Trump anataka kumaliza vita, anadai there is nothing left to target
Wapi regime change, au kumuua Khamenei Snr ndiyo regime change?
Base zake zote walizotumia gharama kubwa na resources nyingi kuzijemga zaidi ya miaka 40 zimekuwa obliterated completely
Mshirika wa vita ndiyo huyo anapelekewa missiles kila siku na hiyo ineffective “Iron” dome yao na tayari kelele za wananchi kuanza kuchoshwa na maisha ya kwenye mahandaki
Aircraft carriers zimejificha kama daladala wakati wa maandamano
Iran inaibuka kama mshindi wa vita, (the total war not the battle) wakati nguvu za kimataifa za United States na Israel zinaonekana kudhoofika polepole katika mfumo wa global power structure.
Ikiangaliwa kwa analytical perspective, Iran inaonekana kuwa inapigana anti-colonial war yaani vita vya kulinda rasilimali (aka vita ya kiuchumi) zake za mafuta (oil), gas na sovereignty ya taifa. Kwa mantiki hiyo, mtu angeweza kutarajia kwamba jamii katika bara la Africa ambazo bado zinakabiliwa na athari za ukoloni wa kiuchumi zingekuwa zinaishangilia Iran, kwa sababu kwa namna fulani inaonekana kupigania mapambano yanayofanana na yao.
Hata hivyo, waAfrika wa kipindi cha neoliberal era hawalioni jambo hilo kwa mtazamo huo.
Watu wanashabikia zaidi kwa emotions na itikadi za kidini
Jamii nyingi zimekuwa miseducated politically, kiasi kwamba hawatambui kwamba colonialism bado ipo katika zama za sasa, lakini katika sura tofauti. Ukoloni wa leo hauji kwa mfumo wa utawala wa moja kwa moja kama zamani; badala yake umebadilika kuwa technical na depoliticised systems kama vile debt structures, international banking systems na global monopolies za kiuchumi
Wengi hawakuwahi kufikiria kwamba kile kinachoitwa Imperialist United States pamoja na Zionist Israel wangeweza kukabiliwa na kile kinachoonekana kama strategic embarrassment katika vita dhidi ya Iran.
Iran imeonyesha kile ambacho jeshi linalochota inspiration kutoka katika historia yake, utamaduni wake, na national identity linaweza kufanya katika uwanja wa geopolitics.
Katika mtazamo huu, free and righteous world pamoja na allies wa Iran wanapaswa kujivunia kile kinachoonekana kama exposure na dismantling ya aura ya US hegemony. Hegemony hiyo imedumu kwa muda mrefu kwa sababu ya perception ya nguvu kubwa ya Marekani, ambayo imekuwa ikiathiri na kudhibiti nchi nyingi zilizoendelea kidogo kiuchumi.
Kwa mantiki hiyo ya kisiasa, Iran imeonyesha kwamba Marekani ambayo kwa muda mrefu imeonekana kama nguvu isiyopingika inaweza kuwa “paper tiger”, yaani nguvu ambayo taswira yake ni kubwa kuliko uwezo wake halisi.
Mfumo wa kimataifa ambao uliwahi kulazimisha baadhi ya mataifa yaliyoendelea kidogo kuingia katika dependency au subordinate position, sasa unaonekana kudhoofika polepole.
Bila kujali outcome ya mwisho ya vita, katika siku zijazo dunia inaweza kuanza kuheshimu Iran zaidi kama nguvu ya kisiasa na kijeshi, kwa sababu hatua zake zinaonekana kuwa sehemu ya kuibuka kwa multipolar world order au mfumo wa dunia ambapo nguvu za kimataifa hazitatawaliwa tena na taifa moja pekee, bali zitagawanyika kati ya mataifa kadhaa yenye ushawishi.
Uthubutu, courage pamoja na resilience ya Iran vinaweza kuwa mojawapo ya sababu zinazochochea mwanzo wa mfumo huo mpya wa kimataifa.
Mara tu vita hii itakapomalizika, China itageuka kimya kimya kuwa superpower ya dunia, bila hata kupigana vita
Russia ina deni kidogo sana la ndani na iko katika nafasi nzuri ya ku-thrive kiuchumi na kisiasa katika siku zijazo.
Kwa hiyo dunia inaweza kuelekea kwenye multipolar world order, wakati US ikiendelea kushuka chini katika global power hierarchy, ikiwa imeelemewa na migogoro ya kisiasa ya ndani pamoja na ushawishi wa kisiasa unaohusishwa na Israel, unaonekana kama ukivuta au kutumia kwa kiasi kikubwa rasilimali na utajiri wa Marekani.