Iran yaishambulia Israel kwa makombora
Subiri how Israel will retaliate alafu ndio uje uongee, na USA yuko hapo, Iran hadi atapike na kukosa pumzi afe utaona


View: https://youtu.be/fILEjXQHOps?si=Vh2-8qKkPm1Cmdma

Punguza mahaba na jitahidi kufikiria ni kwanin marekani ameweka kambi nyingi za kijeshi kuizunguka Iran lakini anaogopa kuivamia, vita sio nyepesi maana haichagui myahudi feki wa kizungu Wala marekani pote inaleta madhara makubwa sana.

Huyo marekani mwenyewe Kambi zake za kijeshi zilipigwa na Iran je, alifanya niny! Kwa Iran mbona hakupiga ndani ya Irani.
 
Waajemi ni shida sana tatizo mnasoma vitabu vyenu ila hamjui kuwa hao watu nao wana matatizo sana sio wa kuchukuliwa poa...
 
Acha propaganda huo uwanja umepigwa na Israel yenyewe imekili na wametangaza kuufunga.
Wenzenu wakipiga target zao wanalenga watu muhimu ktk nchi na wanaondoka na uhai wao!

Wao (wairan) wanalenga material things ( viwanja vya ndege ) ambavyo Mimi naona havina impact yoyote. Thamani ya majenerali walio uawa huwezi kulinganisha na kiwanja Cha ndege, Hapo tu ndo wenzenu wanapokupigeni bao
 
Wenzenu wakipiga target zao wanalenga watu muhimu ktk nchi na wanaondoka na uhai wao!

Wao (wairan) wanalenga material things ( viwanja vya ndege ) ambavyo Mimi naona havina impact yoyote. Thamani ya majenerali walio uawa huwezi kulinganisha na kiwanja Cha ndege, Hapo tu ndo wenzenu wanapokupigeni bao
Unajifariji tu wewe Iran kamkamata kona mbaya muisraeli na bwanake mmarekani
 
Iran haiwezi kushambuliwa na nchi za West isipokuwa kama itafanya makosa ya kimahesabu katika kushambulia targets.
Mahesabu yalikuwa kushambulia wakati Israel/allies na mifumo yao ya ulinzi ikiwa on high alert kuliko siku zote. Ndio maana Iran ilikuwa ikitoa taarifa siku kadhaa kabla. Hayo ni mashambulizi ya kuonesha tu deterrence ama kwa lugha nyepesi, saving face.
 
Km zaidi ya 2000 kutoka Iran. Wameanza kuzuia kuanzia Iraq mpaka Jordan lakini mwanaume kashusha mzigo ndani ya israeli wayahudi wa mchongo mko wapi
Kiongozi Gani alie uliwa hapo uyahudini?? Nitonye pengine Mimi Sina taarifa. Wenzenu wakipiga wanapiga kweli sasa nyie mnapiga kiwanja Cha ndege kitupu?? Mimi mpaka hapo Bado sijaona kisasi Cha iran kwa muyahudi banah!!!.....
 
Kiongozi Gani alie uliwa hapo uyahudini?? Nitonye pengine Mimi Sina taarifa. Wenzenu wakipiga wanapiga kweli sasa nyie mnapiga kiwanja Cha ndege kitupu?? Mimi mpaka hapo Bado sijaona kisasi Cha iran kwa muyahudi banah!!!.....
IDF wamepoteza zaidi ya askari 2000 na wameondoa majeshi yao Gaza. Iran jana kapiga intelligence center na Airbase na haziwezi kufanya kazi tena. Iran anatumia akili amuue kiongozi wa kazi gani?
 
Mimi ninaona wote wanaogopana. Iran Karusha drones na Ballistic missiles ambazo anajua zitatumai almost za tisa kufika Israel ambayo iko 700 miles away from Iran ikiwa ina maana alijua watajiandaa kuzidungua. Angekuwa ana lengo la kusababisha hasara kwa Israel angempiga shambulizi la ghafla. Sasa wewe unarusha kitu kinifikie masaa tisa, Israel na wapambe wake wakasema wanatrack kila drone na kila missile kabla ya kuingia kwenye anga ya Israel.
Upande wa pili ngoja tuone ila sidhani kama Israel naye atajibu kwa kurusha makombora au ndege kwenye anga ya Iran labda kama atapiga proxy wa Iran.
Ila la msingi naombea hawa watuw asiingie vitani maana dunia naona inaanza kuchanganyikiwa. Nikisoma comments za raia wa Marekani, wanaomba serikali yao iache Israel apambane na matatizo yake maana wanadai serikali iko busy na Israel wakati mambo yao ndani yanaharibika uchumi unayumba china anasonga kwa sababu ya kujifanya wanatia mkono kwenye mambo yasiyo wahusu.
Uzuri miaka hii ni kwamba Israel ana watu wake wenye nguvu (America & NATO) na Iran ana rafiki zake ambao mahasimu wakubwa sana wa America na NATO

Yaani hapo hakuna kuogopana,na kama ingekua kuna kuogopana Iran asingethubutu kufanya shambulio lolote Kwa adui yake

Lakini kuna upande ambao kama vile hawana cha kupoteza,then kuna upande ambao wanaanza kuingiwa na hofu ya nguvu/uwezo wa upande wa adui/hashimu wao kwamba wanahisi pengine ana kitu fulani hivi ambacho kama wakiingia kwenye battle field basi upo uwezekano wa kutoshana nguvu au damage ikawa kubwa

Ila muda ni mwalimu mzuri,tusubiri tuone nini kinakwenda kutokea
 
IDF wamepoteza zaidi ya askari 2000 na wameondoa majeshi yao Gaza. Iran jana kapiga intelligence center na Airbase na haziwezi kufanya kazi tena. Iran anatumia akili amuue kiongozi wa kazi gani?
Mbona majibu uliyonipa sio ya swali langu? Mie nimekuuliza ktk mashambulizi ya Jana maafisa wangapi wa ngazi za juu wa Izrael waliouliwa? Hivi unajua maana ya kulipa kisasi Cha mtu alieuliwa??
 
Ujasiri wa kurusha makombora hewa!! Wangetuma wanajeshi tuone huo ujasiri! Hatushabikii vita ila hawa waarabu na waajemi waliokuzwa ktk imani ya chuki ya kidini dhidi ya wanaowaita makafiri wanadekezwa sana na wayahudi na wazungu, dawa yao ingekuwa kuwajibu wanachokifanya kutofuata sheria za kivita ndiyo wataacha ujinga wa kubagua dini za wenzao na kuwaona wenye imani tofauti hawapaswi kuishi duniani au wakiishi wawe watumwa wao tu.
Umeandika kikristo Sana 😀😀
 
Russia na Iran wote hawana lolote ni joka la kabisa tu hao.

Marekani chini ya utawala wa huyu mzee ndio wanaharibu kabisa mambo kuogopa vita mashariki ya kati, waache Iran apigwe vinginevyo watapata kichwa kwa kufikiria kwamba wana uwezo wa kupigana na Israel kitu ambacho sio kweli kabisa.
 
Huenda ni wewe mleta uzi ndiye ambaye uko gizani na ulidhani Iran inatania.

Kama Israel ingedhani Iran inatania basi isingetangaza hadharani kuweka mifumo yake ya ulinzi katika utayari dhidi ya hali ya tahadhari. Matokeo yake, Israel isingeweza kukabiliana na mashambulizi kama ambavyo imefanya mpaka sasa na kwa ufanisi mkubwa.
 
Hata Iran amepeleka rasharasha tu amesema Isreal ikijibu tu basi atapeleka full dose wainywe vizuri.

Isreal hana ubavu wa kupigana uso kwa uso na Iran huwa anategemea support ya mabwawa zake USA na UK.
Hivi ujui Isreal ana nuclear mbona mnaleta ushambiki kwenye vita wanasema na Iran pia ana nuclear Tuombe Mungu hawa jamaa wakae mezani yaishe Nuclear haina mbabe
 
Israel ni strategic ally wa Marekani pale Mashariki ya Kati, hivyo Marekani kuingilia kati kuisaidia Israel ni win-win strategically. Inachokifanya Marekani kwa ajili ya Israel kinaisaidia Marekani pia katika nyanja za kiintelijensia, kijeshi, kiuchumi na geopolitically kwa ujumla.

Kwahiyo, sio kwamba Israel isingeweza kujihami dhidi ya Iran ama adui mwingine bila ya usaidizi wa Marekani, bali ni beneficial zaidi kwa Marekani kuisaidia Israel kama namna bora zaidi ya kulinda maslahi yake ya msingi pale Mashariki ya Kati.
Kifupi,nchi ya Israel ni military base ya marekani, uingereza na ufaransa kwa ajili ya kuidhibiti mashariki ya kati
 
Back
Top Bottom