Ni uongo kuwa Iran aliangusha F-35!!!!
Kwanza tambua kilichawapeleka huko Iran si Mlango bahari wa Hormuz kwa hiyo hiyo si kigezo kwao hayo ni mawazo yako wewe!!
Tambua hili kwanza marekani waliondoa askari wao huko kwenye gizo base walibaki tu labda walinzi wa kulinda mali kidogo iliyoachwa!!
Nashangaa unapotafuta udhaifu wa Marekani kwenye sehemu ambayo aliwaondoa askari wake.
Kama mnatafuta udhaifu wa Marekani anazo meli-vita nyingi sana huko Mashariki ya kati zamisheni moja hapo ndipo tutajua udhaifu wake.
Kama mnataka kuona udhaifu wa marekani nendeni huko Marekani mkamtoe Maduro gerezani!!!
Kuhusu mabomu yanayorushwa Israel mengi ni Craster-bombs ambayo ni kinyume kutumiwa ambayo mengi yanapopolewa hukohuko angani hivyo kuyamalizia nguvu,
Asilimia kubwa ya mabomu ya Iran hupopolewa na mengine huangukia sehemu za wazi na ndiyo maana hakuna madhara makubwa kama wewe unavyokaririshwa na video za AI.
Kinachonishangaza wewe huoni madhara anayopata Iran kwa miundombinu yake kuangamizwa kila uchao na mashambulizi ya ndege-vita za Israel!! Wala hushangai kutokuziona ndege-vita za Iran zikililinda anga la nchi yao!!!
Wala hushangai kwa nini Marekani na Israel waliweza kuwafuata marubani wa ndege-vita ya Marekani F-15 E kuwaokoa na wakaondola nao hilo hushangai na huoni kuwa huo ni udhaifu wa IRGC na mifumo yake ya ulinzi wa anga? Sasa nimeamini wahenga walichokisema Nyani haoni kundule