Unaleta Conspiracy theory sasa
Unachanganya mambo matatu tofauti, maoni ya watu, mipango ya kijeshi , na sera rasmi za nchi.
Mnaikurupukia sana Geopolitics, kuhusu mpango wa nchi saba. Ni kweli kwamba Wesley Clark aliwahi kusema kwenye mahojiano kwamba baada ya 9/11 aliambiwa na afisa mmoja Pentagon kuhusu memo iliyodai mpango wa kushambulia nchi kadhaa kama Iraq, Syria, Libya, Somalia, Sudan na Iran.
Hata juzi nimelisema somewhere,
Lakini hata yeye mwenyewe alisema yalikuwa mazungumzo aliyosikia kutoka kwa afisa mmoja, si sera rasmi iliyopitishwa hadharani na serikali.
Ndiyo maana hata katika miaka iliyofuata ratiba hiyo haikutekelezwa kama alivyosema,kwa mfano Lebanon na Sudan hazikuvamiwa.
kusema kwamba kila tukio la vita duniani ni sehemu ya mpango mmoja wa siri wa miaka 20 ni simplification kubwa sana ya geopolitics., unaingia kwenye Conspiracy theory,
Vita vya Iraq 2003, Libya 2011, Syria na vingine vilikuwa na sababu tofauti za kisiasa, kiusalama na kikanda. Hata wachambuzi wengi wa Marekani wanakubali baadhi ya vita hizo zilikuwa makosa.
Hata kama unakosoa Marekani au Israel kuhusu mikataba,ukweli bado ni kwamba nchi hizo zimesaini na kuheshimu mikataba mingi ya kimataifa.
Mfano ni mkataba wa amani kati ya Israel na Egypt ambao bado upo zaidi ya miaka 40, pamoja na mkataba na Jordan. Kama hawaheshimu mikataba kabisa, mikataba hiyo isingedumu kwa muda wote huo.
Kwa kifupi, ni sawa kukosoa sera za Marekani au Israel, lakini kusema kwamba kila kitu kinachotokea Mashariki ya Kati ni mpango wa siri wa kuvamia dunia ni kuleta Conspiracy theory.
Geopolitics ni ngumu zaidi kuliko mnavyodhani ,
Kuna taifa lenye ukandamizaji wa haki kama hao Iran ?