Makombora mengi ya ballistic (zaidi ya 100) yamezuiwa na Israel yenyewe kupitia Arrow 2 na Arrow 3 defense systems
Arrow?
Kwa kifupi, mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel imeonesha uwezo mkubwa dhidi ya hizo ballistic missiles ambazo ndizo zilikuwa hatari zaidi kuliko cruise missiles na drones ukizingatia flight time pamoja na payload delivery. Ni mtu asiyefahamu kinachoendelea kuhusu haya masuala ndiye anaweza kusema Israel haijafanikiwa chochote dhidi ya hayo makombora.
Nadhani wewe huelewi kabisa. Defensive system ya Israel ni ya USA, EU na UK
Nchi hizo zimesema wazi leo kwamba zilikuwa msaada mkubwa licha ya kwamba system zao ndizo zinatumiwa
Hakuna silaha ya kisasa duniani ambayo Israel haijapewa na USA. Msaada wa USA kwa jeshi la Israel ni Bilioni 18 USD Takribani Trilioni 50 za Tanzania. Hivi unadhani hizo ni pesa za send off
Wiki inayokuja congress itapisha msaada zaidi wa silaha kwa Israel. Hivyo tambua kwamba Israel ipo mgongoni
Kama ni mfuatiliaji wa habari za dunia kwa leo ungeona jinsi Israel ilivyokuwa shocked!
1. Kwanza , haikujua drones za nchi yenye vikwazo miaka 20 zinaweza kufika
2. Hawakuwa na uhakika ingawa walijua kupitia proxy wa Iran kwamba silaha zao zina precision ya hali ya juu na siyo Katush za Hamas
3. Iran imeshambulia kutoka kona 4 ikiwa ni ujumbe kwamba wanaweza kupiga kutokea popote na wamefika miji yote mikubwa , Tel Aviv, Jerusalem , Haifa n.k.
Sasa kama unadhani wanaweza peke yao, ndege za UK ni za nini?
Kwanini Jordan na USA waliingilia kati ikiwemo kuzima GPS middle east?
Kwanini makamanda wa USA wapo Israel akiwemo kutoka central command
Lakini pia kumbuka hakuna nchi iliyowahi kupiga Israel tangu Scud la Saddam Hussein.
Tunachosema hapa si nani kashinda nani kashindwa, huo ni upuuzi
Tunachoonyesha ni kufuta ujinga wa ushabiki wa kipuuzi kwa watu wasiojua siasa za dunia hii.
Wengi waliaminishwa Israel ni super power! Israel siyo super power ni Proxy wa super power USA, UK and EU kama ilivyo Houth na Hezbollah kwa Iran. Wanafanyia kazi wakubwa wakiwa mgongoni , wenyewe hamna kitu
Bila msaada wa UK, USA, EU na kwa maelezo ya viongozi wao leo katika TV zao, hamna kitu
Ni lazima uingalie Israel kwa kijiografia, population kwanza kabla hujaanza kubisha.
Ndugu yangu tunazijua siasa za kimataifa!
Hivi umesoma declassified documents za vita ya 1967 ma 1973 Yom Kipur.
Kama hujasoma nenda Library halafu urudi maana nikikusoma unaongozwa na hisia kuliko ukweli.
Wengine hatujui ushabiki wa kipuuzi wa dini.