Yaleyale unabishana na source na sio sources hata anaye ongea nae unasema uongoa,tena afisa wa jeshi hiyo haitoshi Prime Minister Naftal Bennet, hawa hawaongei hongei wanavyo viongea hivyo ni plan ya baadae.
Wewe hata dunia inavyo enda hujui, vita ni long term plan hizi vita za nchi Saba ambazo US alipigana havikuzuka kama Uyoga.Zaidi ya miaka 20 General Clack aliyekuwa mkuu wa vikosi vya NATO alipokea mpango wa vita kutoka Secretary of Defense wa kuingia vita na nchi saba,Yemen,Iraq,Lebanon, Syria, Somalia,Iran. Baada ya hapo yote yaliyo ongelewa yalitekelezwa.
Kusaini mkataba kitu gani,kwani US si alikuwa na mazungumzo ya amani Iran mara mbili, mara ya kwanza wakati mazungumzo ya kiendelea ,waliwapiga mageneral wa Iran, mara ya pili wakampiga Ayatollah. US na Myahudi tokea lini wanaheshimu mikataba? Kile alichofanya Venezuela ni kinyume,kabisa na mikataba yote ya kimataif,kilicho fanyika Libya,Iraq ni kinyume kabisa na mikataba na ubaya zaidi Libya na Iraq walipigwa kwa sababu za uongo. Myahudi alicho mfanyia Mpalestina ni kinyume na mikataba yote ya kimataifa na kiubinadamu. Kuna mataifa yanaheshimu mikataba ila sio US na Myahudi.
Unaleta Conspiracy theory sasa
Unachanganya mambo matatu tofauti, maoni ya watu, mipango ya kijeshi , na sera rasmi za nchi.
Mnaikurupukia sana Geopolitics, kuhusu mpango wa nchi saba. Ni kweli kwamba Wesley Clark aliwahi kusema kwenye mahojiano kwamba baada ya 9/11 aliambiwa na afisa mmoja Pentagon kuhusu memo iliyodai mpango wa kushambulia nchi kadhaa kama Iraq, Syria, Libya, Somalia, Sudan na Iran.
Hata juzi nimelisema somewhere,
Lakini hata yeye mwenyewe alisema yalikuwa mazungumzo aliyosikia kutoka kwa afisa mmoja, si sera rasmi iliyopitishwa hadharani na serikali.
Ndiyo maana hata katika miaka iliyofuata ratiba hiyo haikutekelezwa kama alivyosema,kwa mfano Lebanon na Sudan hazikuvamiwa.
kusema kwamba kila tukio la vita duniani ni sehemu ya mpango mmoja wa siri wa miaka 20 ni simplification kubwa sana ya geopolitics., unaingia kwenye Conspiracy theory,
Vita vya Iraq 2003, Libya 2011, Syria na vingine vilikuwa na sababu tofauti za kisiasa, kiusalama na kikanda. Hata wachambuzi wengi wa Marekani wanakubali baadhi ya vita hizo zilikuwa makosa.
Hata kama unakosoa Marekani au Israel kuhusu mikataba,ukweli bado ni kwamba nchi hizo zimesaini na kuheshimu mikataba mingi ya kimataifa.
Mfano ni mkataba wa amani kati ya Israel na Egypt ambao bado upo zaidi ya miaka 40, pamoja na mkataba na Jordan. Kama hawaheshimu mikataba kabisa, mikataba hiyo isingedumu kwa muda wote huo.
Kwa kifupi, ni sawa kukosoa sera za Marekani au Israel, lakini kusema kwamba kila kitu kinachotokea Mashariki ya Kati ni mpango wa siri wa kuvamia dunia ni kuleta Conspiracy theory.
Geopolitics ni ngumu zaidi kuliko mnavyodhani ,
Kuna taifa lenye ukandamizaji wa haki kama hao Iran ?