Kwa namna fulani, nilikuwa na mashaka (skeptical) kuhusu idea ya Iran kupigana na America na Israel kwa wakati mmoja. Ila kama nilivyochangia humu hapo awali, hii vita ni asymmetrical, hakuna mshindi outright zaidi ya nani anaweza kuhimili mashambulizi ya muda mrefu kwenye hiyo war of attrition
Kuhusu Israel, sikuiona kama hard nut sana kwa Iran ku-crack, lakini pia sikuwahi kutilia shaka uwezo wa Iran kuwapa America jibu kali. Mawazo yangu yalikuwa kwamba isingechukua zaidi ya siku moja au mbili kwa America kui crush Iran.
Lakini sasa, inashangaza sana kupita kiasi. Inaonekana kama Iran imekaribia kumaliza kabisa (obliterate) nguvu ya kijeshi ya US katika Middle East, uwezo ambao America ilijenga kwa miongo kadhaa kwa gharama na resources nyingi sana
Cha kushangaza zaidi ni kwamba Iran haijatuma hata askari mmoja nje ya Tehran, ni mwendo wa missiles ma drone tu, lakini bado inaonekana inawapunish America na Israel na nchi za kiarabu majirani kwa wakati mmoja. Kwa kweli, hii inaonekana kama kitu kinachozidi uwezo wa kawaida wa binadamu (beyond normal human capabilities).
Hapa kuna rekodi ambayo hakuna taifa duniani limewahi kujaribu, sembuse kuivunja.
Inaonekana Iran inapigana na America na Israel katika fronts nane tofauti kwa wakati mmoja. This is no small feat. Na cha kushangaza zaidi, Iran haionekani kuback down hata kidogo.
Hata Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Aragchi, katika interview moja alisema wazi kwamba hawako tayari kwa negotiation au ceasefire yoyote kwa sasa. Aliongeza kusema kwamba:
“This war is a decisive war between Iran and America.”
Maneno haya yanaonekana kama yanatoka kwa watu wanaojiona wako kwenye position ya strength. Swali linabaki, confidence hii wanaipata wapi?
Inaonekana kama wamejipanga vizuri sana, wako organized na coordinated. Hawapendi bragging wala shouting sana. Mara nyingi wanazungumza kwa utulivu kabisa. Licha ya kupoteza viongozi wakuu kuanzia 12 day war ya June 2025 mpaka hii ya sasa
Tunachokiona ni kwamba wanaendelea tu kutekeleza war programmes zao step by step, according to their schedules.
Kwa mtazamo huo, hawa waajemi wanaonekana kuwapa US na Israel pressure kubwa sana. Wengine hata wanaona kama wanavunja nguvu za kile wanachokiita global Zionist forces.
Moja ya makosa makubwa kabisa unayoweza kufanya ni ku-underestimate au ku-underrate adui zako.
Inaonekana kama US iliwahi ku-underestimate Iran, na sasa kulingana na mtazamo huu wanalipia gharama ya hilo