Iran yageuza gia angani, yasema haitalipa kisasi kwa Israel kama wakisitisha vita Gaza

we ndo unawasemea??
we ni waziri wa ulinzi wa Iran
hiki n kichaa mkuu
 
Mmhh kweli kuna watanzania huwaambii kitu kwa israel, mpaka bendera kwenye magari yao wameweka na wanatembea nazo 🇮🇱

Al hamduliLlah najivunia sana sana kuwa Muislamu
 
Apa ndoo utaona tofauti ya Israel na Urrusi, yaan myahudi anakushughulikia faster haji kulalamika hovyo hovyo kama mrusis. Maana warusii utasikia mara ooooh magaidi yalikuwa yanaenda ukrane mara ooooh magaidi wametumwa na marekani, wazeee Israel hana pigo kama hizo
 
Mkuu,
Siyo kwa hawa magaidi wa sasa wa Kiarabu wanaoua hovyo watu wasio na hatia.
Ukiwachekea nyani utavuna mabua
 
Mkuu,
Siyo kwa hawa magaidi wa sasa wa Kiarabu wanaoua hovyo watu wasio na hatia.
Ukiwachekea nyani utavuna mabua

1. Mkuu, nakubaliana nawe kuwa gaidi si wa kuvumilia.

2. Zingatia tofauti ya HAMAS, Palestina na magaidi wale Boko Haram, ISIS au Al Shabab:

3. Kwa tafsiri ya Leon Panetta Ex-CIA, kwenye mzozo huu:

4. Mtambue mwenyewe anayeuwa watu hovyo hapo.

5. Ni muhimu consistent kwenye kushutumu; huwezi mshutumu Russia kule Ukraine ila ukawa na mahaba na Israel hapa!
 
1. Mkuu, nakubaliana nawe kuwa gaidi si wa kuvumilia.
Vizuri mkuu
2. Zingatia tofauti ya HAMAS, Palestina na magaidi wale Boko Haram, ISIS au Al Shabab:

Zingatia kuwa wakati Mandela anatamka hayo hawa magaidi wa Hamas walikuwa hawajakuwapo bado. Madiba asingeunga mkono hawa wahuni, wauaji..
5. Ni muhimu consistent kwenye kushutumu; huwezi mshutumu Russia kule Ukraine ila ukawa na mahaba na Israel hapa!
Russia alianza kuvamia Ukraine kama Hamas walivyoanza kuvamia Isreal. Kwa hiyo tupo consistent
 
Mpango wa Iran ni kuishinikiza Marekani amwambie jamaa yake Israel asitishe vita ya Gaza kwa kudumu.Iwapo atafanikiwa Iran ataongeza ushawishi mkubwa sana Mashabiki ya Kati kidiplomasia.Iran anaicheza vizuri sana hii karata pande zote mbili.Ngoja tusubiri kama Israel itakubali kumaliza vita yake,kukubali kumaliza vita ni ushindi mkubwa kwa Hamas.Hapo Netanyau atajiweka karibu sana kuangushwa utawala wake.
 
Vizuri mkuu

Maridadi; nathibitisha.

Zingatia kuwa wakati Mandela anatamka hayo hawa magaidi wa Hamas walikuwa hawajakuwapo bado. Madiba asingeunga mkono hawa wahuni, wauaji..

1. Mkuu wewe si nabii kudhani Madiba asingewaunga mkono. Zingatia SA wajukuu wa Madiba wako nao na kesi imeunguruma ICJ huko.

2. Zingatia pia ANC kama HAMAS na wapalestina njia zote za kudai uhuru wao ziliposhindikana walibeba silaha, watu walikufa na wa kuwaita wahuni, wauwaji na magaidi walikuwapo. Madiba mwenyewe alikuwa blacklisted kama gaidi.

3. Uzi huu na mada yake unahusika sana hapa:

Kama Maji Maji au Mau Mau ilikuwa halali, iweje lawama kwa wapalestina?

Russia alianza kuvamia Ukraine kama Hamas walivyoanza kuvamia Isreal. Kwa hiyo tupo consistent

1. HAMAS hakuanza mgogoro na Israel. Mgogoro huu upo tangia 1947 huko. Mgogoro huo Madiba kafa kauacha:

2. Au ni kauli yako kuwa mgogoro aliokuwa akiuongelea Madiba hapo ulikwisha?

3. Tumtafute mchokozi wa aina ya Russia hapa; kwani tunakubaliana Russia ni mwovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…