Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Ndo unafiki wenyewe huo sasa.Kim anayo tayari. Ukimgusa ni mbaya kuliko kumuacha. Huyu hana ndio maana eanamchachafya ili asiwe nayo. Hapa sisemi kwamba ni sawa au si sawa.
Hio mistari miwili ya mwisho tupo pamoja.Majuzi tu hapa Trump alikuwa anazungumzia kuiteka Greenland π€£.
Halafu watu bado wanaiona Marekani kuwa ni nchi yenye wema sana.
Marekani ina mengi sana yaliyo mazuri lakini pia ina mengi yaliyo mabaya.
Kuwa mwanajeshi wa zamani hakumaanishi kila analosema leo ni ukweli wa mwisho,ndio tuhitimishe ni 100%.Huyo Scott Ritter US Marine halafu kazi yake ni mpelelezi kaa ukijua yeye ana sources za uhakika tena zipo kwenye uwanja wa kivita na tena yeye anaongea kwa kujiamini na hata hizo Radar kulipulia kazungumzia tena kwa kujiamini. Sasa Reputable media huziamini hao wachambuzi ambao unaowasema uwahamini,utaziamini Satellite image nikizileta? maana vyombo vya China na India wameshare sana Satellite images za US military resources zilizopigwa. Ila hata zikiletwa bado utasema za Propaganda za uwongo.
Kilicho wazi ni nini? Unafiki wako na wenzio mnaoona ni halali kwa Marekani na Israel kuishambulia Iran?Sijui hata unaniuliza ili iweje wakati kitu kiko wazi.
Unaleta Conspiracy theory sasa
Unachanganya mambo matatu tofauti, maoni ya watu, mipango ya kijeshi , na sera rasmi za nchi.
Mnaikurupukia sana Geopolitics, kuhusu mpango wa nchi saba. Ni kweli kwamba Wesley Clark aliwahi kusema kwenye mahojiano kwamba baada ya 9/11 aliambiwa na afisa mmoja Pentagon kuhusu memo iliyodai mpango wa kushambulia nchi kadhaa kama Iraq, Syria, Libya, Somalia, Sudan na Iran.
Hata juzi nimelisema somewhere,
Lakini hata yeye mwenyewe alisema yalikuwa mazungumzo aliyosikia kutoka kwa afisa mmoja, si sera rasmi iliyopitishwa hadharani na serikali.
Ndiyo maana hata katika miaka iliyofuata ratiba hiyo haikutekelezwa kama alivyosema,kwa mfano Lebanon na Sudan hazikuvamiwa.
kusema kwamba kila tukio la vita duniani ni sehemu ya mpango mmoja wa siri wa miaka 20 ni simplification kubwa sana ya geopolitics., unaingia kwenye Conspiracy theory,
Vita vya Iraq 2003, Libya 2011, Syria na vingine vilikuwa na sababu tofauti za kisiasa, kiusalama na kikanda. Hata wachambuzi wengi wa Marekani wanakubali baadhi ya vita hizo zilikuwa makosa.
Hata kama unakosoa Marekani au Israel kuhusu mikataba,ukweli bado ni kwamba nchi hizo zimesaini na kuheshimu mikataba mingi ya kimataifa.
Mfano ni mkataba wa amani kati ya Israel na Egypt ambao bado upo zaidi ya miaka 40, pamoja na mkataba na Jordan. Kama hawaheshimu mikataba kabisa, mikataba hiyo isingedumu kwa muda wote huo.
Kwa kifupi, ni sawa kukosoa sera za Marekani au Israel, lakini kusema kwamba kila kitu kinachotokea Mashariki ya Kati ni mpango wa siri wa kuvamia dunia ni kuleta Conspiracy theory.
Geopolitics ni ngumu zaidi kuliko mnavyodhani ,
Kuna taifa lenye ukandamizaji wa haki kama hao Iran ?
Sawa.Kilicho wazi ni nini? Unafiki wako na wenzio mnaoona ni halali kwa Marekani na Israel kuishambulia Iran?
Hivi vyombo vya New York Times,Hindustan Times ,Times of India unavyozani hawana hao wataaalam wa Geolocations?Kuwa mwanajeshi wa zamani hakumaanishi kila analosema leo ni ukweli wa mwisho,ndio tuhitimishe ni 100%.
Ndiyo maana hata kwenye masuala ya vita wachambuzi huwa wanalinganisha maoni ya watu wengi na data huru.
Kumbuka pia Scott Ritter ni mchambuzi mwenye msimamo wake wa kisiasa na mara nyingi amekuwa na maoni tofauti na wachambuzi wengine wa kijeshi wa Marekani na Ulaya.
Hilo si kosa, lakini inaonyesha kwamba maoni yake ni mtazamo mmoja, sio lazima yawe consensus ya wataalamu wote.
Halafu kuhusu satellite images, hakuna mtu anayekataa kuziona.
Tatizo ni kwamba kwenye vita picha nyingi za satellite hutolewa bila context au verification. Ndiyo maana wachambuzi wa OSINT hutafuta kwanza geolocation, tarehe ya picha na uthibitisho kutoka vyanzo tofauti kabla ya kusema tukio fulani limethibitishwa.
Kwa hiyo hoja yangu ni rahisi, unaweza kuleta satellite images au report yoyote, lakini ili ithibitike lazima ithibitishwe na vyanzo vingi vinavyojitegemea, sio mtu mmoja, media moja au nchi moja.
Hivyo ndivyo uchambuzi wa kijeshi unavyofanywa duniani.
Trump anaomba msaada kwenye Strait of Hormuz wakati vita kaianzisha mwenyewe.Sikutegemea US na Israel wangekuwa wepesi namna hii.
Trump anawaomba UK wamsaidie kupitisha mafuta Strait of Hormuz.
Chanzo cha habari BBC Jioni hii.
Funny π.
Marekani na Israel wakifanikiwa, basi Iran itatumbukia kwenye matatizo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe halafu walioanzisha hayo madhila watakimbia na kuwaacha Wairan wauane wenyewe kwa wenyewe.Watu wengi tunafurahia USA na Israel wanavyomchangia Iran ila hatutaki kujua sababu ni nini. Anachokifanya Marekani kwa Iran amewahi kukifanya kwa nchi nyingine nyingi tu na matokeo hayakuwa kuwa mazuri kwa ubinadamu. Kwa mtu anayetafakari kwa kina, sidhani kama kuna la kujivunia kwa ubabe wa marekani kwa mataifa mengine.
πHadi sasa kila kitakachosemwa kuhusu Iran ni uongo na kuhusu Israel na US ni ukweli hata kama ni maandishi machache na emoji za Ving'ora hahaha
Watasema ni Ai π€£π€£Sikutegemea US na Israel wangekuwa wepesi namna hii.
Trump anawaomba UK wamsaidie kupitisha mafuta Strait of Hormuz.
Chanzo cha habari BBC Jioni hii.