Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumatatu, Nkuna alidai kushambuliwa na watu wasiojulikana. "Nimeshambuliwa na watu wasiojulikana nikiwa barabarani hapa Iringa," aliandika.
Aliongeza kuwa baada ya kufika kituo cha polisi, viongozi wa Chadema walifika kumuunga mkono.
“Tunatoka Kituo Kikuu cha Polisi Iringa na naelekea kwangu. Kesho tutajua nani alikuwa wanataka kunikamata barabarani usiku huu kwa kunizuia mbele na nyuma. Tutaujuza umma kwa kila hatua”, alisisitiza Nkuna katika chapisho lingine.
Jeshi la Polisi limekanusha madai hayo, likieleza kuwa hakukuwa na shambulio, na tukio hilo lilitokana na ajali iliyosababishwa na Nkuna mwenyewe akiwa amelewa.