Kutarajia Iran au Marekani atashinda vita kama ngumi za mtaani ni kutojua mambo.
Achana na maneno ya propaganda au kushindisha kuwa Uislamu ulikuwepo kabla ya Mtume Mohammed, au ukristo ulikuwepo kabla ya Yesu.
Fact ni kuwa Wayahudi na dini yao walikuwepo pale kabla ya hao wote, na wamepitia vipindi vya manyanyaso kutoka kwa Waislamu na Wakristo wakichinjwa na kuuwawa hovyo.
Iran amekuwa tishio kwao kwa kutaka taifa la Palestine liwepo na lichukue maeneo ambayo Waisrael ni yao.
Matokeo kwa mtazamo wangu Iran na Marekani wataumiza uchumi wao, lakini Iran ataumia zaidi kwa sababu hajawa na maguvu makubwa ya kiuchumi kama mpinzani wake katika vita. Kwa upande Israel huyu anapewa feva na mataifa ya ulaya ataweza kupona haraka.
Waarabu walikosea sana kukataa hii ramani ya kuanzishwa kwa Palestina, Wayahudi walikubali ingawa waliona kama wamepunjwa. Kama wangekubali nadhani ungekuwa mwanzo mzuri wa kuendea mengine wanayoyaamini.
Sioni kama Palestine watapata taifa miaka ya karibuni.