Wacha kuropoka,Iran ametumia bajeti ndogo ya vita na kuiipa hasara Israel kuliko unavyodhani.
Israel imepata hasara kubwa kuliko udhaniavyo,Kuna vituo vya uwekezaji vimelipuliwa,bandari Haifa imelipuliwa,kituo Cha usafishaji mafuta Haifa kimelipuliwa,kambi Tano za jeshi zimelipuliwa.
Kama ulikua hujui utumiaji makombora ni bora kuliko ndege kwasababu ni costless na damage ni ndogo kwa mtumiaji.
Ndege gharama kwa mafuta pia gharama ya maisha inaweza kuhusika ya marubani.
Sasa sijui nani ni mjanja kati ya Iran na Israel!?
Iran hajatumia bajeti ndogo, katumia bajeti kubwa sana tu, ku launch makombora karibu 600 ni gharama kubwa sana.
BUT Israel katumia gharama zaidi ya Iran kufanya yale mashambulizi.
Kuhusu damage, mkuu wote wamepata damage kubwa, haya uliyosema pia yametokea Iran pia kwa kiwango kikubwa. Kwa lugha nzuri, hii Vita wote wamepata hasara, Israel miji yake imeshambuliwa, pia Iran miji yake imeshambuliwa+makamanda wa juu wa jeshi
Utumiaji wa makombora ni bora kuliko ndege, huu ni mjadala mzuri na mrefu. Kwa gharama makombora yapo chini kidogo ya ndege. Lakini Kuna advantage na disadvantage kwa aina zote mbili
Ukiweza kupata air superiority, basi ndege ni option nzuri kuliko kutuma missiles, sababu ndege zinakupa faida ya kuwa versatile wakati wa kufanya mashambulizi, wakati missiles zenyewe zinakosa versatility sababu zitadili na fixed target
Ukikosa air superiority,basi option nzuri ni hiyo kutumia missiles, hata kama 80% ya missiles ikiwa intercepted basi 20% ya yatayopenya yataleta madhara makubwa.
Sio kwamba Iran hataki kutumia ndege, bali ni ngumu kutoa ndege Iran kwenda kushambulia Israel sababu ya kutopata anga. Ukikosa umiliki wa anga ndege zitakua zinashushwa tu
Israel anatumia ndege sababu imekua rahisi kwake kupata anga kwenda Iran kushambulia. Pia Kuna walio ndani ya Iran walikua wakifanya kazi kuhakikisha ndege zinakua free kuingia na kutoka. Iran akipata hii advantage ndani ya Israel basi utaona ndege zake pale ndani ya Tel Aviv
Anayeweza kuingiza ndege kwako kufanya mashambulizi hana sababu ya kutumia missiles. Missiles ni option endapo utakosa kuingiza ndege kwa adui yako