Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Nyie pigeni propaganda tuu hapa lakini mkae mkijua uwanja wa mapambano upo Iran,anapigwa kama ngoma huko. Halafu hata bila kutumia sayansi ya vita,hivi inakuwaje wewe unarusha missile na drone hovyo hovyo halafu nyumbani kwako unashambuliwa kwa hali zote kuanzia,majini,angani wewe unakula kisago tuu hata kuzuia huwezi halafu ndio uje ushinde vita kwa kutegemea land based missile na one way drone kweli.Hamna upro kuna mijadala ukiisikiliza inakupa picha kamili, maana US walivyo anza tofauti wanavyo maliza. Jana wametoa taarifa raia wake wote wa middle east waondoke, jana hiyo hiyo radar yao ya nne Qatar ikalipuliwa, jana na leo Trump kamvutia waya kulimaliza hili swala kidiplomasia.Ukiviangalia hivi unajua US anahali gani na Iran anahali gani japo naiona hii vita ikiingia phase ya pili ambayo ndio hatari sana na Iran kakataa meza ya mazungumzo.