kahtaan
JF-Expert Member
- Jul 11, 2009
- 18,760
- 11,343
Hakuna binaadamu amekamilika.ni vile tu umeandika kwa mahaba ya dini.
Ukweli mapadri na masheikh wapo wenye vitendo vichafu kotekote.
Shida ni hujanielewa nina wsshkaji wakristo na waislamu wanlewa wikiendi halafu wanaenda kulala na wanawake chumba kimoja kila mtu na wake halafu akitoka hapo ijumaa msikitini, jlpili kanisani wakitoka huko wanarudia yale yale.
Ndio nakuuliza sheria za uislamu zinasema kwamba ukitubu unarudi kufanya halafu unarudi tena kutubu kwa makusudi kabsa ukijua unalifanya ni dhambi kwa mwenye mungu?
Na Kurudia madhambi ni asili ya binaadamu yyt.
Uislamu hautegemei wewe uwe msafi asilimia 100% bali unahimiza USIKATE TAMAA NA MSAMAHA WA MUNGU.
Kila ukijisahau ukafanya Dhambi ni wajibu wako KUOMBA TOBA na Kujitahidi Kuacha hio Dhambi.
Lkn ikitokea UKAFANYA tena Dhambi Muhimu ni kurudi kwa Mungu na Kufanya Toba.
Mzunguko huo utaendelea mpk siku utakapo kutana Na Mungu wako siku ya malipo.
Ndipo utahukumiwa .
Usije kusema sababu ulirudia dhambi kwahio HUNA MSAHAMA TENA.
Hapana.
Mungu anaweza kukusamehe hata km umerudia dhambi mara kwa mara.