Mkuu nilichosema ni kuwa Israel ikishambuliwa hakuna atayeweza kuzuia video au picha isitoke. Wanaorecord matukio ni watu na simu zao.
Base za marekani zilizopo Qatar zikishambuliwa utazuia vipi watu wasisambaze hizo habari? Hiyo ndio ilikua hoja yangu
Nikakutolea mfano kuwa Iran wamezima internet siku ya 5 leo, lakini kwa nini Kuna watu bado wameweza kuchukua video na kusambaza?
Kwa irani, tunaona taarifa bila kuficha hadi viongozi wao, wanatoa ripoti ya vifo vya raia wao. Lakini Mbona(Marekani na Israel),wao hawatoi ripoti ya vifo vya askari na raia zao pia athari wanazopata kwa kushambuliwa na iran. Kupiga picha na kuchukua video ya mashambulizi ya irani, ndani ya Israel na base za marekani kama Qatari. Sio kigezo cha kukataa uminywaji wa taarifa unaofanywa na Israel na Marekani.
Alafu serikali ya Iran, kuamua kuzima na kupunguza huduma ya internet kipindi hiki cha vita. Ni kutokana na Faida ambazo zina usalama kitaifa. Kwasababu internet inaruhusu mawasiliana ya haraka kupitia Apps. Hivyo wakati wa vita makundi ya uasi au maadui zake wanaweza kutumia apps hizi kupanga mashambulizi.
Hivyo kuzimwa kwa internet kunasaidia kuchelewesha na kuzima mipango yao. Na kingine ni kudhibiti habari zisizo sahihi(misinformation). Maana wakati wa vita habari za uongo zinaweza kusababisha panic kubwa kwa wananchi. Hivyo serikali inaweza kuzima internet ili kupunguza kusambaa kwa taarifa zisizothibitishwa.
La mwisho kabisa ambalo ninaamini nikwamba serikali ya Iran imeamua kuzima na kupunguza huduma ya internet. Ni kuzuia kusambaa taarifa za kijeshi mfano (mahali askari wao walipo) zinaweza kusambaa haraka sana mtandaoni. Hivyo wameamua kuzima internet ili kulinda siri za kijeshi.
Sasa kwanini watu bado ndani ya irani wanaweza kuendelea kusamba picha na video hizo licha ya huduma ya internet kuwa imezimwa.
1:Wakati mwingine serikali huzuia baadhi ya mitandao au apps tu, sio internet yote. Hivyo watu hutumia VPN kupita vizuizi na kutuma picha na video.
2:Baadhi ya watu au waandishi wa habari hutumia internet ya satellite.
Hii haitegemei miundombinu ya internet ya nchi husika.
3:Mtu anaweza kurekodi video.
Akasafiri au kumpa mtu aliye kwenye eneo lenye internet.
Kisha video ikawekwa mtandaoni.
4:Kuna apps ambazo hutuma taarifa simu kwa simu bila internet, kama Briar.
Data husambaa kutoka simu moja kwenda nyingine mpaka ifike kwa mtu mwenye internet.
Hivyo bado hujanijibu kama Israel na Marekani wanaminya taarifa kuhusu vifo vya raia na askari wao na athari anazopata Israel ndani ya nchi yake kupitia mashambulizi yanayofanywa na irani.
Kama unakataa basi huu mjadala uishe kila mtu aendelee kuamini kile anachokijua.