Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Hii kitu ni kama picha la kihindi hivi
1. Marekani inaua watu 2, Jenerali Qasseim na mwenzake.
2. Iran inakasirika na kuzipiga kambi za marekani, makombora hayauwi mtu na mengne hayalipuki kabisa.
3. Iran wanamzika Jenerali qasseim, watu 56 wanakufa kwa kukanyagana hapo msibani.
4. Iran ikiwa tayari kujibu shambulio lolote la marekani, mara wanaona ndege inakatiza usawa wa kambi zao za jeshi, wanaitungua na kuua watu 176 wakiwemo raia wa irani 82.
5. Iran inaondoa haraka mabaki eneo la tukio, kabla ya uchunguzi kufanyika.
6. Baada ya siku 3 za kukataa kuhusika kulipua ndege hiyo ya abiria, Iran inakiri kuipiga ndege kimakosa,na kuahidi kuadhibu wahusika.
7. Jumla ya raia wa iran waliopoteza maisha kwenye kadhia hii hadi sasa ni 140 (2+56+82).
Sent using Jamii Forums mobile app
Iran ni level za Malawi kwa uwezo walioonyesha kwenye hili sakata, hata bongo tumewashinda.