiyo hiyo Mungu analichukulia taifa la Israel, yaani kalichagua miongoni mwa mataifa yote duniani kama mtoto pendwa anayeaminiwa na baba yake. Nafikiri hapa usipoelewa nitakuwa nimeshindwa mimi...
 
Naona kila ninapokuuliza swali la akili wewe unakwepesha kwepesha utafikiri labda kuna mtu unamuogopa humu JF. Hili ni jukwaa huru kwahiyo hutakiwi kuogopa kujibu unachoulizwa maana wengi hatujuani so jibu lako hata likiwa zuri kwang hakuna atakae ku block au kukutukana eti kisa umenijibu vizuri.

Btw akili ni nywele kila mtu ana zake. Wewe amini unachoamini na mimi naamini ninachoamini.
Shukran kwa kuchangia mkuu, ubarikiwe sana maana tumejadiliana kiutu bila matusi wala kejeli.

Mchana mwema bro
 
Nisome hapo juu nimetoa mfano wa kibinadamu ambao huenda ni rahisi kwako kuelewa namna Mungu anavyolichukulia taifa la Israel dhidi ya mataifa mengine ya ulimwengu, kawapa baraka zote hizo ikiwemo kipawa cha akili na maarifa sababu kawachagua kwa ajili yake miongoni mwa mataifa.
 
Iran mnayoisifia ni hii maandamano kila kukicha wanamsingizia USA anahusika na ishu yao ya kuua Raia mimi nimeona ni Taifa la ajabu kwa kuua raia wake kwa kigezo cha kitu fulani dini inakataza yaani hiyo pepo ya kulazimishana mpaka kuuana pepo gani hiyo..
 
Wewe na ukoo wenu ndio mtakuwa mnaamua Rais gani ana maono au hana maono??
Unahitaji maono kuigeuza nchi kuwa ya wamachinga, bodaboda na mama ntilie?
 
Mfano wako hauna mantiki yoyote, kwa sababu uwezo wa kibinadam na kimungu ni tofauti.

Binadam unaweza kumchagua labda mtoto wako wa kike bila kujali umri awaongoze wanao wakiume baada ya pengine kuona wale wakiume tabia zao na mienedo yao sio mizuri na wewe kama binadam hauna namna ya kuwabadilisha ili wawe kama vile unavyotaka wewe.
So hapo ndo unaamua kuchagua mmoja wa kuwaongoza.

Lakini Mungu yeye hawezi kuchagua mmoja kwa sababu yuko na uwezo wa kuwafanya wote wakawa na uwezo mmoja na wakaongozana bila kubagua yoyote kati yao.

Hayo ya kuchagua taifa 1 tu na makabila 12, ndio yamefanya wachina kushtuka mapema. Maana ni kama vile fursa imetengenezwa kijanja na wajanja fulan wa hayo makabila kupitia mgongo wa dini. So mchina kakataa kushikiwa akili namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…