Makao makuu ya intelligence ya Israel (Mossad) Leo asubuhi.
Wachambuzi wanaeleza kuwa Iran ilitumia teknolojia ya juu kuudanganya mfumo wa kiulinzi wa Israel ambao ulirusha makombora 10 bila mafanikio.
Tuombe amani Hali ni tete.
View attachment 3372854
Allah huichukua akili ya mtu na yule mtu akafanya mambo ya ovyo.
Majuto mjukuu pale Allah anapomrejeshea akili zake.
Wayahudi tunaambiwa ni wataalamu sana sikwambii Wamarekani.
"They did not bargain for this."
Hawa ndiyo na mabingwa wa "theories" mathalan "simulation."
Kabla jambo halijafanywa wanatengeneza mfano wake na kupitia "options" zitakazotumika.
Israel ikishambulia Iran nini Iran itafanya?
Hapo ndiyo "simulation" sasa inatumika.
Vipi hawakuona hili la miji yao pia itapigwa ifanane na Ghaza?
Allah aliwanyang'anya akili zao.
Kingine linanishangaza sana ni kauli kutoka Israel na Marekani kiasi najiuliza hivi hivyo vyuo vya Marekani hawasomeshi historia ya Mashia?
Hawajui ile ari ya kisasi na kupigana ndani ya Mashia?
Mashia wanakwenda uwanja wa vita kufa.
Wasikilize Wayahudi waliopigana na Hizbullah Lebanon hadi wakarudisha majeshi yao nyuma na kuiachia ardhi waliyoteka.
Hawajajifunza kwa Hizbullah?
Wamesahau vita vya siku 34 mwaka wa 2006 kati ya Hizbullah na Israel?
Hivi hawajui Iran imepigana miaka 8 na Saddam Hussein tena vita vya "attrition?"
Kwa mara ya kwanza Wayahudi leo wanajua vifusi ni kitu gani na nyumba ni nini.
9/11 iliwafunza Waamerika maana ya kushambuliwa.
Hili lilikuwa somo hawakupata kusomeshwa.
Nimefika "Ground Zero" New York zilipokuwa Twin Towers.
Nimezungumza na watu waliokuwapo mjini siku ile.
Kujifariji walikunywa pombe usiku kucha ndani ya bar zao.
Kila Mmarekani anaepita hapo anapita kichwa chini.
Hili ni kovu katika saikolojia ya Wamarekani.
Kufungwa kwa Strait of Hormuz hili ni pigo kubwa na linafahamika halihitaji maelezo.