Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Mkuu hujui kwa nini Iran anashambuliwa had leo? Aisee mkwara wote Ayatolah aliyokuwa anamchimba Marekan na Israel ulikuwa huusikiu?
Kwa hiyo kusema tu maneno ndo sababu ya kwenda kuua watu na kuiharibu nchi?

Yale yale ya Iraq kwamba kuna silaha za maangamizi makubwa kumbe ni uongo tu.

Hiyo sababu uliyoitoa ni utoto.

Huanzishi vita kisa maneno tu ya mtu ambaye hawezi kukufanya chochote.
 
Kwa mujibu wa Trump
Kumzuia asiwe na nuclear
Kuharibu uwezo wake wa kutengeneza missiles
Kifupi asiwe tishio kwa US na Israel.
Ushahidi sijui wana ushahidi gani.
Na kwa hili kafanikiwa jamaa kachapika mno hata wale wachambuzi waliokuwa wanampa sifa kuwa ni supper power sasa hivi wametokomea maana walidanganya watoto wa 2000 sasa hivi hawana cha kuwadanganya maana ukweli umejulikana nani mbabe.
 
Hadi muda huu ni zaidi ya majengo 35,600 yameonja joto la USA na zaidi ya raia million 3.4 hawana makazi l

Pro Iran endeleeni kuandika ma paragraph ya kujifariji😀
Nilisema siku watu wanazipuuzia Israel na Marekani

Kwa target walizopiga Iran wanaweza kuteka nchi zaidi ya 20 Africa kwa mwezi
 
Kwa hiyo kusema tu maneno ndo sababu ya kwenda kuua watu na kuiharibu nchi?

Yale yale ya Iraq kwamba kuna silaha za maangalizi makubwa kumbe ni uongo tu.

Hiyo sababu uliyoitoa ni utoto.

Huanzishi vita kisa maneno tu ya mtu ambaye hawezi kukufanya chochote.
Mkuu mtu ambaye anajenga nuclear capability na anasema lengo ni kuifuta Israel kwenye uso wa dunia unasubiri ushahidi kwamba mpaka alipue ndio uchukue hatua?
 
Nilisema siku watu wanazipuuzia Israel na Marekani

Kwa target walizopiga Iran wanaweza kuteka nchi zaidi ya 20 Africa kwa mwezi
Nilisoma hio post niliona ulivyoshambuliwa. Eti kuna mtu akasema Algeria anamtosha Israel! Kuna vituko humu.
 
Okay unacho cha kuonesha kwamba New York Times ni waongo? Hapa issue ni references, wewe unaweza sema based on your differennt sources/references, unataja chombo then unaonesha uongo wao na sio maneno matupu.
Unasoma ninachoandika kweli?

Nimesema waongo?

unajaribu kuniwekea mdomoni kauli ambayo sijaisema ,maana mshazoea cheap propaganda .

Nilichosema ni kwamba kuripoti tukio moja hakumaanishi hitimisho kubwa unalotoa wewe ni sahihi.

Kwa mfano, media inaweza kuripoti kwamba rada fulani iliharibiwa kwenye shambulio, lakini hiyo si sawa na kusema Marekani imepoteza kabisa uwezo wake wa rada au udhibiti wa anga.

Marekani ina mtandao mkubwa wa rada na vituo vya kijeshi katika eneo lote la Middle East, hivyo kupotea kwa kifaa kimoja hakubadilishi mfumo mzima wa ulinzi wa anga.

Hata kwenye masuala ya carrier kama USS Gerald R. Ford, kama kweli ingepigwa na kombora la adui hilo lingekuwa tukio kubwa sana la kijeshi na kisiasa duniani.

Tukio la aina hiyo lingethibitishwa na vyanzo vingi tofauti, satellite imagery, wachunguzi huru wa OSINT, na media nyingi za kimataifa, sio video chache za YouTube za watafuta Viewer unazoweka humu.


Kwa hiyo hoja yangu ni rahisi tu, media inaweza kuripoti tukio, lakini lazima utenganishe kati ya kilichoandikwa na hitimisho unalojenga wewe,kudanganya watu humu ,

Angalia mfano propaganda mbayoisambaza ya Netanyau kuuwawa,mnatia aibu sana,
 
Kwani vita imeisha mkuu?
Bado mkuu ila data zinaonesha wamechapika mno na kama Marekan wataendelea kutumia B-2 bombers had kufikia tareh 28 mwezi huu nahis Netanyahu anaweza akawa anapiga misele kwenye viunga vya Tehran maana jamaa watakuwa wameisha na waliopo watakuwa wanajificha pangoni maana Amerika wameshaweka dau watu watoe location sasa kwa maisha ya wa Iran yalivyo magumu wanaweza kweli achia hilo donge nono la Amerca? Hata ingekuwa ni wewe mkuu unaweza achia donge nono wakati wa njaa kali?

Kifupi ni kuwa raia wa Iran kwa sasa wana uhuru wa kunivinjari kwenye nchi yao kuliko viongozi wao na wanavaa watakavyo hakuna mtu wa kuwabuguzi
 
Wewe unasikilizaga interview za viongozi na maafisa wa Kiyahudi,Aliyekuwa msemaji wa jeshi la Kiyahudi Lipkin anadai nusu Syria ni yao,Lebanon yote yao,Jordan yao Saudi Arabia nusu ikiwemo Makka na Madina yao, kuna portion ya Misri wanadai yao na kuna Portion Turkey wanadai ya kwao. Hao Saudi,Turkey Misri hata Qatar ni swala la muda wataundiwa zengwe kama la Palestine.Myahudi mbabe anachukua maeneo ya watu kibabe.

View: https://m.youtube.com/shorts/WERJ_xXhaeQ
Haya msikilize aliye kuwa waziri mkuu wa Israel anadai Qatar na Turkey wanahatarisha usalama wao, utapata picha kwamba siku yoyote Myahudi ataingia vitani na Qatar pamoja na Mturuki.

View: https://m.youtube.com/shorts/kaOWgujCHtA
Kwa kifupi Myahudi mkorofi hata hii vita huoni sababu ya msingi, so tujiandae na vita ya Myahudi zidi ya Qatar, Turkey, Misri, Saudi Arabia.

Hizo video za YouTube shorts ndizo chanzo cha propaganda nyingi. Unachukua clip fupi ya mtu mmoja halafu unageuza kana kwamba ndiyo sera rasmi ya taifa. Israel ina serikali, jeshi na sera za nje rasmi; si kila mtu aliyewahi kuwa msemaji au mwanasiasa anaongea sera ya nchi.

Huyo unayemtaja, Avi Lipkin, si mtu anayetoa sera rasmi ya Israel. Ni mchambuzi na mwanaharakati wa kisiasa ambaye mara nyingi hutoa maoni yake binafsi kuhusu geopolitics.

Maoni ya mtu mmoja hayamaanishi kwamba Israel inadai Syria, Lebanon, Saudi Arabia au Uturuki.

Halafu ukiangalia sera rasmi ya Israel, imewahi hata kusaini mikataba ya amani na majirani zake kama Egypt na Jordan.

Kama lengo lao ni kuchukua nchi zote hizo kwa nini wasaini mikataba ya amani na kushirikiana nao kiusalama?

Na kuhusu madai kwamba Israel itapigana na Qatar au Turkey, viongozi wengi duniani huwa wanakosoa au kutaja nchi nyingine kama tishio la kisiasa. Hiyo si sawa na kusema kuna mpango wa kuivamia nchi hiyo.
 
Kwa mujibu wa Trump
Kumzuia asiwe na nuclear
Kuharibu uwezo wake wa kutengeneza missiles
Kifupi asiwe tishio kwa US na Israel.
Ushahidi sijui wana ushahidi gani.
Mwezi wa sita Trump huyo huyo alisema nuclear facilities za Iran zimeangamizwa.

Iran asiwe na uwezo wa kutengeneza makombora……huu ni unafiki!

Yeye Marekani anao uwezo wa kutengeneza makombora.

Kwa nini Iran asiwe na huo uwezo?

Iran asiwe tishio kwa US na Israel…….unafiki mwingine huu!

Hivi kuna nchi gani nyingine hapa duniani ambazo ni tishio kwa nchi zingine zaidi ya Israel na Marekani?

Israel na Marekani ndo nchi zinazovamia nchi zingine kwa kiwango kikubwa sana na ushahidi upo.

Marekani imewahi kuivamia Panama, Vietnam, Venezuela, Iraq, Iran, na sasa wanazungumzia kuivamia Cuba, achilia mbali kushiriki kuua viongozi wa mataifa mengine na kuunga mkono serikali za kidikteta kama za Saudi Arabia, Zaire, na zinginezo, hii ndo Marekani iliyo na hofu ya kushambuliwa na Iran?

Iran haijawahi kuanzisha vita wala kuivamia nchi nyingine yoyote ile hapa duaniani!

Ila wale ambao wana historia ya kuvamia nchi zingine ndo walio na hofu ya kushambuliwa na Iran! Vichekesho.

Tuje kwa Israel. Hawa kila siku wanaanzisha vita huko Mashariki ya Kati. Wanaua viongozi wa mataifa mengine.

Hawa nao ndo wana hofu ya kushambuliwa na Iran?

Israel na mshirika wake Marekani ndo waanzisha vita dhidi ya Iran.

Iran haijawahi kuanzisha vita dhidi yao.

Huu unafiki ni wa kipekee sana.
 
Back
Top Bottom