TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

eTI SHOSTI zomba hujalala tu. Aa bwana weh sometime kuwa binadamu kidogo.
 
Laana hii naitoa na iwe juu yao...afu nahisi hizi siku 2 ntapigwa ban..
 
Ilikuwa hivi: CHADEMA walifika Nyololo kufungua ofisi za chama. Wakakuta polisi wamefika tayari kwa ajili ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kwa kisingizio cha sensa. Kukatokea ubishani kiasi huku polisi wakiwa tayari wamejipanga kufyatua mabomu yao. Lakini baada ya kubishana kidogo watu wa CHADEMA wakihoji uhalali wa katazo hilo, ilionekana polisi wameruhusu hao wanachama wafungue tawi bila kufanya mkutano. Kweli ufunguzi ukafanyika na baada ya hapo CHADEMA waliondoka kwenda kufungua tawi la pili ambalo lipo kama kilomita moja hivi kutoka kwenye tawi la kwanza. Walipokuwa wakienda kwenye tawi hilo la pili polisi nao walikuwa wakifuatilia nyuma. Baada ya kufika ofisi ya pili CHADEMA wakaanza utaratibu wa kufungua ofisi bila fujo wala chochote. Cha ajabu bin ghafla polisi waakamrisha watu kutawanyika. Badala ya kutawanyika CHADEMA wakaamua kukaa chini kwa kuwa hawakuwa na sababu ya kukimbia au kutawanyika. Mara polisi wakanyanyua tambara jekundi, mara mabomu. Waandishi kama kawaida ya kazi yao wanatakiwa kuchukua habari wakawa wanaendelea kuchukua habari na hatimaye polisi wakamwua Daud Mwangosi.
Mimi binafsi katika maisha yangu yote sikuwahi kufikiri mtu bila sababu ya msingi awe raia au askari anaweza kumwua binadamu mwenzake kimzahamzaha kama hivi ilivyotokea. Jamani utu uko wapi sasa? Hivi kwa maslahi ya mtu tu haya yanaweza tokea Tanzania kweli? Sijui tukimbilie wapi? HIVI kama wangeacha CHADEMA iendelee na shughuli yake pangetokea nini? Hakuna baya lolote lingetokea. Hivi mimi leo hii naweza sema Tanzania kuna demokrasia na amani kweli? Haya sasa watoto wa Mwangosi waende wapi? Hivi hayo madaraka ya kuondoa uhai wa watu mmepata wapi? Kutoka moyoni, sikufukiri maisha ya binadamu yanaweza kuondolewa na mwanadamu mwingine kimzahamzaha hivi. TANZANIA
 
no nooooo haiwezekani chadema ifutwe hata ccm haitakuwa salama tutaingia kokote kudai haki haiwezekani watajuta
 
RIP Daudi Mwangosi.

Ninachoona ni jinsi gani kifo chako kitakavyochochea mapambano dhidi ya utumiaji wa mabavu bila sababu za msingi.

RIP Kamanda. damu yako na wengine waliotangulia haitapotea bure! Time. Time will tell.
 
jamani hivi chadema ndiyo inayosema polisi waue mbona kuna watu wana udongo mwingi saana vichwani mwao mnaandika chadema ndio imesababisha kwa vipi?
 
Na yawezekana kabisa lengo la kumshambulia mpaka kumuua ni kuharibu ushahidi wa picha alizokuwa amekwisha wapiga! Wasijue kuna mwingine anawapiga picha.

Kama waziri wa mambo ya ndani anapenda mustakabali wake wa kisiasa, AACHIE NGAZI MARA MOJA, Na kama RAIS anawapenda raia wake: AWAFUTE KAZI (kama hawatajuhuzuru wenyewe) wafuatao:
1. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI,
2. IGP,
3. MWENYEKITI WA ULINZI NA USALAMA MKOA WA IRINGA,
5. RPC IRINGA.

Na kama Rais hatofanya hivyo basi na yeye apelekwe the hague! Haya si mambo ya kuvumilia hata kidogo! Vinginevyo tuseme hii ni nchi ya kidictecta, haina utawala bora wala haiheshimu haki za binadamu!

Nzitunga u ve a valid point,hilo halijawahi kutokea siku za karibu watu kuwajibishwa kwa makosa kama haya either kwa kuwiwa na utashi wao wenyewe achilia mbali wanaohusika kuwachukulia hatua.Hili likitokea litaingia kwenye kitabu cha kumbukumbu.Wanahabari/media muhimili wa Nne huu ni wakati wenu unganisheni nguvu katika hili
 
Watanzania tumepewa akili, uwezo na maarifa kwanini polisi watunyanyase na kuwaua watu wetu?
I am impressed to say now we are to take action, action to free from this tyrant regime, action to reshuffle all the security system of this country, action to help our suffering brothers and sisters!

stand up!
 
Mauaji ya raia wasio na hatia ni ushahidi tosha ya kuwa ccm imepoteza dira, imekiuka miiko iliyojiwekea yenyewe.
ccm imegeuka saratani, haina tiba. Lililobaki ni kuiondoa. Kama ambavyo chembechembe hai (cells) zikishaharibiwa na ugonjwa wa saratani au kansa hazitibiki, dawa pekee iliyobaki ni kukata uozo huo. Mtu akiwa na kansa sehemu iliyoathirika hukatwa, ili kuokoa maisha yake. Imefika mahali ili kuiokoa Tanzania ambayo ni kubwa zaidi ya itikadi za ccm, kuna haja ya kuiondoa madarakani ccm.

Nakumbuka enzi za TANU na hata miaka ya mwanzo ya CCM, enzi za Mwalimu kulikuwa na imani za chama. Zilikuwa kumi.
Ya kwanza ilisema 'Binadamu wote ni Sawa'.
Ya pili ilisema 'Kila mtu anastahili heshima'.
Ya tatu ilisema 'Rushwa ni adui wa haki'.
Ya nne ilisema ' Cheo ni dhamana' na kadhalika mpaka kumi.

Sasa unapoona vyombo vya dola inayoongozwa na chama hicho hicho vimejisahau na dola imesahau imani zake hususan za usawa wa binadamu, heshima kwa watu wote, kukataa rushwa na ufisadi, na kutambua ya kuwa vyeo vyao ni dhamana tu ya kuongoza na si vinginevyo, tujue mwisho wa ccm umefika.

Hatuna budi kuikata hii sehemu katika jamii yetu ambayo imeathirika na saratani, ili Tanzania kama nchi iendelee kuishi.

R.I.P. Mwangosi.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Dear Tanzanians, your vote in 2015 has a power to bring a new era of human justice,accountability etc
 
HUU NDIO MUDA Wa KUTOKURUDI NYUMA. HAKUNA NCHI ILIYOTAWALIWA KWA MAUAJI YA RAIA WASIO NA HATIA, IKAWA NI NCHI YA AMANI! TANZANIA SIO NCHI YA AMANI TENA.

CCM NI THE HAGUE, WAKAJIBU MASHITAKA.
 
Back
Top Bottom