Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Israel na Marekani wanazo silaha nyingi tu za nuclear na ni Marekani pekee ambayo imewahi kuzitumia hizo silaha. Uongo au kweli?Mkuu mtu ambaye anajenga nuclear capability na anasema lengo ni kuifuta Israel kwenye uso wa dunia unasubiri ushahidi kwamba mpaka alipue ndio uchukue hatua?
Kwani uongo lazima useme direct, maana huamini wanacho ripoti na sawa na kusema waongo. Hitimisho lipi wakati kweli wamepiga na baadhi ya image ya hizo photo wameshare.Unasoma ninachoandika kweli?
Nimesema waongo?
unajaribu kuniwekea mdomoni kauli ambayo sijaisema ,maana mshazoea cheap propaganda .
Nilichosema ni kwamba kuripoti tukio moja hakumaanishi hitimisho kubwa unalotoa wewe ni sahihi.
Kwa mfano, media inaweza kuripoti kwamba rada fulani iliharibiwa kwenye shambulio, lakini hiyo si sawa na kusema Marekani imepoteza kabisa uwezo wake wa rada au udhibiti wa anga.
Marekani ina mtandao mkubwa wa rada na vituo vya kijeshi katika eneo lote la Middle East, hivyo kupotea kwa kifaa kimoja hakubadilishi mfumo mzima wa ulinzi wa anga.
Hata kwenye masuala ya carrier kama USS Gerald R. Ford, kama kweli ingepigwa na kombora la adui hilo lingekuwa tukio kubwa sana la kijeshi na kisiasa duniani.
Tukio la aina hiyo lingethibitishwa na vyanzo vingi tofauti, satellite imagery, wachunguzi huru wa OSINT, na media nyingi za kimataifa, sio video chache za YouTube za watafuta Viewer unazoweka humu.
Kwa hiyo hoja yangu ni rahisi tu, media inaweza kuripoti tukio, lakini lazima utenganishe kati ya kilichoandikwa na hitimisho unalojenga wewe,kudanganya watu humu ,
Angalia mfano propaganda mbayoisambaza ya Netanyau kuuwawa,mnatia aibu sana,
USA na ISRAEL airpower sio ya dunia hii, hapo Iran inasaidiwa na kua na milima mingi na hizo drones..Nilisema siku watu wanazipuuzia Israel na Marekani
Kwa target walizopiga Iran wanaweza kuteka nchi zaidi ya 20 Africa kwa mwezi
Ushawahi kuzisikia kauli za Smotrich?Ni kweli. Ila sidhani katika ugomvi wake wote ashatishia kumfuta mtu kwa nyuklia. Sijui.
Kim Jong UN, baba yake, na babu yake wote washatoa kauli za kuifuta Korea Kusini, ambaye ni mshirika wa Marekani.Ni kweli. Ila sidhani katika ugomvi wake wote ashatishia kumfuta mtu kwa nyuklia. Sijui.
Sijasema The New York Times ni waongo.,elewa hilo kwanza, Nilichosema ni kwamba kwenye vita claim, report na confirmation ni vitu tofauti. Media inaweza kuripoti kuwa shambulio limetokea au kifaa fulani kimeharibiwa, lakini wachambuzi wa kijeshi husubiri uthibitisho wa kujitegemea kabla ya kusema hitimisho kubwa kama mfumo mzima umeharibiwa au udhibiti wa anga umepotea.Kwani uongo lazima useme direct, maana huamini wanacho ripoti na sawa na kusema waongo. Hitimisho lipi wakati kweli wamepiga na baadhi ya image ya hizo photo wameshare.
Hiki ulicho kiandika sikukiona vizuri....
"Ndiyo maana wachambuzi wa kijeshi huwa wanangoja uthibitisho wa kujitegemea kabla ya kusema tukio fulani limethibitishwa kabisa."
Halafu natamani ukawasikilize wachambuzi wa kijeshi wenyewe wanavyo izungumiza hii vita,tena kule kwenye Podcast unakutana na wanajeshi wenyewe waliopigana vita,kwa kuanzia unaweza ukaaza na US Marine Scott Ritter huyu kazi yake ilikuwa ni kupeleleza Iraq,baada ya hapo unaweza sema bora New York Times, maana sometimes jamaa anaongea vitu vya ndani ,ambavyo hujawahi kuvisikia kwenye media yoyote.
Yaleyale unabishana na source na sio sources hata anaye ongea nae unasema uongo,tena afisa wa jeshi hiyo haitoshi Prime Minister Naftal Bennet, hawa hawaongei hongei wanavyo viongea hivyo ni plan ya baadae.Msemaji wa jeshi anaongea kile kinacho ongewa na jeshi, hajiongelei kwani wana viapo, Waziri nae hajiongelei anashiriki kwenye vikao vya juu vya maamuzi ya kiusalama na kiulinzi ya nchi.Hizo video za YouTube shorts ndizo chanzo cha propaganda nyingi. Unachukua clip fupi ya mtu mmoja halafu unageuza kana kwamba ndiyo sera rasmi ya taifa. Israel ina serikali, jeshi na sera za nje rasmi; si kila mtu aliyewahi kuwa msemaji au mwanasiasa anaongea sera ya nchi.
Huyo unayemtaja, Avi Lipkin, si mtu anayetoa sera rasmi ya Israel. Ni mchambuzi na mwanaharakati wa kisiasa ambaye mara nyingi hutoa maoni yake binafsi kuhusu geopolitics.
Maoni ya mtu mmoja hayamaanishi kwamba Israel inadai Syria, Lebanon, Saudi Arabia au Uturuki.
Halafu ukiangalia sera rasmi ya Israel, imewahi hata kusaini mikataba ya amani na majirani zake kama Egypt na Jordan.
Kama lengo lao ni kuchukua nchi zote hizo kwa nini wasaini mikataba ya amani na kushirikiana nao kiusalama?
Na kuhusu madai kwamba Israel itapigana na Qatar au Turkey, viongozi wengi duniani huwa wanakosoa au kutaja nchi nyingine kama tishio la kisiasa. Hiyo si sawa na kusema kuna mpango wa kuivamia nchi hiyo.
Tutawafukua Mashoga wote kwenye Ardhi zetu takatifu na mabaki yao watapokea kwa lazima Ulaya!!
View: https://x.com/clashreport/status/2032786631036408135
Iran waltegemea nini?
Zelensky ni myahudi na wayahudi wote ndoto yao ni kuzikwa Israel
Huyo Scott Ritter US Marine halafu kazi yake ni mpelelezi kaa ukijua yeye ana sources za uhakika tena zipo kwenye uwanja wa kivita na tena yeye anaongea kwa kujiamini na hata hizo Radar kulipulia kazungumzia tena kwa kujiamini. Sasa Reputable media huziamini hao wachambuzi ambao unaowasema uwahamini,utaziamini Satellite image nikizileta? maana vyombo vya China na India wameshare sana Satellite images za US military resources zilizopigwa. Ila hata zikiletwa bado utasema za Propaganda za uwongo.Sijasema The New York Times ni waongo.,elewa hilo kwanza, Nilichosema ni kwamba kwenye vita claim, report na confirmation ni vitu tofauti. Media inaweza kuripoti kuwa shambulio limetokea au kifaa fulani kimeharibiwa, lakini wachambuzi wa kijeshi husubiri uthibitisho wa kujitegemea kabla ya kusema hitimisho kubwa kama mfumo mzima umeharibiwa au udhibiti wa anga umepotea.
SASA wewe unakuja na hitimisho kabisa ,hapo ndio wenye ufahamu tunakushangaa ,hizi propaganda cheap waachie watu wa fb.
Kuhusu picha ulizosema zimesambazwa, hata kwenye vita nyingi zilizopita imeonekana mara nyingi picha au video hutolewa nje ya context au zinahusishwa na tukio tofauti.
Ndiyo maana wachambuzi wa OSINT huwa wanatafuta satellite imagery, geolocation na vyanzo vingi tofauti kabla ya kuthibitisha tukio.
Halafu huyu Scott Ritter, ni kweli alikuwa United States Marine Corps zamani na alifanya kazi ya ukaguzi wa silaha Iraq, lakini leo yeye ni mchambuzi wa kisiasa mwenye maoni yake binafsi., ,kwenye Mambo kama haya usitegemee mtu au Chanzo kimoja ,mwisho wa siku mnajiabisha na kuleta Propaganda za kipuuzi kama hii ya Netanyau kafa, mara Abraham Lincoln imepigwa,full VITUKO .
Wachambuzi wa kijeshi duniani hawalingani wote; kuna wanaokubaliana naye na kuna wengi wanaompinga. Ndiyo maana kwenye masuala ya vita watu hutazama vyanzo vingi tofauti, si mtu mmoja tu.
Kwa hiyo hoja yangu bado ni ile ile, kwenye vita kuna propaganda kutoka pande zote.
Tofauti ya propaganda na reality ni uthibitisho kutoka vyanzo vingi vinavyojitegemea, sio claim ya upande mmoja au maoni ya mchambuzi mmoja.
Kim anayo tayari. Ukimgusa ni mbaya kuliko kumuacha. Huyu hana ndio maana eanamchachafya ili asiwe nayo. Hapa sisemi kwamba ni sawa au si sawa.Kim Jong UN, baba yake, na babu yake wote washatoa kauli za kuifuta Korea Kusini, ambaye ni mshirika wa Marekani.
Na kila mara Korea Kaskazini huwa inaichimba biti Korea Kusini.
Ushaona Marekani ikiivamia Korea Kaskazini kisa imetoa maneno ya vitisho dhidi ya mshirika wake?
Naomba Link mtaalamKwani uongo lazima useme direct, maana huamini wanacho ripoti na sawa na kusema waongo. Hitimisho lipi wakati kweli wamepiga na baadhi ya image ya hizo photo wameshare.
Hiki ulicho kiandika sikukiona vizuri....
"Ndiyo maana wachambuzi wa kijeshi huwa wanangoja uthibitisho wa kujitegemea kabla ya kusema tukio fulani limethibitishwa kabisa."
Halafu natamani ukawasikilize wachambuzi wa kijeshi wenyewe wanavyo izungumiza hii vita,tena kule kwenye Podcast unakutana na wanajeshi wenyewe waliopigana vita,kwa kuanzia unaweza ukaaza na US Marine Scott Ritter huyu kazi yake ilikuwa ni kupeleleza Iraq,baada ya hapo unaweza sema bora New York Times, maana sometimes jamaa anaongea vitu vya ndani ,ambavyo hujawahi kuvisikia kwenye media yoyote.
Sijawahi.Ushawahi kuzisikia kauli za Smotrich?
Sijui hata unaniuliza ili iweje wakati kitu kiko wazi.Israel na Marekani wanazo silaha nyingi tu za nuclear na ni Marekani pekee ambayo imewahi kuzitumia hizo silaha. Uongo au kweli?
Unaleta Conspiracy theory sasaYaleyale unabishana na source na sio sources hata anaye ongea nae unasema uongoa,tena afisa wa jeshi hiyo haitoshi Prime Minister Naftal Bennet, hawa hawaongei hongei wanavyo viongea hivyo ni plan ya baadae.
Wewe hata dunia inavyo enda hujui, vita ni long term plan hizi vita za nchi Saba ambazo US alipigana havikuzuka kama Uyoga.Zaidi ya miaka 20 General Clack aliyekuwa mkuu wa vikosi vya NATO alipokea mpango wa vita kutoka Secretary of Defense wa kuingia vita na nchi saba,Yemen,Iraq,Lebanon, Syria, Somalia,Iran. Baada ya hapo yote yaliyo ongelewa yalitekelezwa.
Kusaini mkataba kitu gani,kwani US si alikuwa na mazungumzo ya amani Iran mara mbili, mara ya kwanza wakati mazungumzo ya kiendelea ,waliwapiga mageneral wa Iran, mara ya pili wakampiga Ayatollah. US na Myahudi tokea lini wanaheshimu mikataba? Kile alichofanya Venezuela ni kinyume,kabisa na mikataba yote ya kimataif,kilicho fanyika Libya,Iraq ni kinyume kabisa na mikataba na ubaya zaidi Libya na Iraq walipigwa kwa sababu za uongo. Myahudi alicho mfanyia Mpalestina ni kinyume na mikataba yote ya kimataifa na kiubinadamu. Kuna mataifa yanaheshimu mikataba ila sio US na Myahudi.
Sawa.Technical Egpty alimpiga Muisrael 1973 yom Kippur war, so Is Jordan hio vita Yao fupi ya Vifaru.
I don't think Algeria na Egpty capability Yao inatofautiana Sana.
Zipo nyingi ukiandika Scott Ritter zinakuja nyingi ila anachannel yake na vilevile kuna Podcast na Interview nyingi ambazo amezifanya.Naomba Link mtaalam
Wkt huo huo Trump na team yake Awajui Kiongoz mpya wa Iran yupo wapi kias cha kuweka pesa mezani 💰 dollars million 10 kwa yoyote mwenye taarifa muhimu za uko alipo.!!!Kwa mujibu wa Trump
Kumzuia asiwe na nuclear
Kuharibu uwezo wake wa kutengeneza missiles
Kifupi asiwe tishio kwa US na Israel.
Ushahidi sijui wana ushahidi gani.