Iran yapandisha Bendera Nyekundu katika msikiti wa Jamkarān kuashiria vita inakuja

Iran yapandisha Bendera Nyekundu katika msikiti wa Jamkarān kuashiria vita inakuja

Eti kauawa shahidi
Ujinga hautawaisha
Katika hali isiyo ya kawaida na isiyotarajiwa Iran imepandisha bendera nyekundu ikiashiria ishara ya vita kuu.

Kikosi cha mapinduzi ya kiislam kimeapa kulipa kisasi na kutoa jibu kali kwa Marekani. Tujiandae kushuhudia moto ukiwaka.

===
IRGC yaahidi hatua kali ya kulipiza kisasi baada ya kuuawa shahidi Soleimani

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na mashahidi wengine katika jinai ya Marekani Ijumaa asubuhi mjini Baghdad na kusisitiza kuhusu kulipiza kisasi kufuatia jinai hiyo.

Katika taarifa siku ya Ijumaa, IRGC imelaani hujuma ya angani ya vikosi vamizi na vya kigaidi vya Marekani ambayo imelenga gari lililokuwa limembeba Meja Jenerali Soleimani, wenzake na makamanda wa Harakati ya Al Hashd al Shaabi ya Iraq akiwemo mpigana jihadi mkubwa, Abu Mahdi al Muhandes ambaye alikuwa akitekeleza mpango wa kukabiliana na njama mpya ya Marekani ya kuhuisha ISIS na makundi mengine ya magaidi wakufurishaji sambamba na kuvuruga tena usalama wa Iraq.BTaarifa hiyo imesema waliouawa shahidi wamepata fahari kubwa.

IRGC imesisitiza kuhusu kuendeleza njia ya mashahidi na kuongeza kuwa, Meja Jenerali Suleimani hakuwa tu shakhsia bali alikuwa ni fikra kamili na kuanzia sasa maadui wataweza kushuhudia upeo mkubwa zaidi wa fikra hizo katika maeneo ambayo wameeneza satwa yao kinyume cha sheria duniani.

Taarifa hiyo aidha imesisitiza kuwa Meja Jenerali Suleimani na wengine ambao wamelelewa katika fikra za Utawala wa Faqihi na Mapambano ya Kiislamu, wamefungua ukurasa mpya katika mapambano na muqawama dhidi ya Wazayuni na katika kukabiliana na magaidi pamoja na Wamarekani wavamizi katika eneo.

Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema jana Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani baba lao,ikiamua kuiteketeza dunia ni dakika sembuse iran kama kamdudu fulan,ingekuwa Urus au China angalau marekani wangehaha,waulize Iroshma na Agaski kilichowakuta

Israeli tu ina uwezo wa kuwasimamisha waarabu wote Mashariki ya kati na kuwalagaza kwa kila upande,Iran yenyewe inajua kwa marekani vita ya anga na majini hawatawaweza,wana technolojia ambazo hazijawahi kuonekana mahali popote duniani

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni Hiroshima na Nagasaki kama sikosei mkuu, I stand to be corrected


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wadau:
Hivi ktk historia ya Marekani (USA), ni vita gani aliyo pigana nje ya nchi yake na akashinda?
Vita sio Boxing kusema unatafuta mshindi ktk ulingo. Kitendo cha Jazav zharif kutumia Twitter account ni dalili ya kwanza ya kushindwa vita. Wewe unachukulia vita sawa na masumbwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kafa mmoja wanataka waongezeke watu watakaokufa kwanini kutangaza vita na watakaoathirika ni wasio na hatia IRAN ijitafakari kama imepandisha bendera nyekundu ni kuzidisha hofu kwa wananchi wake na si ajabu saizi wakimbizi wameshaanza huko
 
Na ulaaniwe Yani unaamin marekan inauwezo wa kuiteketeza dunia! innalillah wa innaillah rajn
Marekani baba lao,ikiamua kuiteketeza dunia ni dakika sembuse iran kama kamdudu fulan,ingekuwa Urus au China angalau marekani wangehaha,waulize Iroshma na Agaski kilichowakuta

Israeli tu ina uwezo wa kuwasimamisha waarabu wote Mashariki ya kati na kuwalagaza kwa kila upande,Iran yenyewe inajua kwa marekani vita ya anga na majini hawatawaweza,wana technolojia ambazo hazijawahi kuonekana mahali popote duniani

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee nchi yoyote inayopigana vita na USA basi haitabaki kama ilivyokuwa, chukulia mifano tu ya Iraq, Afghanistan, ambazo zilivamiwa na USA zilivyo sasa hivi.

USA yeye kinachomgharimu ni hela na wanajeshi wachache, ila hao wanaovamiwa nchi zao zinaharibiwa totally.
So Iran ange swallow pride yake tu na kubaki zake salama
Kuendekeza pride kwa gharama ya kuvuruga nchi yako na mauaji ya maelfu ya raia ni ujinga.


Sent using Jamii Forums mobile app
Watoto wadogo hawaelewi..wanachekelea tu kama wajinga.
Watu tulikuwa tunasoma Libya..tukashindwa kumaliza Masomo kisa ile issue ya Gadafi..

Zaidi ya mtu kwenda kujitoa Mhanga Marekani..impact yake ni ndogo sana ukilinganisha na uharibifu na vifo vya watu wengi kwenye Nchi inayopigana na Marekani.

Upo sahihi kabisa Mkuu..kuna watu humu wanashabikia ila wamefumba macho saana.

Nitakapoona Kombora limetoka Tehran mpaka Washington DC ndio nitasema yametima la sivyo.

Wanachoaanda wana siasa wa Iran ni njaa na majanga makuu kwa Wananchi wao..Hakuna cha Russia wala China hao wote wanataka Resources kwa ajili ya wananchi wao.
 
Watoto wadogo hawaelewi..wanachekelea tu kama wajinga.
Watu tulikuwa tunasoma Libya..tukashindwa kumaliza Masomo kisa ile issue ya Gadafi..

Zaidi ya mtu kwenda kujitoa Mhanga Marekani..impact yake ni ndogo sana ukilinganisha na uharibifu na vifo vya watu wengi kwenye Nchi inayopigana na Marekani.

Upo sahihi kabisa Mkuu..kuna watu humu wanashabikia ila wamefumba macho saana.

Nitakapoona Kombora limetoka Tehran mpaka Washington DC ndio nitasema yametima la sivyo.

Wanachoaanda wana siasa wa Iran ni njaa na majanga makuu kwa Wananchi wao..Hakuna cha Russia wala China hao wote wanataka Resources kwa ajili ya wananchi wao.
Iran anaweza akapotezea Trump akatoka madarakani, inaweza ikawa mwaka huu au miaka 4 ijayo, akaingia Rais mwingine ambaye atakuwa sio hawkish kama Trump, maisha yakaendelea
Kuliko ku risk kuharibiwa na maelfu ya wananchi wake kuuawa kisa jenerali mmoja
 
Marekani wamevunja sheria za kimataifa na vile vile sheria ya marekani iliyoandikwa kama Executive Order 11905 iliyotolewa February 18, 1976, na Rais Gerald R. Ford ikipiga marufuku staasisi za serikali ya Marekani kufanya mauajiya viongozi wa kiserikali wa nchi nyingine kwa sababu za kisiasa. Amri hiyo ilifanyiwa marekebisho na Rais Jimmy Carter mwaka 1978 kama Executive Order 12036.

Kwa vile Kassim Seleman alikuwa ni kiongozi wa kiserikali wa Iran siyo stateless terrrorist kama Osama bin laden alivyokuwa, mauaji hayo yamevunja executive order hizo. Ni afadhali wangemwua kimya kimya halafu wasitanganze (covert operation). Hili la sasa linatoa mwanya kwa nchi nyingine pia kufanya assasination za viongozi wa nchi wasizopenda kiholelela.
 
Kwan IRAN Anashida Na Mtu Sema Kuna Wapuuzi Wanamuingilia Ingilia Tuu
Iran ingetulia tu yaishe, itapoteza zaidi ya mara dufu kuingia vitani na USA, USA mwenyewe ana washirika kibao..Ana Saudia, UAE, Israel, NATO, bado mwenyewe ana nguvu kubwa ya kijeshi..hata kama Iran atafanikiwa kumuumiza Marekani basi yeye nchi yake itageuzwa vifusi zaidi kuliko hata Syria

Ishu ni kuishi maisha yako tu, mwenye nguvu mpishe, ishi kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili Halitapita Bila Yamajibu Ila Majibu Yake Tu Yanaweza Yakachelewa.............

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom