Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

USA alishajua na yote hayo Iran alikuwa anasema mkitushambulia sisi tunashambulia base zenu huko.
Kama ulifuatilia USA alianza kuondoa staff wake kwenye hizo kambi

Kama unategemea Iran atadumu kwenye huu mchezo kwa muda mrefu sahahu. Ana wiki mbili tu mbele za kujimwambafai baada ya hapo atatepeta sana
Kwa madhara aliyo yapata kwenye kambi zake sizani kama alitegemea.

Kwani Iraq tu hapo na Afghanistan US alitumia wiki ngapi? Vinchi ambavyo havina hata tech aliyokuwa nayo Iran vilimsumbua ,Iraq peke yake US katumia USD 3T,sasa kwa Iran atatumia kiasi gani.

Hamas pale wanatumia silaha za kuungaunga vita ilienda zaidi ya mwaka. Hizi wiki mbili endelea kuota labda kwa Iran uniambie miaka mitano naweza kukubali.
 
Kwanini unasema haikutegemewa? Hapo ndo swali langu lilipo, Nchi kama Iran haina uwezo wa kufanya hili mpaka uhitimishe kuwa haikutegemewa? Kwanini isiwe kwamba ni possibility za gharama za kuivaima Iran ambazo USA iliweka possibility ya kukutana nazo?
Hakutegemea ndio maana hata madhara aliyo yapata ni makubwa ndio points yangu ilipo na hii imetokana na approach ya mashambulizi awamu hii ni tofauti na awamu ya kwanza.
 
Hakutegemea ndio maana hata madhara aliyo yapata ni makubwa ndio points yangu ilipo na hii imetokana na approach ya mashambulizi awamu hii ni tofauti na awamu ya kwanza.
Uwezekano ni alitegemea na pengine anategemea worse zaidi ya hapa. Iran siyo kikundi cha magaidi ni nchi yenye tech na silaha lazima ujibiwe. Tena hapa wasipoingia raia barabarani kuipinga serikali ya Iran wakawa kitu kimoja na viongozi waliopo USA wanajua kabisa hali inaweza kuwa worse zaidi, hata Trump kwenye speech yake msikilize utajua kuwa haichukulii Iran poa kihivyo.
 
Anachofanya Irani kwa sasa ni kupiga kwa kutumia chochote alichonacho na anapiga popote anapohisi panafikika, maana yuko kwa sasa yuko kama simba aliejeruhiwa!

Kuna muda utafika ambao si mrefu sana ataishiwa makombora alafu atabaki kulialia tu.

Mimi namuona mjinga maana anatumia stock yake ya makombora kupiga target zisizo na faida.
Cyprus kwenye kambi za UK ni target zisizo na faida!??
Iran ameshasema anasafisha missile stockpile ya zamani bado hajaanza kutumia mpya.
Hao tangu utawala wa Kishia uundwe wamekua wanajiandaa na vita.
Jiulize kwanini hawakuishiwa silaha katika vita ya MIAKA NANE DHIDI YA IRAQ!?
Hao wana uzoefu wa vita za miaka mingi.
 
Zitaishaje?..
.iran kwa sasa yeye anapiga popote tu.. Yani ni sawa na kuchukua risasi alafu unaanza kupiga hewani kumbe majambazi wanakuangalia tu, ukiishiwa ndio wanakuja kukupelekea moto vizuri
Amepiga popote wapi?
Unaelewa Iran wana missiles kiasi gani? unaelewa wana drones kiasi gani?

Unaelewa vita ya siku 12 US aliishiwa interceptors kuisaidia Israel? unaelewa Israel pia interceptors ziliisha?

Hii ni source toka new york times.
Na wanatabiri kabisa kuna uwezekano Israel ikaishiwa interceptors kama ilivyotokea 12 days war.
Screenshot 2026-03-02 105330.png


Iran wana missiles nyingi ambazo walisha andaa muda mrefu.
Hio kusema watakiwasha middle east yote ni zaidi ya miaka 20 nyuma wanasema, na finally imefika.
 
Uwezekano ni alitegemea na pengine anategemea worse zaidi ya hapa. Iran siyo kikundi cha magaidi ni nchi yenye tech na silaha lazima ujibiwe. Tena hapa wasipoingia raia barabarani kuipinga serikali ya Iran wakawa kitu kimoja na viongozi waliopo USA wanajua kabisa hali inaweza kuwa worse zaidi.
Hali ni worse tayari eneo lote la Middle east ni la moto hata vikundi vingine Hezboullah na Houthis tayari washaingia mzigoni so US anahitaji sana backup ya NATO kwa sasa. Kwani kambi zake nyingi zimepigwa na meli vita yake kubwa Lincoln imepigwa, so hata hao watakao toa msaada wa meli wajiandae na Houthis.
 
Ndo maana nakuuliza unajuaje kuwa hawakutegemea? Kwanini uipige nchi kama Iran, uue viongozi wake halafu usitegemee majibu ya kiwango cha juu?
Mkuu nadhani hujamuelewa jamaa.
Anachomaanisha yeye USA haikutegemea kama Iran ingeshambulia kwa ukubwa wa kupitiliza.
Kila mtu anasema safari hii IRAN IMEPITILIZA IRAN WENT ROGUE.
Hicho ndicho anachomaanisha jamaa.
 
Rais wa France anawanda wananchi wake kwa uwongo eti Iran inashambulia vibaya sana marafiki zetu US na Israel na hatuwezi kukubali maslaha yetu yaathirike hapo ni wazi wamekiri US na israel peke yao hawamuwezi Iran.

Rais wa Faransa anaendelea na uwongo eti tunaingia kuwasaidia wananchi zetu hahahaha


View: https://youtube.com/shorts/i1kB9O76WYE?si=KPnV8bujnxCtTVbt
 
Iran alisema akishambulia ataifanya vita kuwa kikanda naingia hofu na mashaka kwa kinacho endelea hii ni vita ya kulinda uhai wake.

Waarabu wawe makini sana kuhusu usalama wa tawala zao sina hakika kama Marekani ataweza wahakikishia usalama tawala zote za kiarabu hapo mashariki ya kati pale zitakapo tishika kuanguka.

Tuendelee kusubiri kuona mabadiliko yoyote.
Nimesoma posts zako, umekuza mambo au pengine una mashaka fulani. Iran lazima ifanye retaliations, hiki anachofanya Iran katika maslahi ya US na Israel kilitarajiwa kabisa.

Hadi sasa nguvu ya kijeshi ya Iran imeshapigwa kwa zaidi ya 85%. Anachofanya Iran ni kutapatapa na kujaribu kuondoa uchungu ambao anao moyoni mwake baada ya mapigo anayokoea.

Take this, kadri siku zinavyozidi kwenda anytime utaona Iran nguvu yake ikishuka chini zaidi, na hapo ndipo mission inakuwa imemalizika.

Mimi nilivyoona US kaingia kazini hapo, nilijua kabisa Iran ndo mwisho wake. US ni kubwa sana saaana kwa Iran, mbali tu na Israel kuwa kubwa kwa Iran.
 
Wapalestina wanaofurahia watakuwa wajinga au utakuwa haufikirii.

Justification ya kuchukua Silaha zao imeongezeka mara 100, pia hadi sasa Hamas hawana uwezo wowote wakutoa pole kwa Ndugu zao halisi au Wairan.

Pia hii vita imeziweka karibu nchi za Kiarabu kwa Israel kuliko wakati wowote.

Kumbuka Israel ndio nchi pekee kati yao ndio yenye uwezo wa kuingia Iran na kushambulia
Hizo ni wishes zako wewe.
Ila Wapalestina wote wanafurahi kinachomtokea Israel na wanatamani kama Iran iifutilie mbali hiyo nchi japo ni jambo haliwezekani.

Hizo nchi za kiarabu zilizopigwa vita ikiisha sidhani kama kuna mwenye akili ataruhusu nchi yake ibaki na kambi ya USA.
Maana raia wao wanafurahia serikali yao kupigwa mfano ni Bahrain,kombora likitua raia wanashangilia.
Inaonekana raia hawapendi utawala wao unachokifanya.
 
Hali ni worse tayari eneo lote la Middle east ni la moto hata vikundi vingine Hezboullah na Houthis tayari washaingia mzigoni so US anahitaji sana backup ya NATO kwa sasa. Kwani kambi zake nyingi zimepigwa na meli vita yake kubwa Lincoln imepigwa, so hata hao watakao toa msaada wa meli wajiandae na Houthis.
Upo Sahihi, USA imeingia vitani na Iran lazima ipigane. Huwezi sema iliingia vitani bila mategemeo ya kupigana.
 
Hali ni worse tayari eneo lote la Middle east ni la moto hata vikundi vingine Hezboullah na Houthis tayari washaingia mzigoni so US anahitaji sana backup ya NATO kwa sasa. Kwani kambi zake nyingi zimepigwa na meli vita yake kubwa Lincoln imepigwa, so hata hao watakao toa msaada wa meli wajiandae na Houthis.
Hatari!
 
Nimesoma posts zako, umekuza mambo au pengine una mashaka fulani. Iran lazima ifanye retaliations, hiki anachofanya Iran katika maslahi ya US na Israel kilitarajiwa kabisa.

Hadi sasa nguvu ya kijeshi ya Iran imeshapigwa kwa zaidi ya 85%. Anachofanya Iran ni kutapatapa na kujaribu kuondoa uchungu ambao anao moyoni mwake baada ya mapigo anayokoea.

Take this, kadri siku zinavyozidi kwenda anytime utaona Iran nguvu yake ikishuka chini zaidi, na hapo ndipo mission inakuwa imemalizika.

Mimi nilivyoona US kaingia kazini hapo, nilijua kabisa Iran ndo mwisho wake. US ni kubwa sana saaana kwa Iran, mbali tu na Israel kuwa kubwa kwa Iran.
Sio leo wala kesho,piga mahesabu ya kuanzia miaka mitano. Afghanistan na Iraq hazikuwa na tech ila US pale alisumbuka,Iraq peke yake pale zimepotea USD 3T,sasa kwa Iran US atatumia kiasi gani? Bado washirika wake nao ambao kwa sasa wana hali ngumu kiuchumi, Corona na vita ya Ukraine imetikisa uchumi wao,je watakubali kuweka hela kwenye vita ya Iran, ambaye ananguvu kubwa za kijeshi eneo lote la Middle east hamna anaye mkaribia. So tegemea itakula kote kwa Iran ,NATO na US.
 
Unaandika bila kufikiria sijui mmelishwa nini sasa hezbollah kwa sasa watolea wapi nguvu? Hivi hayo mataifa yote ya kiarabu yaliyorushiwa makombira wakiamua kuingilia vita mtasemaje?
Hawezi kukuelewa huyo Jihadist.
 
Rais wa France anawanda wananchi wake kwa uwongo eti Iran inashambulia vibaya sana marafiki zetu US na Israel na hatuwezi kukubali maslaha yetu yaathirike hapo ni wazi wamekiri US na israel peke yao hawamuwezi Iran.

Rais wa Faransa anaendelea na uwongo eti tunaingia kuwasaidia wananchi zetu hahahaha


View: https://youtube.com/shorts/i1kB9O76WYE?si=KPnV8bujnxCtTVbt

Vita ngumu hiyo.
Hata NATO wakijiunga bado ngumu.
Labda wapigane ground battle,na kwa ground battle ndio kabisaa wanapotea.
Iran ndani ya Iraq peke yake ina vikundi vya jihad VINNE. Vyote vinaunda silaha zake wenyewe wala haitegemei silaha za Iran.
Hizbollah wanaunda silaha wenyewe.
Houthi kwasasa ni JESHI KAMILI lenye sila nyingi kubwa.
Na wanaunda silaha zao wenyewe pia.
Kwahiyo huu mzozo utagua mgumu sana,maana hao NATO wakisogea vita itachukuliwa ya kidini zaidi.
Kier Starmer yeye amesema atairuhusu USA itumie kambi zake ila HATOSHIRIKI VITA.
Hapo ni France ndio kapeleka manowari yake,Ujerumani ni kama UK hawajapeleka kitu.
 
Sio leo wala kesho,piga mahesabu ya kuanzia miaka mitano. Afghanistan na Iraq hazikuwa na tech ila US pale alisumbuka,Iraq peke yake pale zimepotea USD 3T,sasa kwa Iran US atatumia kiasi gani? Bado washirika wake nao ambao kwa sasa wana hali ngumu kiuchumi, Corona na vita ya Ukraine imetikisa uchumi wao,je watakubali kuweka hela kwenye vita ya Iran, ambaye ananguvu kubwa za kijeshi eneo lote la Middle east hamna anaye mkaribia. So tegemea itakula kote kwa Iran ,NATO na US.
Mkuu unaongea ukiwa umetafakari kwa kina au swaumu ya leo imekuwa ngumu?
 
Kwanini unasema haikutegemewa? Hapo ndo swali langu lilipo, Nchi kama Iran haina uwezo wa kufanya hili mpaka uhitimishe kuwa haikutegemewa? Kwanini isiwe kwamba ni possibility za gharama za kuivaima Iran ambazo USA iliweka possibility ya kukutana nazo?
Hivi unaona US ni miungu watu kwamba wakipanga lolote linafanikiwa? kwamba wakishapanga tu lazima wafanikiwe?

Kauli zako zina underestimate sana uwezo wa waajemi...
Haijalishi walifahamu ama kutofahamu, intel huwa zinafeli, haijalishi ni US ama Russia... Trump an wenake ni watu kama wewe, wanakunya na wana mapungufu kama mwanadamu yeyote, hakuna u special wowote, same to waajemi na Israelis.

Unataka kulazimisha hoja kwamba kama US wakipanga mkakati basi ni ngumu kufeli, kitu ambacho historia inakataa.

US na Israel kufeli kwenye hii vita ni kawaida.
!2 days war waliishiwa interceptors, walishindwa kuangamiza nuclear facility na material yaliyomo, Iran bado ana nuclear kaificha, walishindwa pia kufanya regime change.
 
Hali ni worse tayari eneo lote la Middle east ni la moto hata vikundi vingine Hezboullah na Houthis tayari washaingia mzigoni so US anahitaji sana backup ya NATO kwa sasa. Kwani kambi zake nyingi zimepigwa na meli vita yake kubwa Lincoln imepigwa, so hata hao watakao toa msaada wa meli wajiandae na Houthis.
Lincoln haijapigwa kwa shambulio lolote, meli ipo active ikiendelea na majukumu yake.

Unafahamu lakini ulinzi wa hizo Aircraft carriers?
 
Back
Top Bottom