Wapigane,tena wapigane sana,tushangilie,tena tushangilie kwa sauti kubwa na kuongeza sauti,maana dunia haina watu tena,vimebaki viatu,tena viatu vya kuvali chooni,nasema chooni na siyo msalani.
Wapigane,haja ya mataifa makubwa ni kuangamiza dunia,maandiko ya vitabu yanatimia.
Atakaedhani kwamba ipo siku shetani atatubu dhambi zake,basi ameingia choo cha kike wakati yeye ni mwanaume.nasema tena ameingia choo cha jeshi ihali yeye ni raia.
Dunia haihitaji amani tena kwani thamani ya amani haionekani,wapigane.