Iran yaishambulia Israel kwa makombora
ninachoshangaa, mashambulizi ya makombora karibia 300 lakini Israel haijaumia wala nini. biden amesema netanyahu asijibu, ila bibi kasema ndani ya masaa 48 anajibu. iran anasema yeye ameshapiga na hapigi tena, hahaha, ati anaogopa anajitetea kuwa ameshamaliza kazi hivyo hatarusha tena ila israel wakimpiga atatumia vichwa vya nukes. cha ajabu, israel ina makombora ya nukes kati ya 100 hadi 200, iran hana hata moja ila nukes aliyeenrich wanasema anaweza kutengeneza mabom 3 tu ya nukes. mtu anayetarajiwa kutengeneza bomb anamtishia mtu ambaye tayari anayo. tuombe tu Mungu vita iishe, though haipendezi kuisha wakati iran ambaye ni threat kwa kila mtu, amesimama. anatakiwa kudondoshwa ili dunia ikae salama.
iran hana cha kupoteza! israel ndio ana cha kupoteza!
 
mchina naye anapiga jaramba kumsaidia Iran! baada ya hapo Kiduku ataweka mguu kati! dunia inachafuka tunaanza tena Upya
mchina hawezi kuingia kwenye vita yeyote ndugu, hataki kabisa kuharibu uchumi wake kijinga. hata hivyo ninachojiuliza, makombora yote yale, kiasi gani israel imeathirika? hicho ndicho kipimo cha uwezo wa kivita wa haya mataifa mawili.
 
iran hana cha kupoteza! israel ndio ana cha kupoteza!
kweli urushe makombora karibia 200 au 300 na Israel hajaathirika chochote, wao wanaita ni total failure, tulitegemea moto uwe unawaka mtaani sasaidi israel, lakini hakuna lolote. ndicho ninachojiuliza.
 
Nyani Ngabu
Tulisema mapema katika huu uzi kwamba kinachosemwa ni vita ya Israel-Iran si kweli. Ni vita kati ya nchi za Magharibi na Iran. Hakuna tena siri, mataifa haya yalishiriki kuzuia drones na missile za Iran yakisema wazi ;
USA , UK, EU , Jordan na unknown Arab country ambayo ni Saudi Arabia.
UK imesema imetuma ndege zaidi za kijeshi

Mtu anayesema makombora hayakuwa na effect na kwamba yamezuiliwa na Israel si kweli, yamezuliwa na mataifa ya Magharibi. Rais wa Israel Isaac Herzog ametokea CNN akizishukuru nchi za Magharibi (allies).

Biden ameitisha kikao cha G7 ili kutengeneza ushirika wa kuishambulia Iran kwa jina la Israel, lakini ukweli unabaki pale pale IsraeL hamna kitu, bila msaada wa USA, EU na UK

By the way hili halikuwa shambulizi la vita. Wachambuzi wote wanasema ''iran ili telegraph' kila ilichokifanya ikiwa ni pamoja na kuwaeleza Marekani saa ngapi drone na missile zitaondoka. Biden alirudi Ikulu kwasababu hizo.
Kwahiyo nchi za Magharibi na Israel zilikuwa zina monitor kila hatua, hii haikuwa shambulio la vita

Tatizo linaloikabili Iran ni majirani maadui kama Saudi Arabia wanaotoa usaidizi kwa Israel na Marekani.
Shambulio lolote litatoa hapo kwasababu ni karibu na Israel ingawa Marekani wanaweza kushambulia kwa makombora kutoka popote. Challenge ni kwamba hawataki kujiingiza katika Vita kwasababu wataunganisha mataifa ya Uarabuni.

JokaKuu
 
Israel kasaidiwa na West! US na UK! walikuwa na ndege kibao angani! lasivyo leo mngeongea mengine leo! na kwa taarifa yako iran ana tudude tule kibaoooo yaan vingi kama sukari kwemye kilo
 
kweli urushe makombora karibia 200 au 300 na Israel hajaathirika chochote, wao wanaita ni total failure, tulitegemea moto uwe unawaka mtaani sasaidi israel, lakini hakuna lolote. ndicho ninachojiuliza.
 
Attachments

  • Screenshot_20240414-213137.jpg
    Screenshot_20240414-213137.jpg
    576.8 KB · Views: 4
hilo halina ushahidi wa moja kwa moja....ila
Israeli kuushambulia ubalozi wa Irani ni jambo liko wazi kwa dunia kujua kuwa Israeli imeishambulia Irani.
hivyo sheria za kimataifa zinairuhusu Irani kujibu mashambulizi.
Unahitaji ushahidi gani wa moja kwa moja? Wa Iran kuifadhili Hezbollah dhidi ya Israel?

Kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, Hezbollah ni non-state actor hivyo Iran inawajibika kwa matendo yanayofanywa na Hezbollah na makundi mengine inayoyafadhili.
 
Nyani Ngabu
Tulisema mapema katika huu uzi kwamba kinachosemwa ni vita ya Israel-Iran si kweli. Ni vita kati ya nchi za Magharibi na Iran. Hakuna tena siri, mataifa haya yalishiriki kuzuia drones na missile za Iran yakisema wazi ;
USA , UK, EU , Jordan na unknown Arab country ambayo ni Saudi Arabia.
UK imesema imetuma ndege zaidi za kijeshi

Mtu anayesema makombora hayakuwa na effect na kwamba yamezuiliwa na Israel si kweli, yamezuliwa na mataifa ya Magharibi. Rais wa Israel Isaac Herzog ametokea CNN akizishukuru nchi za Magharibi (allies).

Biden ameitisha kikao cha G7 ili kutengeneza ushirika wa kuishambulia Iran kwa jina la Israel, lakini ukweli unabaki pale pale IsraeL hamna kitu, bila msaada wa USA, EU na UK

By the way hili halikuwa shambulizi la vita. Wachambuzi wote wanasema ''iran ili telegraph' kila ilichokifanya ikiwa ni pamoja na kuwaeleza Marekani saa ngapi drone na missile zitaondoka. Biden alirudi Ikulu kwasababu hizo.
Kwahiyo nchi za Magharibi na Israel zilikuwa zina monitor kila hatua, hii haikuwa shambulio la vita

Tatizo linaloikabili Iran ni majirani maadui kama Saudi Arabia wanaotoa usaidizi kwa Israel na Marekani.
Shambulio lolote litatoa hapo kwasababu ni karibu na Israel ingawa Marekani wanaweza kushambulia kwa makombora kutoka popote. Challenge ni kwamba hawataki kujiingiza katika Vita kwasababu wataunganisha mataifa ya Uarabuni.

JokaKuu
Nadhani hata wao Waisrael wanajua kwamba wakiachwa wapigane tu wenyewe, huo ndo utakuwa mwisho wao.

Yaani nchi zote hizo zimeisaidia Israel hiyo jana halafu watu wanashangilia ‘uwezo’ wa Israel 😀.

Bure kabisa.
 
Leo katika TV Israel wanasema ''Iran ni tishio middle east' kwamba hata nchi za Ulaya hazipo salama, kwamba USA na masilahi yake wapo matatani. Yote hayo ni kuhakikisha wanaungwa mkono kwasababu wakiachwa wenyewe ni wepesi na wanapiga vizuri.

Kuna historia nzuri, mwaka 2006 katika vita ya Hezbollah Israel iliunda kamati kuchunguza kwanini vita ilichukua muda mrefu. Kamati ikaja na conclusion kwamba Israel ilishindwa vita, ilichokifanya ni kubomoa majengo.

Tangu mwaka 1988 Sadam Hussein alipopiga Israel kwa Scud nchi nyingine ni Iran kwa yale ya jana.

Pentagon wanasema, wametungua drone 2 wakitumia base zao kutoka 'unknow' ambayo ni Saudia, halafu wamezuia missile na drone 70 kutoka Iraq. Wakati huo huo UK inasema ilishirikia kutungua drone 7 kwa ndege za kivita na imetuma zaidi. Jordan nayo iumetungua. Mtu anasemaje Israel imezuia.

Leo ukiwasikiliza Israel wametishika kuliko wakati wowote katika miaka ya karibuni.
Bahati nzuri kwao ni kumiliki TV za Marekani na Europe na kupitia hapo wanafanya propaganda vizuri

Bila kubebwa na USA, UK na EU, hamna kitu !
 
Mtu anayesema makombora hayakuwa na effect na kwamba yamezuiliwa na Israel si kweli, yamezuliwa na mataifa ya Magharibi. Rais wa Israel Isaac Herzog ametokea CNN akizishukuru nchi za Magharibi (allies).
Makombora mengi ya ballistic (zaidi ya 100) yamezuiwa na Israel yenyewe kupitia Arrow 2 na Arrow 3 defense systems kwa sababu uelekeo wa msafara wa hayo makombora ni tofauti na drones ama cruise missiles.

Marekani, Uingereza na washirika wengine wa Israel wamezuia zaidi cruise missiles pamoja na drones ingawa Israel pia ilirusha ndege zake za kivita kwenda kufanya interceptions kadhaa nje ya mipaka yake.

Cruise missiles pamoja na drones zinapita usawa wa ndege vita ama chini yake. Ballistic missiles zinasafiri kwa kasi zaidi zikitumia projectile motion, na zinasafiri mpaka anga za juu ama nje kabisa ya atmosphere kabla ya kurejea ardhini kwenye target. Ndio maana idadi kubwa ya ballistic missiles kati ya 120 zilizofyatuliwa na Iran zilifanikiwa kuvuka interceptions za ndege na kukaribia anga la Israel.

Baadhi zilitunguliwa na defense systems za Israel zikiwa outer space kabla hata ya kugeuza uelekeo ili kurudi ardhini. Chache sana ndiyo zilikutana na mifumo ya ulinzi wa anga ya Marekani huko baharini. Huku chache pia zikipenya bila kuleta madhara.

Kwa kifupi, mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel imeonesha uwezo mkubwa dhidi ya hizo ballistic missiles ambazo ndizo zilikuwa hatari zaidi kuliko cruise missiles na drones ukizingatia flight time pamoja na payload delivery. Ni mtu asiyefahamu kinachoendelea kuhusu haya masuala ndiye anaweza kusema Israel haijafanikiwa chochote dhidi ya hayo makombora.
 
Ila pia USA imesaidia na Jordan ku intercept mashambulizi mengine.
Kama hayo mataifa mengine yasingehusika sidhani kama Israel angeweza ku intercept mashambulizi yote hayo peke yake.
Pia Iran amekiri kutumia medium range missiles ambazo ni unguided.
Sijui angetumia guided zenye ujazo ingekuaje.
 
Makombora mengi ya ballistic (zaidi ya 100) yamezuiwa na Israel yenyewe kupitia Arrow 2 na Arrow 3 defense systems
Arrow?
Kwa kifupi, mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel imeonesha uwezo mkubwa dhidi ya hizo ballistic missiles ambazo ndizo zilikuwa hatari zaidi kuliko cruise missiles na drones ukizingatia flight time pamoja na payload delivery. Ni mtu asiyefahamu kinachoendelea kuhusu haya masuala ndiye anaweza kusema Israel haijafanikiwa chochote dhidi ya hayo makombora.
Nadhani wewe huelewi kabisa. Defensive system ya Israel ni ya USA, EU na UK
Nchi hizo zimesema wazi leo kwamba zilikuwa msaada mkubwa licha ya kwamba system zao ndizo zinatumiwa

Hakuna silaha ya kisasa duniani ambayo Israel haijapewa na USA. Msaada wa USA kwa jeshi la Israel ni Bilioni 18 USD Takribani Trilioni 50 za Tanzania. Hivi unadhani hizo ni pesa za send off

Wiki inayokuja congress itapisha msaada zaidi wa silaha kwa Israel. Hivyo tambua kwamba Israel ipo mgongoni

Kama ni mfuatiliaji wa habari za dunia kwa leo ungeona jinsi Israel ilivyokuwa shocked!

1. Kwanza , haikujua drones za nchi yenye vikwazo miaka 20 zinaweza kufika
2. Hawakuwa na uhakika ingawa walijua kupitia proxy wa Iran kwamba silaha zao zina precision ya hali ya juu na siyo Katush za Hamas
3. Iran imeshambulia kutoka kona 4 ikiwa ni ujumbe kwamba wanaweza kupiga kutokea popote na wamefika miji yote mikubwa , Tel Aviv, Jerusalem , Haifa n.k.

Sasa kama unadhani wanaweza peke yao, ndege za UK ni za nini?
Kwanini Jordan na USA waliingilia kati ikiwemo kuzima GPS middle east?
Kwanini makamanda wa USA wapo Israel akiwemo kutoka central command

Lakini pia kumbuka hakuna nchi iliyowahi kupiga Israel tangu Scud la Saddam Hussein.
Tunachosema hapa si nani kashinda nani kashindwa, huo ni upuuzi

Tunachoonyesha ni kufuta ujinga wa ushabiki wa kipuuzi kwa watu wasiojua siasa za dunia hii.
Wengi waliaminishwa Israel ni super power! Israel siyo super power ni Proxy wa super power USA, UK and EU kama ilivyo Houth na Hezbollah kwa Iran. Wanafanyia kazi wakubwa wakiwa mgongoni , wenyewe hamna kitu

Bila msaada wa UK, USA, EU na kwa maelezo ya viongozi wao leo katika TV zao, hamna kitu

Ni lazima uingalie Israel kwa kijiografia, population kwanza kabla hujaanza kubisha.

Ndugu yangu tunazijua siasa za kimataifa!
Hivi umesoma declassified documents za vita ya 1967 ma 1973 Yom Kipur.

Kama hujasoma nenda Library halafu urudi maana nikikusoma unaongozwa na hisia kuliko ukweli.

Wengine hatujui ushabiki wa kipuuzi wa dini.
 
Tulia dogo kamikaze drones zaid ya 100 zipo hewani saahizi zinaelekea Tel aviv subiri majibu. Hizo hazitunguliwi na kima yeyote .saahizi ndege ya Netanyahu imeondoka Jerusalem
Habari zako za kipuuuuzi unajitungia tungia
 
Back
Top Bottom