TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Plz wekeni link ya hiyo thread.

Thread ya Mzee Mwanakijiji ya kushauri CDM kuandaa maandamano dhidi ya polisi ni Muhimu sana

Katiba mpya iruhusu rais ashitakiwe baada ya kumaliza muda wake sababu yeye ndo amiri jeshi mkuu na ndiye anayewateua hawa watu wake

R.I.P bro. Mwangosi

sio lazima katiba mpya hata sasa wananchi tunaweza kuchukua hatua.
 
Hiki chama cha wauaji kifutwe tu. Kila wanapokwenda wanauwa.


zomba wakati mwingine ni vema ukakaa kimya! Wengine tunasikitishwa na hayo yanayofanywa na vyombo vya dola! Hebu zungumzia mauaji ya mwandishi wa habari Iringa. Mtu mwenye akili timamu utasema kweli kuwa ameuawa na chadema? Wakati mwingine tuache ushabiki wa kisiasa na tukemee maovu dhidi ya raia.
 
Daud%2BMwangosi%2B%2Bkulia%2Benzi%2Bza%2B%2Buhai%2Bwake.JPG

Labda macho yangu yana tatizo embu angalia suruali aliyovaa Daudi dakika 20 kabla ya tukio na hiyo aliowekewa mtutu (Daudi ni huyo mkono wa kulia anachukua picha kwa Video camara na hapo kiunoni amevaa sijui kitu gani)
 
huyo aliekuwa anaepigwa kikatili sio mwandishi.coz mwandishi dakika 20 kabla ya kuuawa alikuwa kavaa jeans ya blue.huyu jamaa anaepigwa kikatili kavaa kadet ya kaki!

Daud%2BMwangosi%2B%2Bkulia%2Benzi%2Bza%2B%2Buhai%2Bwake.JPG


Una matatizo ya kutambua rangi embu fananisha vizuri hizi picha mdau ngozimbili

attachment.php
 
Last edited by a moderator:
The Problem is Polisi walishafanya na wameendelea kufanya uonevu huu sehemu mbali mbali( vyuoni, mikutano ya siasa, maandamano ya wanaharakati mbalimbali)...tumekuwa tukisema na kufarijiana, how abt we suggest the way forward wakuu( IRRESPECTIVE of political, gender, religious differences)?? If so;

- Nashauri Tusikubali kuundwa kwa tume na Polisi
kujichunguza wao kama tulivyozoea .
-Askari / Kikosi kilichofanya hivyo na wawajibishwe.
- W/mambo ya ndani, Ulinzi , RPC +/- IGPa role to play in
this saga.
-Waandishi wa Habari na wamiliki ikawe mwanzo wa
kutambua chachu ya kazi yenu mkitambua wananchi
wanawategemea ninyi, na hasa wale wajao baada yenu
katika taaluma hiyo.

Tutoe maoni nini kifanyike, na tusiishie kuguswa, kusema na kusahau..Let His death not be in Vain..
Rest in Peace David Mwangosi.
 
i am shocked..namfahamu Daudi Mwangosi Mwakipageme,nilisoma naye Tosamaganga.
How long shall they kill our prophets,While we stand aside and look?
 
mpaka watafikia hatua ya kutumezesha mabomu.......jaman polisi hv hamtafakari hata mnapoagzwa na hao magamba? natabiri kama hali itakuwa hivi Maogon chaweza kunuka:baby::yawn:
 
Tatizo hapa sasa hivi ni kwamba hatuna serikali. Hatuna Rais, hatuna uongozi.
Mawaziri ni wezi
Raisi ni hivyo hivyo na safari za kwenye misiba
Usalama ni kulinda Rais na mkewe na watoto wake,
Askari hawana uongozi

Haya yameenedelea kwa miaka mingi na sasa hivi hakuna askari anayeona ubaya wa kuuwa.

Haiingii akilini askari kwenda kutuliza ghasia akiwa na risasi za moto. Si mara ya kwanza, ya pili na hata tatu! Ukiangalia mazingira ni watu wanaoandamana bila siraha.

Sababu eti mikutano imezuiliwa wakati huo mikutano ya chaguzi za CCM inaendelea na wanavurugana.
 
Polisi wanachofanya ni cha kusikitisha, Morogoro wameuwa na sasa Iringa. Lakini nina wasiwasi na waziri wa sasa wa Mambo ya ndani Emanuel Mchimbi. Tangu ameingia madarakani kasi ya polisi kuzuia mikutano ya chadema imezidi. Kuna nini hapa? Je sio uyu kada wa ccm (Mchimbi) anatumia vibaya jeshi la polisi kwa manufaa ya CCM? Sawa tunaweza kumlaumu IGP Saidi Mwema, lakini kwani yeye anapata amri kutoka wapi? Hivi jeshi la polisi si liko chini ya wizara ya mambo ya ndani? Je wanaweza kuzuia mikutano ya vyama vya kisiasa bila amri kutoka mahali fulani?Kwani chain of command ya polisi inaanzia wapi? (wanaojua wanisaidie). Kwangu mimi polisi ni kama robot ni wa kutii amri kutoka juu.Hili tukio lituhamshe tuangalia jeshi la polisi kwa mapana yake, tukiwalalamikia polisi peke yao tunapotea.
 
Daudi my brother kwa nini umondoka mpema kiasi hko ndugu yangu umetangulia nikiwa mbali hakika naja kukupumzisha Muumba hakinipa nafasi daudi nakukumbuka kwa mengi mpaganaji mwezangu hasa hoja yako nzuri pale hall E ruaha university iringa siku ya law day wewe ni kichwa mpigania haki umetangulia kiume daudi mtoto wa mzee mwangosi
 
Hiki chama cha wauaji kifutwe tu. Kila wanapokwenda wanauwa.

Hizi ni mbinu zenu chama cha magamba kutaka kusingizia kuwa Chadema ndio wanaoanzisha fujo na mauaji lakini mkumbuke kuwa matendo ya askari wenu yanachukuliwa picha na huo utakuwa ushahidi kamili kujua nani muhusika wa vitendo hivi vya kihuni!! Kumbukeni magamba, dunia haitawasamehe kwa ujinga wenu huu na viongozi wenu wajue vitendo hivi ni njia moja ya wao kwenda THE HAGUE!! Your leaders are killing by proxy!!
 
japo tunaweza kujifariji kuwa tuna amani, lakini tumefika pabaya kabisa. sijui nani atatuamulia kila mtu akionyesha malimbikizo ya chuki zake kwa serikali.
 
...Mie wala sitashangaa kwa CHADEMA kubambikiwa kesi za uongo sehemu mbali mbali nchini zinazohusiana na mauaji kisha Tume ya uchaguzi ya magamba itamke CHADEMA kinaonekana ni chama ambacho kinataka kuanzisha umwagaji damu nchini hivyo kimefutwa rasmi na hakiruhusiwi tena kujishughulisha na mambo ya siasa nchini....naamini kabisa hili likitokea sehemu nyingi nchini zitalipuka kwa ghasia kubwa sana na mauaji mengi yanaweza kutokea.

Mkuu hiyo ni kazi ya msajili wa vyama vya siasa nchini na wala si tume ya taifa ya uchaguzi.Msajili wa vyama vya siasa nae ni mteule wa raisi.Wote hawa ni watu ambao mtu huhitaji kuwa na degree kujua wako chama gani na wanafanya kazi zao kwa maslahi ya nani.

Katiba mpya ije ifute kabisa watu kama msajili wa vyama vya siasa kuteuliwa na raisi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
...Nina hasira sana kufuatia mauaji ya kinyama ya Mwangosi...Nilipitiwa Mkuu...Ahsante sana.

Mkuu hiyo ni kazi ya msajili wa vyama vya siasa nchini na wala si tume ya taifa ya uchaguzi.Msajili wa vyama vya siasa nae ni mteule wa raisi.Wote hawa ni watu ambao mtu huhitaji kuwa na degree kujua wako chama gani na wanafanya kazi zao kwa maslahi ya nani.

Katiba mpya ije ifute kabisa watu kama msajili wa vyama vya siasa kuteuliwa na raisi.
 
hao polisi wanekana kwa sura, ni rahisi kabisa kuwakamata,...tunaomba vyombo vya dola viwakamate wote, na hapo hamna cha nolle wala nini wanyongwe kabisa hawa.
 
huyo aliekuwa anaepigwa kikatili sio mwandishi.coz mwandishi dakika 20 kabla ya kuuawa alikuwa kavaa jeans ya blue.huyu jamaa anaepigwa kikatili kavaa kadet ya kaki!

Anayepigwa ndio marehemu, usichakachue habari.Nenda Monchwali kamvalishe hizo nguo unazosema ili kuficha ushaidi.
 
Back
Top Bottom