Iran ni nchi ya maajabu sana

Iran ni nchi ya maajabu sana

Uzi mrefu ila ni porojo tupu na matangopori.

Iran pamoja na utajiri wake mkubwa wa mafuta na eneo kubwa

GDP ya Iran ni billioni 191USD, wakati ya Israel ni billioni 402USD.

Kipato cha mtu kwa mwaka Iran ni USD 2,200 wakati Israel ni USD 43,000.
Wakuu vipi, kwema.

Wakuu Iran ni mmoja kati ya nchi ambazo ziliwekewa vikwazo vikali na nchi za magharibi toka mnamo mwa miaka ya 70s huko hadi leo hii na siku zijazo.

Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, kijeshi nk, tena vimekuwa vikiongezwa siku hadi siku.

Tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine kama vile Cuba, Venezuela nk zilizowekewa vikwazo pengine na marekan tu, au baadhi ya nchi za magharibi. vikwazo vya Iran vimewekwa na nchi za magharibi kama zote wakishirikiana na makampuni ya nchi hizo.

Lakini cha kushangaza Iran imeweza kuwa na uwezo hasa wa kijeshi sawa au pengine zaidi ya ule wa nchi ambazo hazijawahi kuwekewa vikwazo na nchi hizo.

Iran ni miongoni mwa nchi zenye eneo kubwa na watu wengi barani Asia, so pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa takriban miaka 50 na zaidi, lkn wameweza kuwa na mifumo mizuri ya kudhibiti hali ya umasikini nchini mwao, tofauti na nchi kama Venezuela ambazo vikwazo vya miaka miwili au mitatu vimesababisha mamilioni ya raia waishi maisha ya shida na ya umasikini kupita maelezo.

Pamoja na vikwazo vikali vya magharibi hasa kwa upande wa mambo ya ulinzi, lkn bado nchi hiyo imeweza kuonesha kuwa haipo chini au nyuma kijeshi hata siku moja. Wengi tuliona jinsi wa Iran walivyoziangamiza ndege zisizo na ruban zilizokuwa zinatumiwa na Marekan kupima upepo katika eneo lao, wengi tuliona jinsi Iran ilivyozilipua meli ambazo zilikuwa zinabeba wapelelezi mbali mbali wa magharibi karibu na eneo lake, wengi tuliona jinsi Iran ilivyoshambulia kambi kadhaa za Marekani kule Iraq na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika kambi hizo baada ya Mmarekani kumuuwa mmoja wa maofisa wakubwa wa Iran kule Iraq, tena kabla ya kufanya mashambulizi hayo wa Iran walitoa taarifa mapema kuwa watalipiza kisasi kupitia kambi za wamarekan kule Iraq, so marekan ikajiandaa kuzuia shambulizi lkn mwisho wa siku shambulizi likashindikana kuzuilika na kuleta maafa kwa jeshi la nchi hiyo kubwa duniani.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyotoa msaada wa silaha kwa kundi la hezbullah ambalo liliichachafya Israel inayopata msaada mkubwa wa fedha kutoka Marekani kwa ajili ya ulinzi wao. Hiyo ilikuwa mwaka 2006 hadi jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuomba ipatekane suluhu ya kudumu baina ya Israeli na hezbullah.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyosimama na kumlinda Asad wa Syria katika vita vyake, hadi kupelekea mipango ya Marekani na nchi za magharibi kumng'oa imeshindikana.

Wengi tunashuhudia sasa jinsi silaha kidogo tu za ndege zisikuwa na rubani za Iran zinavyofanya uharibifu mkubwa, na kusababisha maafa makubwa na zaidi ya yale yaliokuwa yanafanywa na Russia kupitia silaha zake mwenyewe (Russia) huko Ukraine.
Mpaka Marekani na nchi zingine za magharibi zinapiga kelele, maana silaha zinazotumika sio zile za Russia ambazo zilikuwa zinampa jeuri raisi wa Ukraine kuona kwamba sasa vita vimekwisha.

Hata zile himars za Marekani sasa hivi zinaonekana hazifanyi kazi mbele ya maangamizi ya ndege hizi za Iran.

Sasa tujiulize, kama nchi iliyowekewa vikwazo na mataifa makubwa duniani kwa zaidi ya miaka 50 bado ina uwezo iliyo nao leo, sasa je kama isingewekewa vikwazo kwa miaka yote hiyo 50 leo ni nchi gani ambayo ingeitisha pale Asia na hata duniani kwa ujumla.

Hizo nilizosema hapa ni zile silaha ilizotoa kuwawezesha hao niliwataja washinde mapambano yao, hapo hatujazungumzia silaha zake mwenyewe alizoweka kwa lengo la kujilinda ambazo kwa sheria za kijeshi duniani huwa zinafanywa siri kubwa ili adui asizione.

Mpaka sasa Marekani na nchi za magharibi zinashindwa kujua ni njia gani nyingine ya kumdhibiti huyu mtemi, maana wamarekani waliwahi kumtumia msaudi mwaka jana, hapo hapo Iran hakuchelewesha akaangamiza mitungi yake mikubwa ya kuwekea mafuta mpaka saudia na dunia ikapiga kelele.

Hili taifa ni la maajabu sana, japo lina maadui wengi lililotengenezewa na nchi za magharibi na halipati msaada wa kifedha kutoka kwa nchi yoyote lkn bado linajiamini kupita maelezo.

Mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe, namaanisha ukiona nchi za magharibi na vibaraka wao wanapambana kwa hali na mali dhidi ya uchumi na ulinzi wa kijeshi wa nchi moja, basi jua kwamba wamagharibi hao wameshagundua kwamba nchi hiyo ni hatari maradufu kwa mustakabali wa uchumi wao pamoja na ulinzi wao.
 
Tatizo lenu nyinyi mmeng'ang'ania kuamini mambo yalioandikwa kwenye vitabu na sio yale mnayoyaona au kuyatafakari wenyewe.

1) Wa Israel wangekuwa na akili unayosema wasingefanywa watumwa huko Misri (Afrika)

2) Wa Israel wangekuwa na akili wasingeruhusu warumi waingie katika nchi yao na kufanya waliyoyafanya. Kumbuka warumi asili yao ni ulaya. Sasa kama unaamini nchi za ulaya zinaitegemea Israel ilikuje anaetegemewa (Israel) atawaliwe na anaemtegemea (mzungu) hii inaingia akilini kweli?

Wa israel wangekuwa na akili unayosema wasingeangamizwa na Hitler Mzungu tena ni miaka 50 au 70 tu iliyopita, wakati wazungu wameanza kuitawala dunia au sehem kubwa ya dunia miaka zaidi ya elfu iliyopita.

SWALI LA MWISHO:

Kama Israel inategemewa na wazungu inakuaje nchi za wazungu ndio zenye nguvu za kijeshi, uchumi mkubwa na maendeleo ya kiteknolojia zaidi ya Israel yenyewe?

Yan nchi yenye wataalam bado inategemea msaada wa kifedha na kijeshi kutoka kwa wale inaowasaidia, hii inaingia akilini kweli?

Sawa vitabu vya dini tusome lkn na akili zetu pia tuzitumie kufanya tasmini ili kujua ukweli wa mambo.

Israel ingekuwa na sifa hizo unazozisema hapa. Basi leo ndio ingekuwa nchi ya kwanza kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia, ila kwa vile hawana sifa hizo mlizomezeshwa ndo maana leo iko nyuma hata ya China.

Acheni kuweka mambo ya dini kwenye mambo muhimu.
Mkuu mimi ni mwamini wa dini!!
Lakini kwene uchanbuzi hatulinganishi vitu hivo!! Aidha unachanganya mambo sana Shekhe!! na nina uhakika u wa mlengo huo!!
“Israeli ni taifa teule” kidini na kihistoria No doubt
-hata kwen Quran ipo hyo na waarabu au wanaokijua kitabu wanaelewa

Kiuhalisia sasa!
-Usichanganye kati ya akili na Power (Nchi za Africa wenye akili ndyo masikini na wenye power hawana akili so ivi vitu n touti)

-Utajiri na Akili ( Ingawa vinashabihiana lakini si mara zote vinaenda sambamba) -utajiri n matokeo ya mazingira,fulsa na maamuzi sahihi na wala haitegemei uwe genius!…. ndyo maana darasa la saba au mtu ambae hata hajasoma anaweza mzidi mtu aliokua anaongoza darasana

-Kutawaliwa na akili (vitu tofauti pia kutawaliwa ni matokeo ya kuzidiwa kiuchumi,kijeshi,kimabavu nk kama mtu yyte ana power atakutawala itachukua akili nyingi na muda mwingi kujinasua

-Waisrael wengi wana IQ kubwa lakini hyo haifanyi kua wao wawe matajiri kwasababu utajiri una formula yake ingawa akili ina mchango wake ! Mfano mdogo Africa Taifa lenye watu wenye akili zaidi ni Siera Lione, eritrea lakini izi nchi ndyo nchi masikini Africa haziko hata top 20 !! Nadhani unapa picha

-Israel imezaliwa 1948 (isael ya sasa) lakini walipofika leo huwezi kuringanisha na mataifa mengine yaliozaliwa mwaka huo!! nchi iliyozaliwa Jagwani!
Alafu uilinganishe na nchi za ulaya kama britain yenye karne kadhaa
Kifupi kwene kuringanisha kuna kanuni zake
“HUWEZI KUPIMA AKILI YA SAMAKI NA NYANI KWA KUWASHINDANISHA KUPANDA MITI”….
 
Nchi ya Iran ni hovyo sana, hakuna jambo lolote la maana la kimfumo kuiga huko katika utawala wa kidikteta wa ma-Ayatollah.

Uchumi wa South Africa umewaacha mbali sana hao waajemi, kama mnataka igeni mifumo ya bondeni au Algeria.
Nchi yetu kuwa na mifumo aina ile ya Iran bado sana. Itatuchukua miaka 50 na kina Magufuli kama 10 hivi ndo angalau tufikie nusu yake.
 
Nyanja zote za technolojia zinazohitaji akili kubwa ni wao, either wako marekani, ulaya au urusi. Usichokijua waisrael wametapakaa kote marekani, ulaya hadi urusi.
Kutapakaa sio tatizo maana hata waafrika, waarabu, wahindi, wachina nk wametapakaa dunia nzima.

1) Swali ni kwanini hizo nchi unazosema zinawategemea wa Israel zina uchumi mkubwa, teknolojia kubwa na nguvu kubwa za kijeshi kuliko Israel yenyewe?
2) Je hawapendi nchi yao iwe super power zaidi ya Marekan, China, Japan nk?
3) Au inakuaje kuaje hadi Israel ishindwe kufikia angalau nchi ya 5 kwa uchumi na nguvu za kijeshi duniani?

Maana leo hii hilo taifa lako teule linashindwa hata na India uchumi na nguvu za kijeshi.

Naomba unijibu maswali yang hayo matatu tu tafadhali, afu ndio tuendelee.
 
Korea Kaskazini ya Kiduku ni maskini kuliko Kenya na nchi nyingine nyingi za Africa.
Ukimpiga chura teke unampa mwendo zaidi,angalia Russian,North Korea,Irani,Hata akina China but matokeo ya kutumia akili zao wakijua maandui zao kamwe hawayataki maendeleo yao[emoji125][emoji125]
 
Nchi ya Iran ni hovyo sana, hakuna jambo lolote la maana la kimfumo kuiga huko katika utawala wa kidikteta wa ma-Ayatollah.

Uchumi wa South Africa umewaacha mbali sana hao waajemi, kama mnataka igeni mifumo ya bondeni au Algeria.
South Africa ina vikwazo vya kiuchumi?
Miaka ya 2000 kushuka chini SA ilikuwa imeachwa mbali kiuchumi na Zimbabwe, lkn leo baada ya vikwazo vya magharibi dhidi ya Zimbabwe ndo maana unaona iko mbali zaidi ya Zimbabwe na nchi nyingine zilizowekewa vikwazo.

So kama unatumia akili bila kuweka mihamko mbele, ni lazima utaona sababu ya uchumi wa Iran, Zimbabwe nk kuwa chini ya nchi zingine.
 
Ukiacha hizo silaha ulizozingumiza katika posti nzima na makapeti ya kukalia vitu gani vingine Iran wanatengeneza na kufanya biashara kubwa duniani??
Mwenye akili na mfuatiliaji kuhusu Iran anajua kwanini anachungwa sana na kuzuiwa kufanya mengi na hata vikwazo vingi kuwekewa

Iran ana wataalamu wengi sana na ni akili kubwa
Amejiwekeza kwenye maendeleo na kutengeneza silaha mwenyewe kama wazungu wanavyofanya kwa nchi zao

Woga wa wazungu uliwafanya watafute nchi itakayopigana na Iran kwa kuwa tu wanaogopa ipo siku ataishika Saudia
Na Saudia ni kibaraka wa wazungu huku akiwauzia mafuta na wao wakijenga nchi za GCC kwa kupata ukandarasi wote

Hapo wakamshawishi Iraq aingie vita ya bila kichwa wala miguu kwenye mto wa Shat Al Arab ambapo kwa bahati nilikuwa huko na kushuhudia vita zote mbili, hiyo ya 1980 na uvamizi tena wa Iraq huko Kuwait 1990

Iran wana wataalamu wengi sana wa masuala ya utengenezaji wa silaha na mengine mengi ila wanaogopwa sana eti kwa usalama wa ME lakini ukweli ni kuwa wanaemlinda ni Israel


Bora na sisi tuanze kununua silaha za Iran kama Rifles zao za Fajr
Wako vizuri kwa nyanja nyingi na wanatengeneza silaha nyingi sana za maangamizi ambapo kuna wengi humu watashangaa na hata kupinga kuwa jamaa yuko vizuri sana

List ya silaha anayotengeneza Iran ni ndefu sana yaani kama ningekuwa na uwezo wa kupata hata tenda ya kuanza na military uniforms tu halafu taratibu nikaanza kuuwauzia silaha hata bunduki 1000 tu kwa kuanzia

Kuna fursa duniani ila tumekazana za [emoji631] na [emoji636] tu huu ni utumwa na hautaisha
Tuna safari ndefu sana
 
Kutapakaa sio tatizo maana hata waafrika, waarabu, wahindi, wachina nk wametapakaa dunia nzima.

1) Swali ni kwanini hizo nchi unazosema zinawategemea wa Israel zina uchumi mkubwa, teknolojia kubwa na nguvu kubwa za kijeshi kuliko Israel yenyewe?
2) Je hawapendi nchi yao iwe super power zaidi ya Marekan, China, Japan nk?
3) Au inakuaje kuaje hadi Israel ishindwe kufikia angalau nchi ya 5 kwa uchumi na nguvu za kijeshi duniani?

Maana leo hii hilo taifa lako teule linashindwa hata na India uchumi na nguvu za kijeshi.

Naomba unijibu maswali yang hayo matatu tu tafadhali, afu ndio tuendelee.
Ndo hapo sasa wao ni taifa teule, yaani kuumiza kichwa juu yao ni kujisumbua........kuipoteza israel kwenye uso wa dunia ni sawa na dunia kufikia tamati. Maana Mungu hawezi kufanya jambo duniani bila uwepo wa taifa la Israel, yaani ni lango lake kwa jambo linalotakiwa lifanyike au litokee duniani.
 
Ni akili ndogo na za hovyo sana zinazoweza kutamani kuwa kama Irani katika karne ya 21
Kuna akili inanambia tz nasisi tungewekewa vikwazo tangu Uhuru tungekua Kama Iran.
 
Nitoe mfano wa kibinadamu, tuseme unao watoto 12..........ila kuna mtoto mmoja unayemwamini kumwachia maagizo, maelekezo au kuwasimamia wale wengine na yeye ndo unategemea akupe taarifa ya kitu gani kinaendelea. Ndo jinsi hiyo hiyo Mungu analichukulia taifa la Israel, yaani kalichagua miongoni mwa mataifa yote duniani kama mtoto pendwa anayeaminiwa na baba yake. Nafikiri hapa usipoelewa nitakuwa nimeshindwa mimi...
 
Ndo hapo sasa wao ni taifa teule, yaani kuumiza kichwa juu yao ni kujisumbua........kuipoteza israel kwenye uso wa dunia ni sawa na dunia kufikia tamati. Maana Mungu hawezi kufanya jambo duniani bila uwepo wa taifa la Israel, yaani ni lango lake kwa jambo linalotakiwa lifanyike au litokee duniani.
Naona kila ninapokuuliza swali la akili wewe unakwepesha kwepesha utafikiri labda kuna mtu unamuogopa humu JF. Hili ni jukwaa huru kwahiyo hutakiwi kuogopa kujibu unachoulizwa maana wengi hatujuani so jibu lako hata likiwa zuri kwang hakuna atakae ku block au kukutukana eti kisa umenijibu vizuri.

Btw akili ni nywele kila mtu ana zake. Wewe amini unachoamini na mimi naamini ninachoamini.
Shukran kwa kuchangia mkuu, ubarikiwe sana maana tumejadiliana kiutu bila matusi wala kejeli.

Mchana mwema bro
 
Naona kila ninapokuuliza swali la akili wewe unakwepesha kwepesha utafikiri labda kuna mtu unamuogopa humu JF. Hili ni jukwaa huru kwahiyo hutakiwi kuogopa kujibu unachoulizwa maana wengi hatujuani so jibu lako hata likiwa zuri kwang hakuna atakae ku block au kukutukana eti kisa umenijibu vizuri.

Btw akili ni nywele kila mtu ana zake. Wewe amini unachoamini na mimi naamini ninachoamini.
Shukran kwa kuchangua mkuu, ubarikiwe sana maana tumejadiliana kiutu bila matusi wala kejeli.

Mchana mwema bro
Nisome hapo juu nimetoa mfano wa kibinadamu ambao huenda ni rahisi kwako kuelewa namna Mungu anavyolichukulia taifa la Israel dhidi ya mataifa mengine ya ulimwengu, kawapa baraka zote hizo ikiwemo kipawa cha akili na maarifa sababu kawachagua kwa ajili yake miongoni mwa mataifa.
 
Iran mnayoisifia ni hii maandamano kila kukicha wanamsingizia USA anahusika na ishu yao ya kuua Raia mimi nimeona ni Taifa la ajabu kwa kuua raia wake kwa kigezo cha kitu fulani dini inakataza yaani hiyo pepo ya kulazimishana mpaka kuuana pepo gani hiyo..
 
Wewe na ukoo wenu ndio mtakuwa mnaamua Rais gani ana maono au hana maono??
Unahitaji maono kuigeuza nchi kuwa ya wamachinga, bodaboda na mama ntilie?
Umenena vema mkuu hata ikikitooea rais bora mwenye maono watataoa atawale miaka mitano ampishe mwingine asiye na uelekeo thats why waliumwa na vichwa waliposikia tetesi Magufuli anataka abaki madarakani....

Ni ukweli mchungu pia hata huu unaoitwa upinzani ni mbinu ya mabeberu kuleta mbambamba kwenye mataifa yetu thats why upinzani kwa afrika umefeuka kua fujo na mapambano dhidi ya serikali zinazotawala

Kikubwa ni kwamba wameya design haya iwa makusudi kabisa na wanajua kabisa kwamba mazingira yao s kama yakwetu wao nchi kwanza mambo mengine yatafuata

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Nitoe mfano wa kibinadamu, tuseme unao watoto 12..........ila kuna mtoto mmoja unayemwamini kumwachia maagizo, maelekezo au kuwasimamia wale wengine na yeye ndo unategemea akupe taarifa ya kitu gani kinaendelea. Ndo jinsi hiyo hiyo Mungu analichukulia taifa la Israel, yaani kalichagua miongoni mwa mataifa yote duniani kama mtoto pendwa anayeaminiwa na baba yake. Nafikiri hapa usipoelewa nitakuwa nimeshindwa mimi...
Mfano wako hauna mantiki yoyote, kwa sababu uwezo wa kibinadam na kimungu ni tofauti.

Binadam unaweza kumchagua labda mtoto wako wa kike bila kujali umri awaongoze wanao wakiume baada ya pengine kuona wale wakiume tabia zao na mienedo yao sio mizuri na wewe kama binadam hauna namna ya kuwabadilisha ili wawe kama vile unavyotaka wewe.
So hapo ndo unaamua kuchagua mmoja wa kuwaongoza.

Lakini Mungu yeye hawezi kuchagua mmoja kwa sababu yuko na uwezo wa kuwafanya wote wakawa na uwezo mmoja na wakaongozana bila kubagua yoyote kati yao.

Hayo ya kuchagua taifa 1 tu na makabila 12, ndio yamefanya wachina kushtuka mapema. Maana ni kama vile fursa imetengenezwa kijanja na wajanja fulan wa hayo makabila kupitia mgongo wa dini. So mchina kakataa kushikiwa akili namna hii.
 
Back
Top Bottom